Kama uko Dodoma una laki 6, kila siku nitakuzalishia 10000

Hiyo ni mipango yako mkuu!!, maana mimi siko hapa kutapeli bali kile nilichokikusudia kukifanya biashara na mtu mmoja kwasasa maana soko halijawa kubwa kuhitaji watu wengi uliyowapigia mahesabu wewe... Halafu si vzr kumhukumu mtu kwa hisia zako acha itakusaidia sana na kuepuka mikwaruzano na watu mkuu... Leo hii mimi nikiibuka tu nakusema wewe ni tapeli hutojisikia vzr linda heshima ya watu kama wao wanavyikuheshimu.. Ahsante
Unaitwa tapeli kulingana na unachopost jukwaa la maelfu Kama hili hutakosa wafuasi watatupa mrejesho wa kiontario
 
Kwa kifupi hii ni fursa nzuri sana kuna siku ilikuwa kidogo nitapeliwe kilichonisaidia niliwaza tu kama kuna dili zuri kama hili mtu atamtafuta mtu wake wa karibu kuliko kutafuta tu mtu baki.
 
Hiyo ni mipango yako mkuu!!, maana mimi siko hapa kutapeli bali kile nilichokikusudia kukifanya biashara na mtu mmoja kwasasa maana soko halijawa kubwa kuhitaji watu wengi uliyowapigia mahesabu wewe... Halafu si vzr kumhukumu mtu kwa hisia zako acha itakusaidia sana na kuepuka mikwaruzano na watu mkuu... Leo hii mimi nikiibuka tu nakusema wewe ni tapeli hutojisikia vzr linda heshima ya watu kama wao wanavyikuheshimu.. Ahsante

Nenda NMB au CRDB, utakuta hela zinacheka kule! Huku utaambulia matusi tu maana kila mtu anakuona ni tapeli tu!
 
Ninachoweza kusema kuhusu ni kwamba umasikini ni kitu kibaya sawa, tujitahidi kukifukuza..

Unafukuza umasikimi kwa kuomba upewe 600,000 na kumrudishia ntu 10,000 kila siku, yaani 300, 000 kwa mwezi?? We bwana nenda benki ili ukajikwamue na umasikini huo. Ndivyo tunavyofanya wenzio! Hakuna hela ya mchezo hapa kwenye jukwaa hili! Utaambulia vumbi tu hapa!
 
mara,namba unayoipigia haipo....
Nilimkopesha ndugu WA ukoo kaja ofisini Analia mama MTU mzima anasema ndugu yangu hata mwezi haufiki kuna shamba tunauza. 2019 huyo mama anaonekana Fala huwezi amini akikupa namba Leo baada ya wiki anasajili nyingine. Nikamtafuta Hadi mama yake na yeye nikampa vitisho kuna siku akatuma laki mwaka Jana hiyo kwenye laki 3 nikaokoa laki. Undugu umeisha na iliyobaki nimesamehe maana hata kama Nina Nia ya kumdai hapatikani kwenye simu.
 
Kwa kifupi hii ni fursa nzuri sana kuna siku ilikuwa kidogo nitapeliwe kilichonisaidia niliwaza tu kama kuna dili zuri kama hili mtu atamtafuta mtu wake wa karibu kuliko kutafuta tu mtu baki.
Nina mtoto WA dada ana mtindo huo 'ma mdogo tafuta milioni 2 tufanye ABC 'alishawahi kuniingiza mjini mara moja kuna siku nilimuuliza hivi hizi Taasisi zote zinazokopesha huzioni mpaka uje kwangu? Hajawahi kurudia.
 
"Nipo kwenye kelele subiri nitakupigia baadae" hiyo baadae haifiki mpaka unaamua kutuma text "mbona kimya?" Text haijibiwi

Unapiga tena "haloo nipe mda kidogo namalizia hesabu fulani hapa ndg"

Biashara kama hii nimeshaifanya nikiwa chuo, nilikuwa nikipokea boom silitumii maana nilikuwa na hela za ziada za kutumiwa na ndg jamaa na marafiki nikiwapiga vizinga

Sasa nikatokea kuwa na urafiki na jamaa mmoja wa kiduka cha M-Pesa baadae akadai nimpe laki tatu atakuwa akinipa kila mwezi elfu 50 na pesa yangu ikibaki kuwa pale pale

Nikaona isiwe tabu na kuzingatia nilikuwa na kama mia saba ipo tu sikuwa naziona fursa kipindi kile, si nikampa jamaa

Aisee sio tu hiyo elfu 50 kwa mwezi hata hiyo laki tatu sikuipata, hapa ndio nilijua mahakama haina msaada wowote nilipeleka ushahidi wa kutosha ila hakimu anakuja kutoa hukumu jamaa anilipe milion au aende jela miezi sita kwa utapeli

Jamaa alikuwa na madeni mengi sana biashara yake iliyumba si akaamua kutumikia kifungo, na kashatokaga tayari sasa hivi yupo mtaani na mahakama inajua jamaa kashatumikia adhabu yake ila sasa alipoitumikia hiyo adhabu mimi nilifaidika na nini wakati kanipotezea laki tatu yangu?

Nasema tena hata unipe kila siku milioni kwa kiyo hiyo laki sita sikupiiiiiiiiiii
Narudia tena sikupiiiiiiiiiiii
Pole sana
 
Back
Top Bottom