Kama umewahi kupona maumivu ya misuli, mishipa, magoti na kiuno kwa njia asilia, naomba msaada

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
127
62
Tafadhali naomba unijuze

Ili kupona ulitumia mimea ipi

Kwa kiasi kipi

Na matokeo ya kupona hilo tatizo yalitokea ndani ya siku ngapi?

Na huo mmea unapatikana mkoa upi,wilaya ipi,au maeneo yepi?
 
Mkuu Mimi nilishapata maumivu ya kiuno, hadi miguu, nikashindwa hata kutembea kwa siku kadhaa.

nakusihi usifanye chochote cha operation au kingine kwenye mwili wako.

Nenda hospital watakupa dawa za antibiotics na za kuzuia maumivu.

Pata muda mwingi wa kupumzika.

Utakuja kunishukuru.
 
Kupona kwa hayo maumivu kwa namna uliyosema inategemea na chanzo/aina ya hayo maumivu. Mfano kama ni aina ya magonjwa ya athritis ni changamoto kidogo.

Ila kama yanahusiana na labda aina ya kazi au lifestyle yanaweza kuondolewa kwa kuchukua mfumo bora wa maisha kwa mfano mapumziko ya wastani wa masaa 8, kulalia au kuegamia, magodoro rafiki ya mgongo na mifupa (orthopaedic matress), au godoro gumu, vyakula vya kuimarisha mifupa na uroto, mazoezi ya yoga, mavazi yenye kurekebisha mkao wa mifupa n.k

*Kuna kazi hatarishi kama udereva, kazi za kukaa muda mrefu labda ofisini, kazi za kusimama muda mrefu mfano viwandani, kazi za ubebaji vitu vizito, vilalio visivyofaa, n.k
 
Arthritis ni kubadili mfumo wa chakula tu, kunywa maji ya kutosha kwa siku at least Lita tatu uwe umepiga. Ila maumivu ni makali yamenikuta sana we tumia dawa za kuua maumivu kama Cataflam au Diclopa MR hizo ukipiga ndani ya lisaa unakuwa poa kabisa ndio inakuwa maisha yanaendelea otherwise hayo maumivu ni zaidi ya kutahiriwa kwa kisu mzee kwa sisi tuliopita huko tunajua maana huwezi hata kunyanyua mguu au kuutingisha tu.
 
Binafsi hii hali iliniisha nilivyobadili lifestyle, vyakula na hatimaye kupungua kilo kadhaa za mwili.. Nilikuwa slightly overweight na toka nilivyorudi kwenye normal weight Yale maumivu siyapati tena..

Pia nimejifunza kunyanyua vitu Kwa kutegemea zaidi miguu na mikono bila kuinamisha Mgongo.

images.jpg
 
Kama juma moja lililopita nilipatwa na maumivu ya kiuno nilikuwa najikanda na kujichua nashukuru najisikia vizuri
Nalog off
 
Back
Top Bottom