Kama umejiunga na matawi ya CCM USA unaweza kunyimwa Green Card na Uraia Kisheria!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,598
8,738
Kama umejiunga na CCM hapa marekani na ukitaka kuchukua Green Card au uraia na ukasema ukweli kwenye swali hili hapa.

Je umewahi kujiunga au kusaidia chama chochote cha ki communist au socialist na jibu la ko likawa ndiyo basi hupewi uraia au green card. Kuna wacuba wachache ambao wanaachiwa kwasababu walikuwa kwenye serikali ya Castro lakini si sasa bali ni zamani na ni lazima wathibitishe walilazimishwa. Kwa wa cuba inakuwa rahisi kwasababu wengi ni wa Kimbizi.

Kama unakubaliana nami kwamba CCM ni chama cha ki socialist badi kaa chonjo au achana na vyama vya kudakia hiyo member list ikienda kwenye mikono ya serikali umekwisha labda uwe raia wa Marekani! lakini kama unaomba kaa chonjo ndugu
 
Wewe ulishapeleka maombi yauraia wa marekani?

Maana nasikia maswali hayo ni kwa wale wanaoamua kuukana uraia wa kuzaliwa na kuamua kukubali kuvikwa koti la uraia wa kuasiliwa.
 
Ina maana ukitaka kuwa Mmarekani lazima uwe na imani ya kihafidhina (conservative)? Sasa huo uhuru wa mawazo , kujieleza na kujumuika tunaoimbiwa kuwa ndiyo 'values' za Marekani uko wapi?

Lakini hivi ni deal kuwa Mmarekani hata kama huna la maana unalolipata zaidi ya kubeba mabox na kupata hela ya pango la nyumba? Someni, pateni taaluma, rudini nyumbani.

Opportunities kibao kama unaongeza na za kwako za mbayuwayu.
 
Wewe ulishapeleka maombi yauraia wa marekani?

Maana nasikia maswali hayo ni kwa wale wanaoamua kuukana uraia wa kuzaliwa na kuamua kukubali kuvikwa koti la uraia wa kuasiliwa.

Mzee, umeambiwa hata green card ni tatizo kwa wana CCM!!!
 
Ina maana ukitaka kuwa Mmarekani lazima uwe na imani ya kihafidhina (conservative)? Sasa huo uhuru wa mawazo , kujieleza na kujumuika tunaoimbiwa kuwa ndiyo 'values' za Marekani uko wapi? Lakini hivi ni deal kuwa Mmarekani hata kama huna la maana unalolipata zaidi ya kubeba mabox na kupata hela ya pango la nyumba? Someni, pateni taaluma, rudini nyumbani. Opportunities kibao kama unaongeza na za kwako za mbayuwayu.

Halafu akirudi bongo utampa ki-note kwenda kwa bosi mwenye maamuzi ampe ajira?
 
Back
Top Bottom