Kama ujui hili, kajifunze zaidi kuhusu mapenzi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
ASANTE KWA KUNILIZA.

1.Nilijua nimefika,nawe utanituliuza
Wakufa na kunizika,leo tena waniliza
Mdomo naufunika,wala sitokuuliza
Asante kwa kuniliza,nakuombea baraka.

2.Japo chozi lanitoka,maumivu napuuza
Mbali nawe naondoka,nakwacha dada muuza
Nenda kunako endeka,nibaki najiuguza
Asante kwa kuniliza,machozi nitayafuta.

3.Mapenzi yameanguka,shetani kayakatiza
Moyoni ninafunguka,sitoweza kulipiza
Mabaya yakaja zuka,tena yakupitiliza
Asante kwa kuniliza,nakiri nimepigika.

4.Kwako nimejeruhika,kupona bado nawaza
Dawa inahitajika,nitanywa kujiliwaza
Moyoni nimevunjika,sana umenishangaza
Asante kwa kuniliza,na mola atakulipa.

5.Tamati tumeshafika,penzi umeliunguza
Penzi limevurugika,tumeshindwa kulikuza
Leo tunatawanyika,tamaa umetukuza
Asante kwa kuniliza,na fimbo umenichapa.

SHAIRI-ASANTE KWA KUNILIZA.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
Pole rafiki

Pole yaliyokusibu, endelea vumilia
Vumilia majalibu ,usiendele kulia
Usijitwishe azabu, yaitaji kutulia
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Penzi ulimtunzia, na mengi ukatenda
siri ukamtunzia, leo hii amekwenda
Mbali alikuwanzia, kumbe ni mdananda
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Utenzi umeufuma,jinsi ulivyompenda
Bilashaka atausoma, popote alipokwenda
Usije jipamahoma, kwa Mumbaa ukaenda
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole rafiki

Pole yaliyokusibu, endelea vumilia
Vumilia majalibu ,usiendele kulia
Usijitwishe azabu, yaitaji kutulia
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Penzi ulimtunzia, na mengi ukatenda
siri ukamtunzia, leo hii amekwenda
Mbali alikuwanzia, kumbe ni mdananda
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Utenzi umeufuma,jinsi ulivyompenda
Bilashaka atausoma, popote alipokwenda
Usije jipamahoma, kwa Mumbaa ukaenda
Pole uwangu rafiki, usiendele kulia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kongole sana.
 
ASANTE KWA KUNILIZA.

1.Nilijua nimefika,nawe utanituliuza
Wakufa na kunizika,leo tena waniliza
Mdomo naufunika,wala sitokuuliza
Asante kwa kuniliza,nakuombea baraka.


2.Japo chozi lanitoka,maumivu napuuza
Mbali nawe naondoka,nakwacha dada muuza
Nenda kunako endeka,nibaki najiuguza
Asante kwa kuniliza,machozi nitayafuta.


3.Mapenzi yameanguka,shetani kayakatiza
Moyoni ninafunguka,sitoweza kulipiza
Mabaya yakaja zuka,tena yakupitiliza
Asante kwa kuniliza,nakiri nimepigika.


4.Kwako nimejeruhika,kupona bado nawaza
Dawa inahitajika,nitanywa kujiliwaza
Moyoni nimevunjika,sana umenishangaza
Asante kwa kuniliza,na mola atakulipa.


5.Tamati tumeshafika,penzi umeliunguza
Penzi limevurugika,tumeshindwa kulikuza
Leo tunatawanyika,tamaa umetukuza
Asante kwa kuniliza,na fimbo umenichapa.


SHAIRI-ASANTE KWA KUNILIZA.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Haya mambo ya karne ya 20, Saivi tunajipigia bila vina na mizani.
 
Back
Top Bottom