Kama uko Dodoma una laki 6, kila siku nitakuzalishia 10000

Unashindwa nini kuweka hadharani huo mpango ulionao na hiyo hela. Kwamba kuna mtu ataiba wazo lako la biashara ya laki sita?

Unabaki kutia huruma na kupokea maneno makali.
Acha kujibu comment moja moja, eleza mpango ulionao usaidiwe.
Yani unataka msaada halafu hutaki ku-take trouble kueleza huo msaada utautumiaje, yani serious kabisa mimi ndo nikutafute ili unieleweshe namna msaada wangu utakavyokufaa..!!?

Eleza hapa. Mtu anaweza asiwe interested na hizo elf 10 za kila siku ila akajisikia kukupa sapoti utoke. Au ukapewa mbinu yakupata hiyo hela bila kutia huruma kwa watu.

Kuna mengi tuu, msingi ni kuweka mpango wako hapa watu wauone.
 
wewe mwenyew hio laki6 imekushinda kupata, utawezaje kumpa mtu elfu10 kilasiku 😂 utapeli wa kizaman sana...
Njoo Bambalaga au Royal village nikufundishe utapeli wa kidigitali
 
Hiyo biashara ya mtandao sijui jina ila kuna mtu alinidokezea nijiunge chini yake kwa 600k afu kila siku napata 10 kitu kama hicho kwa miezi 6 hivyo nakuwa nimeingiza kama milioni na nusu hivi, (
mambo ya good morning hata kama ni mchana)
Hahah!!!eti good morning....natabiria kuwa walikuwa ni forever living..yaana wanahamasisha uongee english hata kama hujuii...ila sehem walikuwa wananipa raha ni zile semina zao ambapo mseminishaji kakanyaga na kiatu mpk kimelalia upande mmoja ila ushuhuda anaoutoa ni wa mtu anaemiliki miroshen kadhaa...nliona tu huku ni kupigwa nikaamua kuwachana ukwel na kuondoka
 
Weka namba Yako ya simu,kitambulisho au namba Yako ya NIDA,Majina Yako halisi matatu,Picha zako kadhaa Ili watu wa kuamini.... Hahahaha
 
Ask the speaker/Comments (Kwa kiswahili )wasiliana na Spika Ndugai au tuma maoni.
Mkuu ukikosa hapa basi kaoge Maji ya Ubuyu.😎
Screenshot_20210921-003743_Chrome.jpg

 
Natafuta mtu ambae yupo Dodoma, nina biashara atoe laki 6 halafu kila siku atakuwa anapata faida ya 10000, kama upo tayari na una huo mtaji tafadhari tuwasiliane tufanye biashara.

0621604087
Laki sita ipo tena nakurushia kwa mpesa kama utanionyesha vitambulisho vyako... Lakini nipe mpango na mchanganuo wa biashara yako niitathmini kwanza .
 
Natafuta mtu ambae yupo Dodoma, nina biashara atoe laki 6 halafu kila siku atakuwa anapata faida ya 10000, kama upo tayari na una huo mtaji tafadhari tuwasiliane tufanye biashara.

0621604087

Baada ya siku sita. Sikusikii vizuri ngoja nitoke kwenye kelele nitakupigia
 
UPDATE

NAWASHUKURU WOTE KWA MICHANGO YENU YOTE..

TAYARI NIMEMPATA MTU HIVYO SITAHITAJI MTU MWINGINE KWA SASA.. NAWATAKIENI MAJUKUMU MEMA KATIKA UTAFUTAJI WENU
 
Back
Top Bottom