Kama uliingia kwenye mgogoro na mke, mchumba/mpenzi wako kwa kutomtimizia ulilomuahidi, kuna haya...

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,603
2,000
Habari wanajukwaa!
Katika jukwaa hili mimi si mwenyeji sana licha ya kwamba huwa nakuja kucheki na kujifunza mambo mazuri mara chache.

Katika hali ya kawaida tu , wanaume ndio tunaojibebesha mzigo wa matatizo ya wapenzi wetu, wachumba ama wake zetu zaidi ya wao wanavyobeba mizigo yetu sisi.

Katika kuonyesha upendo wakati mwingine tunaamua kuwapa ahadi kwamba tutafanya jambo fulani juu yao. Wakati mwingine mwanamke anapokushirikisha jambo akiomba msaada wako kama mtu wake wa karibu pia unaweza jikuta unaweka ahadi.

Ahadi hizi mara nyingi tunaziweka huku tukipiga picha mipango iliyopo mbele yetu. Pale inapotokea ile mipango kuharibika, au kutokutimia kwa asilimia mia na mara nyingine linapotokeaa jambo serious zaidi ya tatizo ambalo analo mwenzi wako basi hupelekea ahadi kuchelewa au kuharibika.

Sasa basi ukiona mwanamke ameanza kukasirika, kuropoka maneno ya ovyo au kuonyesha any negative kwako basi ndugu nakuhakikishia kwamba huyo mwanamke ataangukia katika kundi mojawapo au haya yote na hakufai kabisa;

1. Kahaba, mwanamke kahaba huwa hana huruma nawe kwani kwako yupo ili tu apate pesa au jambo fulani tu na si kuwa na future pamoja nawewe.

2. Hana uvumilivu, uvumilivu ndiyo msingi wa mapenzi endelevu. Kama kashindwa kukuvumilia kwa mwezi mmoja au miwili ambayo ungeweza kutatua tatizo lake basi jua kwamba atakusumbua ndani ya ndoa.

3. Yawezekana akawa si kahaba ila yuko kwako kwa lengo maalumu . Yuko tayari akuue mbele ya safari ili tu atimize ndoto yake. Huyu hajakuweka moyoni.

Nina mengi zaidi ila tu ngoja niishie hapa. Kama ukiona huwezi kumwacha mpenzi au mchumba wa namna hii jiandae kuishi kwa hudhuni katika ndoa. Na kama umeshamwoa na umeshtuka sasa basi nichek in nikushauri ila usimwache. Ndoa ni jambo muhimu na takatifu.
 

corasco

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
3,529
2,000
Mwanamke ukiona wewe unamsaidia mwanaume shida zake,we ukamshirikisha zako zaidi ya Mara tatu hajatatua hizo shida,hesabu huna mwanaume muage tu hakufai..mana utavumilia mpaka utachanganyikiwa...ahadi tu kila siku hatimiz.eeh mwanamke ondoka ...
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,603
2,000
Aiseeh! Haya yamenikuta toka juzi tu
Pole, raha jipe mwenyewe, mtafute mwanamke ambaye ni house girl mwandae umwoe. Mwanamke yeyote kama tu si kilema kama akitunzwa na kupendwa ni mzuri sana.
Usikubali elimu au jambo lolote la mwanamke aligeuze kama ndoana kwako.
Wengi wa mahause girls wako katika shiida, ukimtoa katika shiida zake hakika atakukumbuka na kukupenda daima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom