Kama Ubunge ni umasikini, mbona unagombewa kwa nguvu kubwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Ubunge ni umasikini, mbona unagombewa kwa nguvu kubwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Fredy Azzah
  BAADA ya miaka 29 ya kuwa bungeni na 17 ya kuwa Mbunge wa Njombe Kusini, Spika Anne Makinda amesema sasa inatosha.

  Makinda amewaomba wananchi wa Jimbo la Njombe Kusini hivi karibuni, kumruhusu kuweka silaha chini mwaka 2015, atakapo fikisha miaka 33.

  Pamoja na sababu nyingine za kuachia nafasi hiyo, Makinda anataja ukata kwa wabunge kuwa ni moja ya sababu zilizomfanya afikie uamuzi huo.

  “Ubunge ni mzigo, wabunge wengi sana sasa hivi wako Frastrated, (wamechanganyikiwa) kutokana na ugumu wa maisha, ubunge ni mzigo, hakuna pesa kama watu mnavyoona,” anasema na kuongeza:

  “Watu mnavyoniona kama mimi tena spika ndiyo kabisa mnafikiri kuwa nina pesa nyingi tu, ukweli siyo hivyo, huku hakuna pesa kabisa na ninaomba mnikubalie mwaka 2015 sigombei tena na wabunge wengi ambao wana taaluma zao mtaona hawatagombea tena.”

  Historia ya Makinda katika siasa
  Makinda amekuwa mwanasiasa kwa miaka 45 sasa, tangu alipojiunga na TANU mwaka 1965 na Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977

  Akiwa sekondari alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa TANU na mwaka 1975 aliteuliwa kuwa mbunge kupitia vijana, akiwa ndiye mbunge kijana kuliko wote kwa wakati huo akiwa na umri wa miaka 23.

  Anasema, wakati anawania kiti cha ubunge kwa nafasi za vijana alikuwa yuko katika majaribio ya kikazi katika Kampuni ya TIC, lakini mawazo yake yalikuwa katika siasa tu.

  Makinda alikuwa mbunge wa kawaida kwa miaka nane hadi mwaka 1983 alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
  Mbunge wa Njombe Kusini tangu mwaka 1995

  Akiwa Waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais alifanya kazi na aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Edward Sokoine kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali mbaya ya kiuchumi.

  Mbali na ubunge amewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma mwaka 1995 hadi 2000. Anasema hiyo ni kazi aliyoipenda zaidi kwani alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu zaidi na wananchi.

  Aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa bunge, akimsaidia spika kuendesha vikao, halikadhalika alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya maliasili, mazingira na kuondoa umaskini.

  Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge nafasi ambayo ni ya kwanza kushikiliwa na mwanamke hapa Tanzania.

  Mwaka 2010 Makinda aligombea nafasi ya spika na kufanikiwa kupitishwa na chama chake baada ya kupambana na aliyekuwa katika nafasi hiyo Samuel Sitta.

  Baada ya kupigiwa kura na Wabunge, Makinda alimtupa vibaya Mabere Marando kutoka Chadema baada ya kupata kura 265 dhidi ya kura 55 za Marando.

  Katika kipindi chake kama Spika, Makinda ameibua msuguano mkali kati ya Bunge na wananchi kutokana na madai ya posho za wabunge.

  Awali madai ya posho yalipingwa vikali cha Chama cha Demokrasia na maendeleo. Lakini madai hayo sasa yamekuwa ya wananchi wote huku Rais Jakaya Kikwete akipinga kuyaunga mkono.

  Makinda amekuwa akitetea nyongeza ya posho za wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.

  Je, kazi ya ubunge ni mzigo?
  Baadhi ya wabunge ambao wanataaluma mbalimbali, wanaungana na Makinda juu ya hali ngumu ya Wabunge wakisema kuwa, hali ni ngumu.

  Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangala ambaye kwa taaluma ni daktari, anasema mtu aliyeingia kwenye ubunge kwa ajili ya kutafuta masilahi, lazima aone kuwa nafasi hiyo ni mzigo.

  “Mtu aliyeingia kwenye ubunge kwa lengo la kutafuta ajira au fedha nyingi, lazima aone kuwa ubunge ni mzigo, ubunge hauna hela kama watu wanavyodhani, ” anasema Dk Kigwangala”

  “Ubunge ni kazi ya kujitolea, kutumikia wananchi, leo hii hata wakisema ubunge iwe ni kujitolea hakuna chochote, mimi nitagombea kwa nguvu zote mpaka nishinde kwa sababu napenda tu kuwa mbunge,”.

  Dk Kigwangala anasema kuwa, ukilinganisha fedha anazopata sasa hivi akiwa mbunge, ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na zile ambazo alizokuwa akipata alivyokuwa akifanya kazi yake ya ushauri.

  “Mimi nikwambie tu kuwa sikuwa nafanya kazi ya kutibu, mimi ni mshauri, kwa siku nilikuwa nalipwa dola 300 za Marekani, hivyo kwa mwezi nilikuwa napata kama dola 9,000, hiyo ni mbali na mambo kama fedha za usafiri, mawasiliano na fedha za safari,” anasema Dk Kigwangala.

  Kwa upande wake mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, anasema ni kweli kuwa wabunge wengi wana hali mbaya kifedha, tofauti na watu wanavyowaona.

  “Sitaki kusema kuwa ubunge ni mzigo, ila kwa watu wengi ambao wanafikiri kwenye ubunge kuna hela, sisi tuliokuwa na kazi nyingine mwanzoni, mapato yetu ya mwanzo na sasa hivi ni tofauti kabisa,” anasema Lisu.

  “Wabunge wengi wana matatizo ya fedha, wana mikopo mikubwa iliyowalemea, walitoka kwenye kampeni wametumika fedha nyingi, hivyo kweli hali zao siyo nzuri,”
  Anasema kuwa, fedha alizokuwa akipata katika shughuli zake za uwakili kabla ya kuwa mbunge, ni nyingi sana ukilingana na zile anazopata akiwa mbunge.

  Hata hivyo anaeleza kwamba, bado Bunge lina hitaji watu wenye taaluma mbalimbali ili shughuli za nchi ziweze kwenda vizuri.

  “Bunge linahitaji watu wenye taaluma mbalimbali, wanaojua dunia inakwenda vipi, kwa hiyo lazima watu wenye taaluma waendelea kuwapo bungeni kwa kuwa hii ni kazi ya kutumikia umma zaidi,” anasema Lisu.
  chanzo. Kama Ubunge ni umasikini, mbona unagombewa kwa nguvu kubwa?
  Mapato ya Mbunge
  Mshahara wa mbunge ni Sh2.3 milioni kwa mwezi, mafuta ya gari kwa mwezi lita 1000 lita moja Sh2,000 jumla Sh2 milioni, posho ya ubunge Sh1 milioni, posho ya kukaa bungeni ni Sh80,000, posho ya kuendesha ofisi Sh700,000 na simu/mawasiliano Sh500,000 jumla Sh7.3 milioni Fedha nyingine ni fedha ambazo hulipwa wakati wa vikao Sh70,000 kwa siku, posho za kujikimu Sh80,000 na usafiri Sh50,000.
   
 2. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Aache ujinga wake!huyu bibi,unajua binadamu unapofikisha kuanzia 60 .......huwa ni kero kwa kwa familia na ndugu,sasa huyu bibi nikero kwa taifa!
   
 3. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,211
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  vijihela viduchu sana jamani Wabunge wetu wanapata taabu saana....hebu tuwafikirie jamani....
  tuchukue mijihela ya waalimu na watumishi wengine tuwaongezee jamani waweze kutunga Sheria vizuri.
  Wakiachia ngazi nusu ya wabunge tutakosa wasinziaji kule!
   
 4. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tumekwisha ona thread kama hizi mbili hapa jamvini!
   
 5. m

  mhondo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Inawezekana wanakimbilia umaskini.
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Kuna siku nilimkuta lema(MB) akihutubia Hapa Arusha maeneo ya Ngarenaro kwenye ufunguzi wa tawi la CHADEMA.
  Nanukuu "Mm sasa hv siwezi kuhongwa na mtu yeyote, maana nina hela!!! Juzi tu tumepewa milioni 290. hapo bado mshahara na marupurupu mengine" alisema Lema!
  kwahiyo hili la umaskini wa wabunge ni moja ya kauli tata sana, Tunavyoona maisha yao halisi mtaani, na tamko la Speaker ni tofauti!
   
 7. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  1 + 1 = 3 !!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mtanzanika ukitaka kujua hasira za mlevi mwaga pombe yake,mdakitari wanachokifanya ni cha mtoto ,sisi tunaua kimya kimya ,si umeona mwanae wa mkuu wa kaya ,tukihakikisha aliye faulu awe na divition 4 au sifuri kabisa:hat:
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Nafikiri akifika mwaka huo huyo mama atakuwa kesha maliza kahekalu kake pale Sinza alikowafungia barabara wenzake ili ajenge hicho kihekalu chake,na hapo njombe itakuwa kwaheri kwani atakuwa mjumbe wa nyumba kumi Sinza
   
Loading...