Kama ujumbe kwenye kamati tu imekuwa kimbembe, vipi Zitto angeteuliwa Waziri?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Kama ujumbe kwenye kamati tu imekuwa kimbembe, vipi Zitto angeteuliwa Waziri?

Na Charles Charles

NOVEMBA 13, mwaka huu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitimiza ahadi ya kuunda Kamati ya Madini ili pamoja na mambo mengine, ipitie sheria na mikataba ya sasa katika sekta hiyo muhimu kiuchumi popote duniani.

Akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ukumbi wa Kizota, nje kidogo ya mji wa Dodoma, Kikwete aliahidi kuwa kamati hiyo ingejumuisha wajumbe kutoka sekta tofauti nchini wakiwemo wapinzani kwa vile suala hilo linahusu maslahi ya nchi na siyo ya vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, kuteuliwa kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe kuwa mmoja kati ya wajumbe 12 wanaounda kamati hiyo si tu kwamba kuliibua malumbano mazito katika chama hicho, lakini pia alituhumiwa kuwa msaliti na kibaraka wa CCM.

Waliokuwa “wameshika bango” zaidi ni Mbunge wa Tarime ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Mara, Chacha Zakayo Wangwe na mwanasheria wa chama hicho aliyegombea ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kusambaratishwa vibaya na CCM, Tundu Lissu.

Wote katika ujumla wao walikuwa “vinara” wa kampeni ya kupinga uteuzi wa Zitto kwa kutaka asiwe Mjumbe wa Kamati hiyo bila hoja zilizosheheni hoja!

Kwa mfano, wakati Wangwe alinukuliwa na vyombo kadhaa vya habari akimshutumu Zitto kwa kumsifu Kikwete kwamba ni Rais makini na hivyo kudai “amenunuliwa”, Tundu Lissu alikuwa aking’ang’ania kuwa kamati hiyo haina nguvu za kisheria utadhani imeundwa ili kuwachunguza, kuwakamata, kuwashtaki na hatimaye kuwahukumu watu kufungwa jela!

Hata Mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo (CHADEMA) naye alikaririwa kutokubaliana na kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Kwanza Mzalendo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Mark Danhi Bomani akidai inapaswa iundwe na chombo kama bunge na siyo mamlaka nje ya hiyo.

Msimamo huo wa Lyimo pia ulielezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu wakati akiwa Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Victor Kimesera akisema “bunge ndilo lilipaswa kuunda kamati hiyo kwa kuwa ingepata nguvu ya kisheria”.

Viongozi hao waandamizi wa CHADEMA walikuwa pia wakienda mbali zaidi na kufikia mpaka hatua ya kumtaka Zitto atoke katika chama hicho na kuhamia CCM.

Akionekana kuyumba na kuungana na jopo hilo lisilokuwa na hoja madhubuti, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Peter Slaa naye alikuwa akiunga mkono harakati za kutaka Zitto ajiuzulu uteuzi wa Rais, wito ambao Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini aliujibu kwa msisitizo kwamba asingefanya hivyo.

“Sitajitoa kwenye kamati (hiyo). Nitaendelea kushikilia msimamo huu (isipokuwa) labda Rais (mwenyewe) anifukuze”, alisema Mbunge huyo wakati akizungumza na gazeti moja la kila siku.

Kila aliyewahi kuhudhuria angalau mkutano mmoja tu wa hadhara uliohutubiwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA hususan kuanzia Agosti hadi Septemba, mwaka huu, ni dhahiri kuwa alisikia fitina za sheria na mikataba ya madini zilivyokuwa zikichongwa majukwaani.

Kilichokuwa kikizungumzwa sana ni madai kuwa raslimali za taifa na hasa madini kama vile dhahabu, tanzanite, almasi na mengine mengi yamekuwa yakiporwa na wawekezaji wa kigeni kutoka nje ya nchi, na kwamba adui mkubwa wa Watanzania ni CCM na serikali yake iliyotunga na kuweka sheria na mikataba mibovu katika sekta hiyo.

Kikwete ambaye siku zote ni kiongozi mwenye tabia ya usikivu kwa matatizo na matakwa ya Watanzania alisikia kilio hicho na kuamua akitafutie ufumbuzi wa kudumu kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Sitaki niamini kuwa viongozi wa CHADEMA walipokuwa wakilipigia kelele sana suala hilo mikutanoni walikuwa “wakiwatapeli” wananchi, kwamba mioyo yao ilikuwa haimaanishi kile wanachotamka midomoni isipokuwa shida yao kubwa ilikuwa ni kutaka washangiliwe kwa makofi na miluzi na kuishia hapo.

Ni vigumu kwa mfano kumwamini tena Tundu Lissu wala Dk. Slaa waliokuwa wakijifanya wana uchungu mkubwa na raslimali za nchi yetu na kufikia mpaka hatua ya “kuwapakazia” watendaji kadhaa wa CCM na serikali kwa ufisadi, lakini leo inapotafutwa “dawa” ya kutibu maradhi waliyodai yanaiangamiza Tanzania wanachachamaa na kupinga jambo hilo kwa kutaka lisifanywe.

Kamati ya Madini iliyopewa miezi mitatu iwe imemaliza kazi iliyoagizwa kuifanya imeundwa ili kusaka “dawa” ya kutibu majeraha ya uchumi wetu, hivyo haieleweki kwa CHADEMA inaposhirikishwa kwa mwanachama wake kuteuliwa kuwa mjumbe inakuwa “issue” inayotishia amani.

Jambo lililoshangaza wengi ni uteuzi huo wa Zitto kukaribia kukisambaratisha kabisa chama hicho utadhani cha waganga wa mitishamba au wapiga manyanga hadi ikabidi iitwe Kamati Kuu ya dharura kuzungumzia suala hilo tu.

Kila wakiambiwa vyama vyao ni vichanga vinavyopaswa vipewe muda zaidi wa kujifunza utawala na uongozi, wapinzani nchini wamekuwa waking’ang’ania kutoa kauli za “kitoto” wakidai wanaweza wakati “hakuna kitu kabisa”.

Lakini kwa vile Mungu hamfichi mnafiki popote alipo, uteuzi wa Zitto kuwa Mjumbe wa Kamati ya Madini tu hatimaye umedhihirisha ukweli kuwa bado ni wachanga kupita kiasi.

Kwa mfano, kama wapiga kura mwaka 2005 wangedanganyika na magwanda ya khaki na mbwembwe za “hakuna kulala mpaka kieleweke” na kuikabidhi nchi yao kwa CHADEMA bila shaka wangeona maajabu ya firauni!

Mbowe ambaye angeapishwa kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne huku Anna – Maulida Komu aliyekuwa mgombea mwenza wa kiti hicho akiapishwa kuwa Makamu wa Rais, Tanzania ingesambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo wakati wa kuteua Mawaziri na hasa Waziri Mkuu.

Watu kama Wangwe au Dk. Slaa bila shaka kila mmoja asingetaka kuona hateuliwi yeye kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo wadhifa huo kupewa mtu mwingine.

Mbali na hao, mtu kama Tundu Lissu huenda naye asingekubali kabisa kutokuwa mmoja kati ya Mawaziri pamoja na kusambaratishwa ubunge, hivyo angehakikisha anafanya kila anavyoweza awe Mbunge wa Kuteuliwa ili aingie katika chombo hicho cha juu kabisa cha utawala na uongozi serikalini.

Wangwe aliyekuwa mstari wa mbele kupinga Zitto asiingie katika Kamati ya Madini wakati uhai wake ni wa miezi mitatu tu bila shaka asingeweza kukubali kuona Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Frederick Tluway Sumaye pale Ikulu.

Katika hali hiyo, Wangwe angeweza hata kukimbilia msituni na kuanzisha vita vya uasi dhidi ya Mbowe kama asingeteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hii.

Ili kutimiza azma yake, Wangwe angeibua madai kadhaa kwa Mbowe ili kumshinikiza abatilishe uteuzi wake kwa Zitto au Mbunge mwingine yeyote, vinginevyo angedai kuwa “amenunuliwa” na Waziri Mkuu Mteule ama angefanya kila anavyoweza ili kuhakikisha kwamba bunge halipitishi jina la mtu huyo.

Mbali na Chacha Wangwe, mtu kama Tundu Lissu naye huenda angekuja na kila aina ya upotoshaji kuhusu muundo wa serikali kama asingeteuliwa kuwa mmoja kati ya Mawaziri wa utawala wa CHADEMA.

Dalili hizo zinatokana na ukweli kuwa licha ya “kuiponda” Kamati ya Madini kwa madai kwamba haina nguvu za kisheria kama alivyoungwa mkono na Susan Lyimo na Kimesera, Tundu Lissu hakusema chochote alipopendekezwa na Chacha Wangwe aliyetaka aingizwe katika kamati hiyo ya Rais.

Hali hiyo inaashiria kuwa kelele zote dhidi ya Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ilikuwa ni agenda yenye “umimi” zaidi kuliko ukweli.

Kama ujumbe kwenye Kamati ya Madini tu imekuwa kimbembe kikubwa kiasi hicho, vipi Zitto angeteuliwa kuwa Waziri wa Serikali ya Mseto?

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi Mkuu, Idara ya Taifa ya Uhamasishaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu. Anapatikana kwa Simu Na. 0762 633 244

source majira
 
Lakini na Zitto asipewe misifa sana...maana tunawaonaga wengi kama yeye lakini wakishalamba nafasi nyeti wanazimikaga kama kibatari kilichokwisha mafuta. Ngoja tuone kazi zake kwani ameanza kupewa meno ya kuanza kutafuna nyama, sasa tutaona kama atatafuna kwa meno yake au ataomba nyama isagwe ili ameze kiurahisi. Tumuombee sana..lakini tusianze kumvisha masifa sana. Kwani kuna aliyetegemea anayoyafanya Kikwete ssa hivi?
 
Tundu Lissu hajawahi hakugombea ubunge 2005 kama mwandishi wa makala hii anavyojaribu kudanganya. Mwanakijiji huyu jamaa ameweka namba yake; hebu fanya naye mahojiano. Kuna mtu ana maswali yoyote ambayo angependa huyu jamaa aulizwe?

I miss u all

Asha
 
huyo mwandishi kauliza swali lisilo na mantiki zaidi. Zitto hawezi kuteuliwa kuwa Waziri as long as yuko Upinzani. Hakuna mpinzani ambaye atapewa Uwaziri zaidi ya wanachoweza kupewa "Unaibu". Why?

Kwa sababu Uwaziri siyo Kamati ya Siasa! Uwaziri ni cheo ambacho kina sheria zake kina nguvu zake n.k Hivyo mtu kama Zitto kwa mfano akipewa Uwaziri wa Madini, ana nguvu kwa mujibu wa sheria ya madini na sheria inayoongoza ofisi yake. Atakuwa na uwezo wa kuamua mambo ambayo sasa hivi hana; atakuwa na uwezo wa kwenda mahali popote na kutaka taarifa zozote kutoka chini yake ambao sasa hana; sasa ukiniuliza mimi, Zitto akipewa Uwaziri watu watafurahia na kushangilia; nitakuwa mmoja wao.

As long as usiwe Uwaziri wa Mambo ya Siri na Mahusiano ya Mafisadi!
 
Kikwete hana ubavu wa kumpa zitto uwaziri. Mwinyi alikuwa na nafasi kubwa ya kufanya hili kuliko Kikwete. Na ikitokea amempa zitto uwaziri basi atakuwa amejipiga bonge la bao kwa sababu zitto ni very unpredictable na usishangae video clips za Kikwete akisaini mikataba au kupanga mipango ya kifisadi zikiweka bongoradio na hapa JF.

Of all pple, Kikwete hawezi kutoa mafisadi kwenye baraza lake maana yeye naye ni fisadi tu.
 
Nakubaliana nawewe katika hili kwani mpaka sasa akili yangu bado huwa haikubaliani na ukweli kwamba NK bado ni waziri pamoja na so la wazi la BUZWAGI!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom