Kama ulikuwa mpinzani 2015 -2021, wewe ni mwamba na umeyashinda mabaya mengi

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
Kuanzia 2015 mwishoni Hadi 2021 Tulipokuwa tunawaambia TIME WILL TELL mlijua tunajifunza kingereza, we tumwa ukaue, tesa watu, dhulumu watu, shadadia watesi, zarau watu, tukana watu na wafanyie mabaya yote lakini kaa ukijua hiyo nayo ni mbegu ambayo itaota tu, mvua inyeshe au jua liwake itaota tu. Mzee Kikwete aliwai sema "akili za kuambiwa changanya na zako". Mzazi au mlezi akikufundisha kupora haki za watu ujue hakupendi.

Kama uliweza kuwa mpinzani kwa kipindi chote cha Mwendazake hakika wewe ni mwamba na umeyashinda mabaya mengi mno maana waitwao wapinzani walivhukiwa, walitengwa, kuteswa na mabaya mengi bila kosa lakini walivumilia Hadi leo wapo imara.

Kwenye maisha Mambo muhimu ni kuwapenda watu, kuwatendea mema, kupata kipato kwa haki, kuwaheshimu wote, kuwa mwenye hekima, kuepuka dhulma na kumwaga damu za wanadamu wenzio. Hii dunia Ni uwanja wa fujo imetupasa kuwa waungwana nyakati zote .

Kumbuka Hata viungo vya mwili wake vilimkataa na kumsaliti Bi. Kirembwe wa Giningi. Palikua na kijana jina lake Mtolewa katika nchi ya Giningi, huyu alikua mwanaharakati wa Haki za kiraia haswaaaa. Hakuogopa kumkosoa Bi. Kirembwe Wala kuwafungua watu kimawazo.

Bi. Kirembwe alikua Hakimu, Dikteta, mshauri wa mabaya, polisi, magereza, mwanajeshi, Mwalimu uchwara, nesi, daktari, mkulima, Balozi, Rais, Jaji, spika, waziri, jambazi, muuaji, mwigizaji, muongo, mfitini n.k.
Alikua zaidi ya Mungu mtu.

Ndipo Taifa lile lilipata Uhuru baada ya kifo Cha Dikteta Bi. Kirembwe. Ijapokua mwanaharakati na mtafuta mabadiliko kijana Mtolewa alikua ameshauawa na Bi. Kirembwe katika Taifa lake, bado mbegu ya kimapinduzi aliokua ameipanda ilizidi kustawi kwa watu wote.

Hakika Kivuli kinaishi.
Sheria Ni msumemo.

Na
Mwanshinga Jr
 
Bwana Mungu ameweka fundisho kubwa sana kupitia kwa utawala wa mwendazake.

Mwenye akili timamu ya kawaida kabisa anayo mengi sana ya kujifunza.

Muda huongea nyakati zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom