Kama tunataka mabadiliko ya kweli Tanzania, siasa cheap za Nape, Dr. Slaa tuzipe kisogo

dkn

Senior Member
Oct 7, 2010
139
42
Kama CCM wataweza kutuleza wananchi kashfa za ufisadi na nini wamefanyiwa mafisadi kama kina Chenge etc na kupangua hoja za upinzani (Chadema hasa hasa), nitaipa CCM kura yangu ila huu upumbavu wa kuulizana nani karudisha kadi sijui CCM wanafanya nini. Wizi wa Tanzania uko waziwazi, watu wanaiba hela (EPA) wanaombwa kurudisha, wanarudisha bila kufikishwa mahakamani..kiongozi anaiba anasema ni vijisenti anabaki tu kuwa kiongozi. Tanzania imefikia mahali wananchi wanaona hata sifa kumchagua kiongozi fisadi hata kututetea wezi, viongozi wa CCM akiwemo Rais amekaa kimya serious human rights violations, corruptions of high level (deals za oil explorations...). Kama basi tunaipenda nchi yetu, njia moja ni kutokuchagua viongozi hovyo, CCM inatakiwa mabadiliko makubwa sana kutoa viongozi wake ambao wengi wanataka kuwa madarakani kuepuka kupata matatizo iwapo upinzani utachukua nchi. Kila kiongozi wa juu wa CCM, agenda yao ni moja..kuwa madarakani kama hutaki kucheza hiyo game basi utapata shida. Rais hawezi kumwambia kiongozi fisadi mbona hivi na yeye pia ataambiwa wewe vipi, hapa ni kulindana mpaka mwisho.

Upande wa Chadema na vyama vya upinzani kwa ujumla, kuna mambo mengi sana wanatujuza wananchi wa kawaida ambayo tusingeyajua kabisa tena hii si effort yao pekee bali na CCM wenyewe ambao labda hawakupata fungu lao..marginalized individuals/grounds ndani ya CCM wametoa information muhimu na hizi zinawapa kina Dr. Slaa nguvu na majigambo wao wanaweza kuendesha nchi. Kujibishana na makesi sijui ya kuoa, mara kadi ya CCM/CCJ, wananchi wa Tanzania tumekuwa washabiki wa mambo yasiyo na tija; tunataka upinzani ufanye kazi zake kisayansi zaidi..evidence based kuwa kuna hela zimeibiwa ziko Uswisi etc. kaeni chini mpate ushahidi wa kutosha then mkitoa data za kueleweka na facts zote mtakuwa mmefanya la maana kwa Watanzania. Kuna mafisadi inasadikika walikuwa na mahoteli walipoanza kuongea ni miaka sasa, watu walishauza assets zao na wengine tunasikia wanastores za noti na mahela yanapelekwa nje mchana kweupe, twiga wanaondoka, dhahabu.

Watanzania tusiangalie chama eti CCM kwakuwa ndiyo wenye serikali au wamekusomesha n.k. siyo justifications ya ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu au Chadema kwa kuongea watafanya hivi au wao ndiyo wamegundua mapungufu ya CCM na mafisadi; tuangalie viongozi wasio na uroho wa madaraka ambao tunawaona kwa vitendo hawakubaliani na uozo wa sasa hivi hata kama wako CCM au vyama vya upinzani. Sioni ubaya wa viongozi wa upinzani kujiunga na CCM kama team ya watakaowekwa CCM ni nzuri au CCM kwenda upinzani kuwa na watu wenye uzalendo na nchi yao. Unachanganya mafisadi ndani ya CCM na viongozi wasafi hakutakuwa na mabadiliko. Siasa za ujinga wa kufuatana kwenye personal life, matusi, sijui hujarudisha kadi, sijui wewe umesoma zaidi etc, tunataka majibu ya matatizo ya wananchi na nini serikali imefanya kuhusu mafisadi, wananchi wanatoa kodi, mama zetu wanauza nyanya sokoni eti kesho wanatakiwa kulipia deni la Tanesco wakati wezi wanajulikana badala ya kupiga hatua ya kufanya mambo muhimu kama elimu ya bure mpaka vyuo vikuu, kufufua viwanda, kuongeza ajira viongozi wanaweka mabilioni nje ya nchi na pesa za walipa kodi.

Mungu ibariki Tanzania na wale wote waliotuweka kwenye hali baada ya miaka 50 ya uhuru uwashushie mkono wako wa adhabu hapa hapa duniani. Amina
 
Back
Top Bottom