Kama uliipigia Kura CCM basi wewe umelaaniwa katika Taifa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama uliipigia Kura CCM basi wewe umelaaniwa katika Taifa letu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzalendo80, May 15, 2011.

 1. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kama uliwapigia Kura CCM katika Chaguzi zote basi ujue wewe umelaaniwa, watoto na wajukuu zako watakulaani mpaka kufa kwako. Laana zitawatafuna Viongozi waovu kama Kikwete, Lowassa, Chege, Nimrod Mkono, Rostam, Mkapa na Viongozi wengine wote wasio na Mapenzi na nchi yetu Mungu awaangamize wote wanaolihujumu Taifa kwa manufaa yao.
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mzalendo80 umefika mbali sana. Tambua CCM ni chama cha siasa kinachoongozwa kwa kufuata katiba yake ambayo wanachama na raia wengi wa Tanzania waliifahamu (ilikua inafundishwa kama sehemu ya mitaala mashuleni). Imani ya CCM inaeleweka na inatoa matumaini kwa raia. Mambo hayo ya kimsingi yanaweza kumfanya raia kufanya uamuzi wa kuwapigia viongozi wa CCM. Mtazamo wako ulizingatia ukweli huu? Watanzania wanawafahamu viongozi wa Chadema na Vyama vingine vya siasa lakini je wanazifahamu katiba na Imani za vyama hivi kama ilivyo kwa CCM. Tafadhali tafakari bila kujaribu kufikiria mtazamo wangu kisiasa.
   
 3. k

  kiloni JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukweli sijawahi kuifahamu imani na katiba ya CCM. Nilipotaka kuanza kuitafuta na kuisoma nikasikia kuna watu walikaa bila kuwa na hadidu za rejea wakafuta ile sera ya Ujamaa na kujitegemea. Ndipo ukahalalishwa uharamia wa raslimali na UFISADI tunaopigiana kelele sasa.

  Laana itatokana na kilio cha wajukuu kinacholetwa na hayo makubaliano ya kukomba raslimali za nchi hii yaliyofikiwa gizani.
  Laana itatokana na Kukiri matumizi ya nguvu za giza ambazo tumeambiwa kuwa aliyechaguliwa Urais 2010 oktoba anazifaidi. (Kulindwa na majini sita) (source: Sheikh Yahya) Haijawahi kupingwa hii ni laana kubwa.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mkuu CCM imeanza tangu kipindi cha Nyerere ati! chaguzi zipi? tangu ilipoanzishwa au mwaka jana, usije kuta unajilaani bure kupitia wazazi wako!!

  Mwisho tangaza sera , wabadilishe watu kwa hoja, kulaaniana huku hakuna mpango unajidhalilisha
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Taratibu ndugu. Hivi mbona thinking yako iko narrow sana katika thinking yako? Kwa taarifa yako unapotoa laana yako feki, ujue unalaani pia na wale unaowaamini kama wakombozi wako walio ndani ya Chadema maana na wenyewe wamekuwa wanaipigia kura CCM huko nyuma mpaka mfumo wa vyama vingi ulipoingia. Hata huyo Slaa, Mpendazoe na wengi wengine wameguswa na laana zako za kitoto na zenye jazba!
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  A novice in the propoer sense of the word. Kama ameweza kuropoka hivi unatarajia atatangaza sera? Azitoe wapi?
   
 7. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  kumbe kuna vichaa ndani ya jf na vijidicteta uchwara kuipivia kura ccm ndio ulaanike?chama hiki ndicho kilichokufikisha hapo ulipo.kama kuna matatizo basi ni viongozi waliochaguliwa wengine hawana tofaiti na wewe
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Haya yote matokeo ya ufisadi wa kikwete na ccm ndiyo maana watu wamechoka kupita kiasi...........nadhani nchi hii silaha zingekuiwa zinanunuliwa kirahisi k hapo bondeni basi akina rostam wasingekuwa wanapumua kufikia dakika hii
   
 9. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  usiwalaani hivy wapiga kura. ila wambie nafasi zao ziwasute kwa kutufikisha tusipopataka. after all hao waliopigia ccm kura ni wachache sana (27%) na kama ni nguvu za wengi ccm haipo ikulu leo
   
 10. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  jamaa una hasira kichiz,
  itabidi tuunge msafara kwenye opereshen sangara
   
 11. p

  peacebm Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Jan 31, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi walioichagua ccm wanaishi kwa below 1US $ per day mi mwenyewe nawaona hata wale waliopewa T-shirt na kofia za njano na sh 10,000 mwaka jana waipigie ccm domo sasa iv wanapigika kichizi wako hoi, chali, yani its beyond xpression! pale kinondoni tu juz wameanza kumlaumu mbunge wao waliompigia debe watanzania naona wamelaaniwa na akili zao zimeganda au hawa viongozi wanaenda kwa waganga wa kinigeria kuwaloga wapiga kura waooo?
  Nakuunga mkono si kama hao watoto wa mafisadi wanaokukebehi,wakaki mwingine natamani tungeomba Mungu amfufue Nyerere angewafilisi hao mafisadi sio kuwavua magamba!
   
 12. O

  Ombeni Charles Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haaaaa! Hii nayo kali.
   
 13. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waliopigia kura ccm hawakuifanya hivyo kwa sababu ya kusoma na kuelewa sera za chama hicho ila ni kwa sababu ya uoga wa kwamba vyama vya upinzani vitaleta vita kama vikitawala, kura nyingi za ccm ni za wale waliokuwa waliokuwa uninformed kama vile waishio vijijini, vikongwe na kaliba kama hizo. Lakini siungi mkono jazba aliyoionyesha mtoa mada katika andiko lake.
   
Loading...