Mwanamboka
Watoto wa miaka ya 90 hamtaelewa kitu. Tushukuru Magufuli ana mpango wa kuleta treni mpya. Nchi ikikosa treni ni afadhali tu irudi kwenye stone age (zama za kutumia mawe)
Hmmnn!Baada ya kumaliza likizo ya form one (nyumban Shinyanga alipozaliwa Kanumba, Noorah mzee wa Icecream, Johari muigizaji, Andrew Chenge na Hayati Bob Makani)
Basi nikamuomba dingi nauli ya treni (ilikua 5000 kutoka Shinyanga mpaka Tabora).
Khaaa dingi akasema hana hela, nisubiri next week. Nikaona ananizingua.
Mfukoni nilikua na 3500.
Nikasema mi Mboyzia bana (waliosoma Tabora Boys alikosoma J.K.Nyerere, Samuel Sitta, Mukandara, Zitto Kabwe, Joshua Nassari) wanajua nini maana ya neno Mboyzia.
Basi nilikua na hamu ya kuwahi Boys kwenda kuwaonea ma form nyoya wapya, usiku ule nikatoroka home na begi langu.
Huyooo mpaka stesheni. Ngoma tano usiku Gogo la kutoka Mwanza hili hapa.
Bila ajizi, kama mshale vile nikadandia behewa limeandikwa herufi F ubavuni (kwa chaki).
Kufika maeneo ya Tinde Tiitii akapita kukagua tiket.
Mboyzia nikatoa 3500 Mfukoni na excuse kibao juu, nawahi shule, baba kafariki, sina msaada.
Kubabake yule Tiitii alikua bandidu kishenz.
Akanikomalia dogo ongeza hiyo jero, umeificha sio??? La sivyo nakushusha.
Ebana eeeeh...
Kufika stesheni ya Bukene nikashushwa kweli... Niliangua kilio pale usiku wa saa nane (mpaka Makamasi) Tiitii akanihurumia, kabla Gogo halijapiga kipenga akaniambia "Panda dogo kuna wachawi hapa, siku nyingine usirudie"
Sitosahau kwa kweli.
Mtumishi Mcharo