Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Siku zote ukiwa mwongo usiwe msahaulifu. Nashangaa sana kuona jinsi Tundu Lissu na CHADEMA wanavyosahau kwa kasi licha ya kila siku kutumia propaganda za uzushi na uongo dhidi ya Serikali ya awamu ya Tano.
Nimesikia taarifa juu ya Tundu Lissu kumuandikia Barua Rais Magufuli ya kutaka kukutana naye Ikulu kwa Mgongo wa TLS. Tena ameenda mbali na kusema kwa tambo na majigambo kuwa Mkutano huo utakuwa baina ya Marais wawili.
Nimkumbushe Lissu kuwa Magufuli anayemuomba kukutana naye ni yule yule Dicteta Uchwara. Na moja ya sifa za Madikteta kote Ulimwenguni ni kutotoa nafasi ya majadiliano ya kidemokrasia. Udikteta na Demokrasia hazichangamani.
Rais Magufuli ni yule yule Rais wa Ajabu kuweza kutokea katika nchi yetu tangu tupate uhuru.
Rais Magufuli ni yuleyule kiongozi anayeminya uhuru na demokrasia ya wapinzani.
Rais Magufuli ni yule yule aliyedhalilisha hadhi ya Ikulu.
Moja ya Kampeni ya Lissu wakati anagombea TLS ni kukomesha kitendo cha Rais Magufuli kuwahutubia Wanasheria wakati wa Siku ya Sheria nchini kwa madai kuwa Magufuli hana hadhi ya kuongea na wasomi.
Yapo mengi ambayo Lissu amesema tena kwa jazba dhidi ya Rais wetu mpendwa. Nichukue fursa hii kumshauri Tundu Lissu. Kama anataka Juice ya Ikulu, ni vema akafuta kauli zake na kumuomba Radhi Rais Magufuli. Akishindwa kufanya hivyo ni vema akaendelea na msimamo wake juu ya Rais Magufuli. Unafiki haukubaliki.