Kama ukiweza basi utaikomboa pesa yako, hakuna maadili ya kazi kwenye mitandao ya simu kwa sasa

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,207
1,755
Sasa hivi hakuna maadili ya kazi katika taasisi za mawasiliano, na hili halizungumzwi na wahusika.

Ni vyepesi sana kuibiwa simu na sim card zikiwemo, na Kibaya zaidi ukichelewa kurenew ndani ya masaa matano tu, basi hautakuta pesa zako tena ndani ya sim card husika.

Namna ya kushitaki ni shida hakuna ushaidi wowote kwamba haukutoa pesa mwenyewe bali mwizi, hivyo zikishaibiwa zimeibiwa.

Nachojua na kitakacho kusaidia ni wewe kubadilisha mtindo wa maisha yako.

1.penda kutembea na kitambulisho chako cha Taifa ama mpiga kura. Ili kama utaibiwa simu mchana basi fanya juu chini ili kurenew number yako muda huo huo lakini hii bado ni bahati na sibu ila inasaidia.

2. usiweke pesa zaidi ya elfu 50 kama akiba ndani ya sim card, jaribu kuacha bank, kama ikitokea shida ya ghafla unasafirisha pesa kupitia simu banking.

Hata hivyo njia hizi ni sumbufu tu, ila kwa mtazamo wangu naona ni njia bora kwa kuwa wahusika wa mitandao kwa sasa hawana maadili, kuna mtu kaibiwa pesa ndefu na tena town cha ajabu ni kwamba pesa hiyo kakuta Haimo na akienda kwa mtandao husika wanasema amekwisha toa masaa machache yaliyopita na huu umekuwa mchezo wa mjini.

NB: Siwezi kukaa na kuandika vizuri wenye akili wamenielewa, JAPOKUWA NIMEANDIKA VIZURI.
 
Hawawezi wanawezaje kutransfer pesa bila namba ya siri?

Kingsmann

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
“Hata hivyo njia hizi ni sumbufu tu, ila kwa mtazamo wangu naona ni njia bora kwa kuwa wahusika wa mitandao kwa sasa hawana maadili, kuna mtu kaibiwa pesa ndefu na tena town cha ajabu ni kwamba pesa hiyo kakuta Haimo na akienda kwa mtandao husika wanasema amekwisha toa masaa machache yaliyopita na huu umekuwa mchezo wa mjini”

Wahusika wapo kwenye system,na hasa upande wa customer care na kitengo cha ku-activate line pia kitengo cha pesa za kwenye simu,kwamba ukipoteza simu kitendo cha wewe kupiga simu kutoa taarifa amana zako zilindwe hapo hapo unakuwa umejiharibia maana wanakonyezana wanaambiana na wahuni wao huko mitaani faster wanafanya yao.

Ukitaka kuwa salama pale ukipoteza simu yako tu bora usitoe taarifa yoyote zaidi fuatilia taratibu za kawaida police za ku-renew lain taarifa kwamba ulipoteza line yako wafanyakazi wa mtandao husika watazijua pale umeenda ofisini kwao kutaka form ya kujaza upate line yako wakijua kabla imekula kwako.
 
nadhani kuna haja ya kurudhisha ule utaratibu wa kuwasilisha nyaraka binafsi wakati wa kutoa pesa kwa wakala.

kuanzia elfu 10 tunataka kitambulisho kinachowiana na jina lako la kwenye muamala,la sivyo wakala awe anakutambua.

kuna uzi humu mdada wakala katapeliwa pesa kwenye line binafsi,na tapeli likapiga simu kugeuza muamala,kwahiyo wakala yule line zake zimezuiwa na mpaka alipe pesa ambayo hakuipata.
 
“Hata hivyo njia hizi ni sumbufu tu, ila kwa mtazamo wangu naona ni njia bora kwa kuwa wahusika wa mitandao kwa sasa hawana maadili, kuna mtu kaibiwa pesa ndefu na tena town cha ajabu ni kwamba pesa hiyo kakuta Haimo na akienda kwa mtandao husika wanasema amekwisha toa masaa machache yaliyopita na huu umekuwa mchezo wa mjini”...
Inasikitisha kwakweli

Kingsmann

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
nadhani kuna haja ya kurudhisha ule utaratibu wa kuwasilisha nyaraka binafsi wakati wa kutoa pesa kwa wakala.

kuanzia elfu 10 tunataka kitambulisho kinachowiana na jina lako la kwenye muamala,la sivyo wakala awe anakutambua.

kuna uzi humu mdada wakala katapeliwa pesa kwenye line binafsi,na tapeli likapiga simu kugeuza muamala,kwahiyo wakala yule line zake zimezuiwa na mpaka alipe pesa ambayo hakuipata.
Hii itasidia sana,sijui ninani aliyetoa utaratibu huu
 
Back
Top Bottom