Kama uchaguzi ungefanyika leo....j2 hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama uchaguzi ungefanyika leo....j2 hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Oct 3, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Its part of challeng but very interesting....!!!

  Hii mada ni kwa mawazo yangu ikiwa ni kutoa upupu na matongotongo yaliyokuwepo kwenye mada yenye kichwa kama hiki iliyotolewa na majjid mjengwa siku kadhaa zilizozopita. Ni hoja ambazo zikipuuziwa zinaweza kuharibu saikolojia ya watu wakati huu ambao mabadiliko yanatakiwa katika uwanja huu wa siasa. Lengo sio kumjibu mjengwa lakini ni kutoa mawazo yangu ambayo yanakinzana kidogo na mjengwa!

  Kiukweli kama uchaguzi huu wa Rais ungefanyika leo hii siku ya jumapili hii (tarehe 3 october 2010) ikiwa zimebakia siku 28 tu kufanya uchaguzi, ni wazi kwamba DK SLAA angeibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia 60, huku JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa 1ST RUNNER-UP, na LIPUMBA 2ND RUNNER-UP (wakigawana asilimia zilizobaki) na wengine wakibakia wasindikizaji kama kawa.
  Nianze kwa kusema hivi kama huu uchaguzi ungekuwa wa HURU NA HAKI basi mambo yanatazamiwa kuwa kama nilivyoanza hapo juu. Hili halina ubishi kwa sababu zifuatazo:

  CHADEMA NA UJIO WA DK SLAA:
  Ujio wa Dk Slaa katika kinyang'anyiro cha urais kimeipa sifa kubwa Chadema kwa kuonekana ni chama chenye mvuto na kinaweza kuwa mbadala wa CCM na watu wanakiamini. Kiukweli ujio wake licha tu ya kustukiza watu bali ni ''suprise'' kwa wananchi wote. Kwakuwa hakuna aliyejua ujio wa DK Slaa ni wazi kuwa Chadema wanaweza na wana USIRI mkubwa sana ndani ya chama kwa sababu hata mashushushu wa CCM hawakuwa wakijua kama huyu bwana atawania uraisi. Mbowe alishawahi kusema mara moja pale Jangwani kwamba tulisoma nyakati na kufahamu kwamba DkSlaa 'anauzika' na anakubalika sana na ndio maana akawekwa pale. Hali hii inanipa moyo kwamba anaweza kukaa na kurudisha heshima ya Ikulu ambayo imeshuka hadhi kwa kiasi kikubwa mno tangu huyu Mkwere aingie pale.

  Ameigeuza ikulu kuwa ''family building'' na leo hii hata panya akikatiza mbele ya raisi pale ikulu basi habari hii kesho utaikuta mtaani imezagaa, hamna tena heshima katika lile jengo. Wafanyabiashara wakubwa, mafisadi wakubwa na Watabiri wakubwa wameigeuza ikulu ni pahala pao. Hamna tena siri yoyote pale.

  Mjengwa aliandika kuwa DK SLAA kakosa mvuto:
  Hii sio kweli na ninaipinga. Itakumbukwa kuwa mjengwa aliandika hivi pale Dk Slaa alipokuwa mapumzikoni Dar es salaam kwa zaidi ya wiki. Alifanya vikao vya ndani na wanachama wake huku kikubwa wakitafuta ridhaa au suluhishi la wabunge wanawake wa viti maalum, ambapo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa.
  Na ikumbukwe kuwa ndani ya mapumziko yale hata kama alikuwa kimya kwenye majukwaa ya siasa mpaka baadhi ya TV channels zikawa hazionyeshi habari zake, lakini tuliona jinsi CCM iliyokuwa inawaka moto na kugeuka majivu huku wasemaji wake makamba na kinana wakijipatia glass ya maji kupitia mgongo wa pumziko la DK SLAA. Tulishuhudia jinsi Ridhiwani alivyotolewa mbio huko iringa asifanye vikao vyake vya suluhishi. Tuliona jinsi zomeazomea iliyomkuba KIKWETE katika baadhi ya kampeni zake majukwaani. Kwa hiyo si kweli kwamba Slaa kakosa mvuto. Na huu ndio muda pekee ambao watu wa dini walipombariki na kumpitisha Huyu Dk Slaa.

  UDHAIFU WA CHADEMA:
  Ni kweli kwamba inabidi ifanye kazi ya ziada kupenyesha mianya yake ya ukombozi katika maeneo mbalimbali, hii kwangu sioni kama ni udhaifu bali ni changamoto ambazo zipo mbele yao. Mbona CCM imejaza mabango mengi sana huko vijijini?kwani watu hawaijui Ccm huko? Kifedha bado ni changamoto nyingine kwani wana Chadema hawataki CRIMINAL FINANCE ziingie kwatika mifuko yao ya uchaguzi na mara zote huwa wanapitisha KAPU ' katika kila kampeni zinazofanyika, ofisi zipo na sio kweli kwamba akitoka na chopa basi watu hawajui pa kwenda kupata usajili wa Chadema, huu ni unafiki.

  ZITTO KABWE:
  Uwepo wa zitto kabwe haudhoofishi mbio zozote za kampeni kwa Dk Slaa. Nilikuwa najiuliza hivi huyuu mjengwa kakosa au kawa mvivu kiasi hiki wa kufikiri? Mjengwa atambue kuwa zitto kaingia bungeni mwaka 2005 akiwa na miaka 29, mpaka kufikia mwaka wa 2015, huyu bwana atakuwa na miaka 39. Ndio kusema kwamba bado hadi muda huo zitto atakuwa bado hajawa ''qualified candidate for presidential racing/rally'' kikatiba. Isitoshe hata akiulizwa na watu wake kwamba viti mzee uliambia utagombea uraisi, jibu ni rahisi sana, hata akisema kwamba chama hakijaniruhusu inatosha sana, sidhani kama watu wataandama kwa jibu hili. Hii ni hoja nyepesi mno Mjengwa.
  Na kwa mdahalo wa jana toka Kigoma Kaskazini, huyu bwana ataongoza kwa muda mrefu sana pale jimboni kwake. Kawafunika mno wale wenzake kwa hoja zenye mantiki.

  KWA UPANDE WA CCM;
  KAULI NA ISHARA: Kitendo kinachafanyika sasa hivi cha mgombea urais JAKAYA KIKWETE cha kuwanadi na kuwasafisha watuhumiwa wakubwa wa ufisadi ROSTAM AZIZ, MZEE WA VIJISENTI-CHENGE, MRAMBA, ADEN RAGE na wengineo, kunaidhoofisha sana chama chake, hii ndio kusema kwamba wanajiua wenyewe.
  Kitendo cha Ccm ku'deal' na mtu mmoja mmoja ambao wao wanamwona kama ni msaliti sio kizuri kwa chama. Mfano ni pale Ccm inapowahamisha wakurugenzi wake toka sehemu moja na kupelekwa nyingine bila sababu maalum kuainishwa ni unfair. Hii ndio kusema kuwa CCM badala ya kudeal na katiba na ilani zao mbofumbofu wanaona bora wadeal na mtu flani. Hii sio ishara nzuri kwa chama.

  Kitendo cha CCM kukwepa midahalo sio ishara nzuri kwao na kinainyima haki demokrasia ya ukweli. Hali hii inajaza watu maswali kuliko majibu kwamba kuna nini ndani ya CCM? Hali hii vilevile imeonyesha kuwa maamuzi mengi ndani ya Ccm yanafanywa na watu wachache(akina makamba na kinana) kwani hata Msekwa alishangaa ni katika vikao gani vya chama kuamua kutoshiriki midahalo.
  Kitendo cha CCM kupanda majukwaani na kupoteza muda wao wakipiga makelele kwamba hamna mpasuko ndani ya chama, ni dhahiri kwamba CCM inayumba vibaya sana, mienendo ya mama salma na ridhiwani yanzidi kuleta wasiwasi kwamba chama kina makundi makubwa.

  KUISHIWA KWA WATU WENYE MANTIKI YA KUJENGA HOJA.
  Hii inatia moyo kwa wanachadema. Huu ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Ccm imeishiwa watu wenye mantiki ya kutoa hoja mbele za watu. Nithubutu kusema kuwa ukiwaondoa MAGUFULI NA MWANDOSYA, chama cha mapinduzi kipo hoi hapo baadae tuseme 2015 kumweka mtu makini wa kugombea kiti cha uraisi, Nianze na hawa:

  SPIKA SITTA: Ni juzi tu huyu bwana katangaza kuacha siasa 2015 kama alivyosema mwenyewe kwamba 'kasoma alama za nyakati'. Isitoshe huyu bwana kwa sasa ana umri wa miaka 68, hadi kufikia 2015 atakuwa na miaka 73 so ''age factor'' itamtoa Knockout kwani kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kupambana na vijana wa sasa wenye nia ya dhati ya mabadiliko. This is good for him.

  PETER PINDA: Huyu nae anapanda boti moja na spika sitta kwa kuachana na siasa za bongo.

  BERNARD MEMBE: Huyu bwana ni smart/handsome kama JK, akisimama kuwania uraisi atatupwa vibaya sana na upinzani, hana msimamo na huenda ana kundi kubwa la watu nyuma yake, nina maana kwamba hana maamuzi yeye kama yeye, bali anasubiria watu wake ili atoe maamuzi, Rejea swala la mahakama ya Kadhi lilivyomsumbua na ile swala la Uraia wa nchi mbili. Vilevile akigombea uraisi kuna mijitu mingine inakuja na kusema haiwezekani kwanini Mkapa atokee kusini na Huyu bwana inakuwaje atokee tena kusini?? watu wengi hawatakubali kuongozwa mara mbili mfululizo na watu toka kusini-LINDI NA MTWARA(Ni maoni yangu tu).
  Na kama CCM itasimamisha mtu mwingine mbali na hawa watu itatumia fedha maradufu kumnadi na ndio mwisho wa CCM hapo baadae.

  UJIO WA SHEIKH YAHYA MNAJIMU
  Ujio wa huyu mnajimu umeondoa kwa kiasi kukibwa mvuto wa chama cha mapinduzi kwa watu wake. Kitendo cha ukimya baada ya matapishi yale ya mnajimu kumeleta hofu kwa wananchi kwamba ccm kinaongozwa na mapepo yasiyoonekana. Kitendo cha waislamu kutolea jicho na kukemea hotuba ya KAKOBE na kuacha yale ya yahya kuondoa roho ya mgombea flani maarufu , kumeishushia hadhi sana CCM. Hii sio ishara nzuri kwa CCM.

  CUF. CHAMA CHA WANANCHI
  Ni kweli kwamba hama wa wananchi CUF kimejizatiti mno kanda ya kusini lakini hii sio kigezo kwamba kitafanya vizuri au kitaibuka kidedea kwenye urais. Ni uhuni kusema kwamba CHADEMA hakikubaliki sana kanda ya kusini. Ni jana tu tumeona jinsi Dk slaa alivyokusanya watu huko MBINGA na SONGEA, hii ni ishara nzuri kwa chadema kuchukua ushindi wa zaidi ya asiliamia 60 na kuendelea. Tunasubiri Dk Slaa akienda Lindi na Mtwara upepo utakuwaje, na hapo ndipo tutakapotoa good conclusion about southern zone, na sio tu kwakuwa LIPUMBA kasoto mawiki kibao south basi ndio kusema anakubalika kuliko mgombea mwingine

  MY TAKE:
  UCHAGUZI WA RAISI UNGEFANYIKA LEO, CHADEMA WANGEIBUKA KIDEDEA KWA ASILIMIA NYINGI KITU AMBACHO KINGELETA HOFU SANA KWA CCM NA HUENDA WASIKUBALLIANE NA MATOKEO KWAHIYO USHINDI WA CHADEMA MPAKA SASA UNAWEZA KULETA VURUGU KWA WATU WASIOKUBALI KUTANGAZIWA KWAMBA KWA MIAKA ZAIDI YA HAMSINI BALLOT PAPER IMEMWEKA MADARAKANI MTU AMBAE KATOKA NJE YA CCM. NASUBIRI UTABIRI WA SYNOVET HUKU NIKILA KOROSHO KAVU NA SPARETA BARIDIIII NASUBIRI GAME YA ARSENAL NA CHELSEA SASA..!1...SIASA NI TAMU LAKINI NI CHAFU KWA WALIO WACHAFU...NAWAKILISHA. 0655457605
   
 2. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,961
  Likes Received: 1,778
  Trophy Points: 280
  hiyo iko wazi na ccm imeshalisoma hilo..kuthibitisha hilo ni pale mnadhimu wa jeshi aliposhikwa kiuno na jk chini ya ushauri wa kina makamba ili aingilie mambo ya siasa...kama ni machafuko imetokea mwembechai na hatujaona jeshi kutoa kauli miaka ile....
   
 3. P

  Percival Salama Senior Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi Ccm wapo hoi kilichobakia ni kutafuta mbinu mbadala za kujihalalishia ushindi na vyombo vyetu vya dola bila kufikiri kwa makini wanaingia kwenye mtego wa wanasiasa

  Wanatakiwa wauelewe msemo huu maarufu "KUPANGA NI KAZI YA BINADAMU LAKINI MATOKEO NI KAZI YA MUNGU". Hebu chukulia Dr Slaa ameshinda Urais na mbinu zote za kuchakachua matokeo zimeshindikana na akatangazwa kuwa Rais wa tano wa Tanzania, hao watoa kauli watajificha uvungu gani?
   
 4. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jama CHADEMA ilifanya mkutano wake Amana Ilala. Kama ni wakweli basi leteni picha za "umati wa watu" uliokusanyika kuwasiliza nyie mnaotakiwa kuchukua nchi. Hata Tanzania Daima pia hizo picha hakuna. :tonguez:
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu acha wajipe ushindi hapa janvini. naona jamaa anahasira sana na Mjengwa sijui kamkosea nini, kwani hata title ameiga kutoka kwake. Kwanza hii thread tyake haieleweki vizuri. Achukue likizo ili akaiandike vizuri.
   
Loading...