Kama umetoka mkoani kuja Dar kutafuta maisha, tulia nikupe siri ili utoboe

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,696
36,083
From my experience nitaweka vitu viwili vitatu vidogo ila ni muhimu sana kwa watafutaji tuliotoka mkoani kuja Dar kutafuta maisha.

Maisha popote pale yapo na yanaweza kukunyookea. Ila vijana wengi tumekuja Dar kwasababu mbalimbali. Dar es Salaam ni rahisi kupata fedha kuliko mkoa wowote Tanzania.

Mambo ya kuzingatia unapofika Dar kutafuta maisha ni haya;

- Chagua marafiki wachache sahihi, usiwe na marafiki wengi.

- Usikae kwa ndugu au rafiki kama una uwezo wa kupanga na kujilipia kodi(Usipende kitonga).

- Weka pembeni tabia ya ulevi na uzinzi au uesharati. Achana na starehe zisizo na ulazima kama disco na visherehe vya watoto wa mjini vi birthday party, sijui kuvalishana pete beach n.k.

- Aibu weka pembeni kwenye utafutaji.

***** Kuwa mwaminifu******

- Kumbuka Dar ina kanuni ya Natural selection, tambua kuna kipindi kigumu kitakujia (sio lazima) ambapo hata buku mfukoni itakupotea. Hapo ukianza kuomba nauli urudi kwenu umekwisha na utakuwa ulikuja Dar kutalii tu, utaichukia Dar mpaka uzeeni.
 
Pambana sana na Fanya kazi kama mtumwa ili baadae uje uishi kama mfalme hata kama sio kama mfalme lakini basi angalau uwe na unafuu mkubwa wa maisha, achana na aina zote za starehe ana anasa mda huu bado unatafuta utazifanya baada ya kuwa umefanikiwa ila kwa mda huu jinyime kwa mda ukifika utafanya tu acha haraka

Mali au maisha mazuri yanatafutwa na hakuna kisichowekana kila unachokiona hapa Duniani kimetafutwa mpka kikatokea au kupatikana kwa iyo usikate tamaa ni kweli kuna watu wana mali za kuridhi ila sio wote kuna watu walizaliwa kweny family maskini sana ila wamepambana mpaka wametoboa tundu.. Kuzaliwa ktk family masikini sio tatizo ila tatizo ni ww kufa ukiwa bado na fukara na masikini wa kutupwa ilihari una viungo vyote yaani sio kirema

Pia kubali kuchekwa na watu wa mtaani kwako na kuitwa majina ya kila aina hasa wanaokufahamu kwa kazi unayoifanya au lifestyle yako mfano kutokuwa mtu wa kupenda anasa, starehe, kuwa msiri wa ndoto zako sio kila mtu utamuambia wengine watakukwamisha maana kuna watu hawatak kuona wengine wanafanikiwa, nifanye huna malengo na hauko serious na maisha hasa wakati wa kupiga story uwe mtu wa kuponda mafanikio na badaka yake ushauri na uonekane ni mtu wa starehe, tungi, madem nk kwamba mafanikio unayapenda ila haiwezekani kifanikiwa ikiwa hata kwenye uko wenu hamna aliefanikiww hata kumiliki pikipiki mnaishia kweny baiskel tu.

Kuna watu hata ukiwa na bidii ya kazi tu watakusema eti ww jamaa mbona hupumziki huna weekend ww na kazi tu umetumwa na ukoo??!! Wew huna dem au ni hanithi nk yaani ni mengi ilimradi tu wakutoe kweny njia.. We komaa tu nakuahidi kuna siku watakuita mchawi kwa kuwa umefanikiwa wakati wao bado hawana kitu na wakat ulikuja mjini ukowakuta wao ni maaruwatani..




Kuliko kukaa kwa ndugu bora ukae getho yaani chumba muwe watu hata wa3 ila usikae kwa ndugu coz utakuwa huna bidii wala haraka ya kumbana kiatafuta vyako unaona kama maisha umesha yapatia ilihali bado ila unaweza kukaa ikiwa unaweza kujisimamia mwenyewe au kwa mda fulani tu ukishapa pa kuanzia unasepa zako kujitegemea, ukiwa unajitegemea kwa kila kitu utakuwa na bidii ya kupambana ili utoke kimaisha kuliko ukiwa una kaa kwa mtu ni wachache sana waliokaa kwa ndugu ambao wametusua kimaisha, unakuwa huna mtu wa kumtegea Mana ww ndo baba na ndo mama..

ngoja niishie hapa niache na wengine wachangie kila nilichokiongea hapa nmekiishi na ukweli nmeona mabadikiko ktk maisha yangu now niko poa sio haba .. Kutoka kuwa machinga wa kutrmbeza vitu mitaani kwa mda wa miaka 4 na kukaa getho mtu 4 na baadae nikapata mtaji nikafungua kiduka kikachanganya na kuwa duka na sasa namiliki mjengo wangu wa room 3 jijini dar mitaa ya tabata kinyerez, kiwanja tu nilinunua 8milion, pia nimeweza kusomesha mtoto kweny shule za English medium mpaka amemaliza darasa la 7 mwaka huu. Yote haya nmewiwa kuyasema hapa sio kuwatisha watu wala kuonekama no bali kuwatia hasira na moyo wa wengine kupamba maana inawezekana.
 
Kwani ukikaa kwa ndugu, halafu hiyo hela ya kulipia pango ukafanya saving haiwezekani wandugu?
Nakubaliana na mengine ya jitihada za kukomaa kutafuta.
Mkuu acha ubishi ila ukweli ndo huo hata kama ni mchungu lazima tuuseme ukikaa kwa ndug huwa unajisahau na kuridhika wala hutapambana sana na kufanya kazi kwa bidii ni tofaut na mtu anaehitegemea mwenyewe mda mwingi utakuwa unashinda na remot ya tv ana radio na kuwa kama mzawa wakat ww niwakuja na unatakiwa utafute vyako watu wanao kaa kwa ndug ni wachache walio fanikiwa.. We endelea kukaa kwa ndugu tu ila faham hayo hatukatazi wala kuzuia watu kukaa kwa ndug zao bali tunawashauri usikae kwa mda mrefu kaa kwa mda fulani kila kajitegemee
 
From my experience nitaweka vitu viwili vitatu vidogo ila ni muhimu sana kwa watafutaji tuliotoka mkoani kuja Dar kutafuta maisha.

Maisha popote pale yapo na yanaweza kukunyookea. Ila vijana wengi tumekuja Dar kwasababu mbalimbali. Dar es Salaam ni rahisi kupata fedha kuliko mkoa wowote Tanzania.

Mambo ya kuzingatia unapofika Dar kutafuta maisha ni haya;

- Chagua marafiki wachache sahihi, usiwe na marafiki wengi.

- Usikae kwa ndugu au rafiki kama una uwezo wa kupanga na kujilipia kodi(Usipende kitonga).

- Weka pembeni tabia ya ulevi na uzinzi au uesharati. Achana na starehe zisizo na ulazima kama disco na visherehe vya watoto wa mjini vi birthday party, sijui kuvalishana pete beach n.k.

- Aibu weka pembeni kwenye utafutaji.

***** Kuwa mwaminifu******

- Kumbuka Dar ina kanuni ya Natural selection, tambua kuna kipindi kigumu kitakujia (sio lazima) ambapo hata buku mfukoni itakupotea. Hapo ukianza kuomba nauli urudi kwenu umekwisha na utakuwa ulikuja Dar kutalii tu, utaichukia Dar mpaka uzeeni.
Acha uoga wewe sehemu za kula bata ndiyo kuna mishe kubwa kubwa Ukimiliki demu mkali anakufanya kufikiri kwa kasi maana ukilegea unaporwa hivyo itakufanya kumiliki pesa muda wote.
Kama huendi club unatafuta pesa ya mini.
Acha ujinga basi. Hunywi pombe, huendi club, huna Demu, hupendi Mpira,marafiki zako wapo Kama were, huli pilipili, hata bhangi huvuti kufanikiwa sahau maana michongo inapatikanahuko
 
Back
Top Bottom