Kama uchumi wetu unakua, kwa nini zamani tulikuwa na mashirika ya ndege ya nje makubwa yakija Dar na leo hatuna?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Unajua najiuliza sana. Zamani, enzi za Nyerere na Mwinyi ambapo uchumi ulikuwa mdogo sana, bado tulikuwa na mashirika makubwa ya ndege ya kimataifa yakija na ndege zao hapa Dar es Salaam. Ninavyoelewa, kiashiria kimojawapo kwamba uchumi wa nchi uko vizuri ni kuwa na mashirika ya ndege mengi ya kimataifa yakifanya safari kuja nchini kwenu.

Sasa iweje kama uchumi unakua ndipo tunapoteza hayo mashirika?

Baadhi ya mashirika ya ndege yaliyokuja Tanzania;

  1. British Airways
  2. Air France
  3. KLM
  4. Sabena
  5. Scandnavia Airlines (SAS)
  6. Lufthansa
  7. Alitalia
  8. Ethiopian Airways
  9. Etihad
  10. Aeroflot
  11. Gulf Air
  12. South African Airways
 
Mkuu yapi bado yanakuja na yapi hayaji kutokana na hiyo list yako? Nina uhakika mengine bado yanakuja
 
Achana na hii nchi ndugu yangu......ukishighulika nayo sana utajikuta unaishia na mental problems.......kikubwa tafuta pesa ya kuendesha life yako tu
 
Back
Top Bottom