Kama umepitia Msingi na sekondari pita na hapa pia.

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
Kipindi tukisoma msingi na sekondari tuliimizwa sana kuifahamu lugha yetu vyema pengine na bakora zilikuwa zikitembea lakini yote hiyo ni kukufanya uelewe. Ukijiuliza namna ulivyokuwa ukijifunza juu ya misemo (nahau,methali na vitendawili) na kukumbuka baadhi ya misemo uliyokuwa ukilazimishwa kuikariri au kuifahamu nadhani unatabasamu mwenyewe.

Misemo hiikipindi cha sasa unaona umuhimu wake baada ya kuinukuu katika maongezi yako sehemu mbalimbali. Hata mi nimeinukuu sana hata kipindi namtongoza shemeji yenu lakini sitaki kuwaambia nilinukuu misemo gani. Leo nataka tufanye kale ka mchezo ka mwalimu na wanafunzi ka kuimba table ambapo ukishindwa wakutana na vifinyo au ruler ya kichwa. Tutajikumbusha misemo mingi ambayo tuliwahi kufundishwa au kuijua kutokana na sehemu tulizokaa.

Najua wengi wametoka kula sasa ili usingizi usikupate changamsha ubongo hapa weka msemo (nahau, kitendawili na methali) atakae toa post baada yako atajibu tukishindwa tutampa mchumba kutoka humu humu JF tukikosa basi tutamtafutia kutoka nje na zaidi tunaweza mpa mji akapumzike honeymoon.

Usi-google tumia kumbukumbu ya bongo yako tu...
Ngoja nianze mimina kwa sababu naanzisha nitauliza tatu kwa mpigo,
  • Kombe ya Sultani i wazi (Kitendawili)....................
  • Kupigwa Kalamu (Nahau)............................
  • Jino la pembe (Methali) .........................................
 
Nahisi hapa tutakutana wachache sana, nadhani wengi walisoma Cambridge schools..
 
Kisima cha bibi kimejaa ndago ...... (Kitendawili)

Kozi mwana mandanda ..... (Methali)

Mkono wa birika ..... (Nahau)
 
Priiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mpaka maka
 
Back
Top Bottom