Kama udini utakuwepo sensa, weka uenyeji (uasili) kupinga udini tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama udini utakuwepo sensa, weka uenyeji (uasili) kupinga udini tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WaMzizima, Jun 25, 2012.

 1. W

  WaMzizima Senior Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nafuatilia hii mizozano hasa toka kwa waislamu na hususan Bakwata kushinikiza serikali iweke kipengele cha dini kwenye sensa ya taifa. Mi binafsi sioni tija kwenye hilo na mawazo yangu ni kuwa baada ya hapo hawa watu ambao wamepofushwa na kufungwa uelewa wao na kuona kila kitu kwa kutumia tafsiri na darubini ya dini zao hawaitakii mema nchi yetu.

  Ni wazi kuwa pinde dhamira yao itapotimia basi hapo wataanza kuishinikiza serikali na taasisi zake kuwa lazima uteuzi wa nafasi nyeti na ajira ziendane na uwiano wa kidini badala ya kuangalia ufanisi na uwezo wa watu kufanya kazi hizo, na baadae kudai pia wapewe ruzuku kufundisha au kujenga nyumba zao za ibada. Si unajua tena binadamu haridhiki ukimpa kidole kesho atakuja dai mkono na zaidi na zaidi!

  Ni kwa dhana hiyo napendekeza kama serikali ikiwakubalia kwa huo upuuzi, basi sisi wapenda maendeleo tujaze kwenye hiyo sensa kuwa dini yetu ni uenyeji hata kama ni waislam au wakristo maana hakuna tija yeyote kwenye hilo au tuache hilo swali wazi, huu ni upuuzi tu tusiendekeze...

  Kuna watu wanadai eti oo mbona UK au US wanacho hicho kipengele kwenye sensa zao, hizo nchi asilimia kubwa ni wakristo na hizi dini nyingine ni minority na nyingi waumini wake ni wageni na nia halisi ni kuona jinsi gani ya kuwahudumia wageni huko. Sasa hapa kwetu sidhani kama waislamu au wakristo ni minority au hata wageni ni wazi kuwa wengi wao ni wenyeji na priority ya serikali yetu ni kuleta maendeleo kwa wote sio group fulani la watu.

  Uenyeji / Uasili Juu!, tuweke hilo mbele...Down with udini na utengano kwenye taifa letu!
   
 2. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ungalikuwa mzalendo Ungalihoji matumizi ya billion za serekali kwa makanisa huku Migomo ya madaktari ikirindima. Huna chochote ni Mnafiki na MDINI tu wewe. Huna uchungu na Nchi unauchungu na kanisa tu wewe
   
 3. W

  WaMzizima Senior Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa taarifa yako mi sifuatilii dini yeyote, kwa hilo nipo neutral...pili tueleze mabilioni yetu yepi ya walipa kodi serikali inayoyatumia kufadhili makanisa...hili ni muhimu maana serikali yetu inatakiwa kuwa haina dini wala kulalia upande wowote kwa hilo. Hivyo kama una data kuhusu hilo tueleze ili tuweze kulifanyia kazi na kuhoji.

  Ndugu yangu nina uchungu sana na mustakabali wa nchi yangu, ndio maana nipo hapa kujadili maendeleo na kuhoji umuhimu wa dini kwenye hulka nzima ya sensa. Kama unaweza kunifafanulia kuwa nikijua kuwa waislamu/wakristo wako wangapi na jinsi data hiyo itakavyosaidia kwenye maendeleo yetu, basi nipe hiyo hoja... sio kuropoka tu na kudai kuwa ooh wewe mdini na unasaidia kanisa ambalo sijui hata likoje ndani... leta hoja sio ubabaishaji...
   
Loading...