Pre GE2025 Kama uchaguzi wa mwaka 2024 ungefanyika kwa haki, wapinzani wangekubali kushiriki Uchaguzi ujao kwa Katiba na sheria hizi hizi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kimalingano

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
786
1,015
Ni kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliharibiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali kiasi kwamba ukaonekana ni hovyo.

Ndiyo maana akina Lissu wanapojenga hoja ya mabadiliko kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wanaeleweka vema na Watanzania na Jumuiya ya kimataifa.

Na mbaya zaidi hoja ya upande wetu kuwa muda wa mabadiliko hautoshi imejibiwa kikamilifu na akina Lissu.

Kama uchaguzi wa mwaka jana ungefanyika kwa namna ambayo ingewaridhisha wapinzani mwaka huu wangekubali kushiriki uchaguzi Mkuu kwa Katiba,Tume ya Uchaguzi na Sheria hizi hizi zilizopo.
 
Mhe.Mchengerwa ametuangusha CCM.Ilitakiwa awazuge wapinzani ili mwaka huu tushinde kiulaini.
 
Back
Top Bottom