Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Hebu akilini mwako jenga picha ya mtu aliyeamka asubuhi akapiga mswaki wa mti kwa kutumia povu la sabuni ya kufulia kama dawa yake ya meno, ndani kavaa underwear aina ya VIP, shati la kuvutika, suruali buga, viatu vya laizon huku anakunywa hiyo chai ya sukari ya kuunguza!
 
Nkikumbuka hayo maisha sometime huwa machozi yanantoka tu.
Juzi kati majani ya chai yalikuwa yameisha ofisini kwetu so nkawaambia wale wafanyakaz wenzangu masista duu "chomeni sukari fasta tupate chai njaa znatuuma" huwezi amini hawajui kitu kuhusu hii sayansi....
Mama zetu walifanya kazi sana.
Kuna kuchoma sukari
Na kunywa chai isiyo na sukari

Yaaani maziwa yanawekwa kwa mbaaali na majani ya chai yale ya kupima manene manene bila sukari.
 
Hebu akilini mwako jenga picha ya mtu aliyeamka asubuhi akapiga mswaki wa mti kwa kutumia povu la sabuni ya kufulia kama dawa yake ya meno, ndani kavaa underwear aina ya VIP, shati la kuvutika, suruali buga, viatu vya laizon huku anakunywa hiyo chai ya sukari ya kuunguza!
Huyu muhenga si wa nchiiii aseee
 
Balaa....ila tulizoea tu
Tisa kumi nkaenda Kusoma chimala,mbeya,shule ya Msingi nkakaa na familia fulani wao wasabato chai Yao walikuwa wanachemsha juisi ya chungwa tu,manani ya chai Kwao mwiko,Hata soda pia nooo....
Wengine tumepitia mchanga wa chuma Nahsi ndomana tumekuwa manunda mkuu

Ova
Chimala nyumbani kabisa
 
Huu utaalamu ndiyo nausikia kwa mara ya kwanza, ila iliwahi kutokea nikasahau kununua majani ya chai mimi hupenda kununua vitu in bulky halafu unasahau kwa kipindi kirefu bahati nzuri ilikuwa Jumamosi nikachepuka dukani haraka haraka maana mie bila chai ya uhakika kama breakfast siku haiendi kabisa.

Kwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kunywa chai ya kuunguza sukari kama majani ya chai tukutane hapa.

Chai ile ilikuwa inatengenezwa kwa kuchukua Sukari unaiweka kwenye sufuria iliyopo motoni baada ya hapo sukari itayeyuka na kuungua kidogo alafu unachukua maji unaweka basi kitu kinakuwa Cheusi kama umeweka majani ya chai na ilikuwa tamu tu.

Kama ulishawahi kunywa hiyo chai kweli udogoni mwako au ata sasa hivi basi utakuwa umepitia maisha halisi ya mtanzania.

Tuambie hapa kama wewe ulishawahi kuinywa na inakukumbusha wapi kipindi hicho.!?

.
 
Ndio, ilikuwa sukari inaunguzwa inapatikana chai maridadi sana
kisha unapaka sabuni mwilini yaani mbadala wa mafuta
safari ya shule inaanza. Mimi mara moja moja huwa nafanya mpaka leo
huwa unafanya mpka leo aiseee ..ckuwezi mkuu
 
Chimala nyumbani kabisa
Ohhk nmelima sana mpunga mkiwa darasa la tatu hapo,hapo chimala unapajua wa mjerumani walikuwa wanamuita,nmekaaa pale ulikuwa unaingiaa ndani kidogo.....shule ya chimala Msingi nmesoma....hapo
Unakufahamu pale kwenye uwanja wa helikopta ya kajima .......jirani na hapo
Hivi ile hospital ya mmarekani bado ipo hapo

Ova
 
Huu utaalamu ndiyo nausikia kwa mara ya kwanza, ila iliwahi kutokea nikasahau kununua majani ya chai mimi hupenda kununua vitu in bulky halafu unasahau kwa kipindi kirefu bahati nzuri ilikuwa Jumamosi nikachepuka dukani haraka haraka maana mie bila chai ya uhakika kama breakfast siku haiendi kabisa.

Mkuu utakuwa ulipitia kwenye maisha safi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom