Chee4
Member
- May 17, 2021
- 35
- 125
DAda zangu wa mjini nawapa angalizo, Kama boyfriend wako aliwahi kukuambia kajenga nyumba kijijini kwao ambayo hujawahi kuiona, halafu leo kwa namna yoyote ile umemsikia au umemshudia akilalamika kuhusu kulipa kodi ya majengo kwa LUKU, achana nae, hana nyumba huyo. ALIKUDANGANYA. Kwanini nasema hivi;
Kodi ya Majengo sio kodi mpya, ipo tangu kitambo, mafaza wengi wameshalipa na hawajawahi kulalamika, wengi wanaopiga leo ni wapangaji, HAKUNA mwenye nyumba anaweza kulalamikia Serikali wakati mfumo huu mpya unamrahisishia kero za ulipaji kodi, kutoka Kwenda kupanga foleni Halmashauri siku nzima, hadi kulipa kwa Simu akiwa anakula Katles nyumbani kwake, easy tu yaan.
Inawezekana maneno haya 'kodi ya majengo' ni MSAMIATI mpya kwa vijana wengi waliokimbilia magari na iphone mjini kabla ya kujenga nyumba zao, nashangaa hawa mabrazamen wanatoa wapi ujasiri wa kujadili jambo lisilowahusu, Hili la kulipa Kodi kwa njia ya Luku linatuhusu sisi wakina baba wenye nyumba mjini, nyie wapangaji KAENI KIMYA. Haliwahusu. Nyie ni mamidoman tu.
Kama mnataka kujadili basi njooni tujadili changamoto zake, ambazo kimsingi ni mbili tu, ya kwanza ni Nyumba nyingi wapangaji ndio wanalipa LUKU, sasa kama kodi itakatwa kwenye Luku hatuoni kama wapangaji ndio watakuwa wakilipa Kodi za majengo badala ya wenye nyumba? Changamoto ya pili ni Je kwa nyumba moja yenye wapangaji watatu na luku 3, Kila mpangaji (kila Luku) atalipa kodi ya jengo?
Kwa kuwasadia, hizi changamoto ni ndogo mno ukilinganisha na faida za huu mfumo mpya, Kuhusu nani atalipa Kodi, wewe Mpangaji kubaliana na mwenye nyumba wako, mkatanaje, unaweza ukamkakata elfu 6 ambayo ni kodi ya jengo ya miezi sita, wakati unamlipa hela yake au vyovyote mtakavyokubaliana. kama mwenye nyumba wako hakubali utaratibu wa kumkata kwenye kodi yake, hama kwenye hiyo nyumba, huyo ni TAPELI.
Kuhusu Nyumba moja yenye Luku 3, mwenye nyumba atachagua Luku ipi iwe inalipa kodi ya jengo ya nyumba yake yote (nzima), hamtalipa wote, mpangaji mwenye Luku itakayochaguliwa na mwenye nyumba ndio atakayekubaliana na mwenye nyumba utaratibu wa ulipaji, kama ni kukatana kwenye kodi au vinginevyo.
Sasa mlikuwa tunalalamika nini? Hata kama mna stress za kodi za nyumba mlizopanga, muwe mnatafakari kabla ya kutoa maoni yetu, ANYWAY, siwalaumu sana, siku mkijenga zenu, mtaelewa.
Ahsante TRA, Ahsante TANESCO na Ahsante kubwa kwa Serikali kwa kuturahisishia sisi wenye Nyumba ulipaji wa Kodi ya Majengo, Hakuna kupanga foleni tena.