Kama tunaendelea kuruhusu ndege kuingia nchini, serikali izuie ibada na mikusanyiko mingine yote isiyo ya lazima ikiwemo kudhibiti masoko

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Wakati baadhi ya nchi za wenzetu sasa zimefikia hatua ya kudhibiti raia wake kwa kuwataka wabakie majumbani, kufunga mashule na vyuo, kupiga marufuku mikusanyiko ya michezo kama soka, kufunga mipaka n.k zikiwa ni hatua za kudhibiti kusambaa kwa Corona, sisi tume-relax tukiamini udhibiti unaofanywa katika viwanja vya ndege unatosha kukabiliana na ugonjwa huu kuingia nchini.

Ni bahati mbaya tunasahau katika nchi za wenzetu, mfano Rwanda, mtu aliegundulika kuwa na ugonjwa huo aliingia nchini humo huku akionekana hana ugonjwa huo ila baada ya siku chache akaanza kuonesha dalili na alipopimwa aligundulika kuwa na huo ugonjwa.

Taarifa kama hizi zinatosha kabisa kutufanya tuchuke maamuzi magumu ya kuzuia ndege kuingia nchini kwa muda fulani huku tukiangalia hali ya kusambaa ugonjwa huu duniani.

Hivyo, kwakuwa tumeruhusu ndege na wageni kuendelea kuingia nchini, basi ni vizuri tukachukua hatua za kudhibiti mikusanyiko isiyo ya lazima humu ndani ya nchi kama vile kuzuia watu kukusanyika ili kufanya ibada, kukusanyika katika viwanja vya michezo, kwenye masoko n.k vinginevyo unaweza kuja kutokea mlipuko wa ghafla utakaotushinda kuudhibiti na tukalazimika kuchukua hatua hizi when it is already too late.

Kwa mfano, sioni logic ya Rais kusema kaagiza vibali vya watumishi wanaokwenda nje ya nchi kudhibitiwa wakati wageni kutoka nje ya nchi bado wanaingia nchini tena kwa wingi tu kama hakuna tishio la ugonjwa huu.

Nchini Hispania kama siosei, serikali sasa inachukua hatua za kudhibiti raia wake kutoka nje ya majumba yao lengo likiwa ni kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huu.

Naelewa serikali ikichukua hatua hizi wakati huu ambapo hakuna mtu aliethibitika kuugua ugonjwa huu humu nchini, watu hawataielewa serikali na wataanza kulaumu ila ni wananchi hawa hawa watakaokuja kuilaumu serikali kwa kutochukua hatua mapema na hasa pale itakaposhindwa kuwahudumia wahanga wa gonjwa hili maana binadamu ndivyo tulivyo.

Inawezekana pia tunaangalia zaidi impact za kiuchumi zinazoweza kutokana na kuzuia ndege kuingia nchini kama vile kukosa mapato yatokanayo na watalii kuingia nchini ingawa sidhani kama na hao watalii kwa sasa wana moyo wa kusafiri huku hali ya ugonjwa ikiendele kuwa tishio duniani. Au tunahofia kuharibu mahusiano yetu na nchi zingine ila ni lazime tupime impact ya gonjwa hili kuingia nchini ukilinganisha na impact hizo za kiuchumi na za kidiplomasia.

Kama tunangoja mpaka ugonjwa uingie nchini kisha usambae na watu waanze kupukutika ndio tuchukue hatua, basi tusubiri wakati huo ufike alafu tutakuja kuona kama tumefanya maamuzi sahihi au laa.

Nayasema haya nikizingatia pia ukubwa wa nchi yetu, umasikini wetu na teknolojia duni tuliyonayo kama taifa kuweza kukabiliana na milipuko ya magonjwa achilia mbali uewlewa mdogo walionao watu wetu.
 
Bado hatujamaliza mzaha tukimaliza tutakua tumeisha ipata, eti timu ya mpira ya wasichana nchini ya miaka 17 wametua Uganda wakiwa wamevaa maski za pua na mdomo kuonesha utayari wetu watanzania!

Huo ni mzaha wa kitoto kama ulivyo umri wao, sijui na hiyo mechi waliicheza wakiwa wamezivaa hizo maski! Tukumbuke Malawi wazazi walikataa watoto wao wasichana nchini ya miaka 17 kuja Tanzania kucheza mpira wakihofia Corona huku sisi tukitamba eti tunao wataalamu nchi mzima kuidhibiti Corona tunaifananisha na Chadema.
 
Wakati baadhi ya nchi za wenzetu sasa zimefikia hatua ya kudhibiti raia wake kwa kuwataka wabakie majumbani,kufunga mashule na vyuo,kupiga marufuku mikusanyiko ya michezo kama soka,kufunga mipaka,n.k zikiwa ni hatua za kudhibiti kusambaa kwa Corona,sisi tume-relax tukiamini udhibiti unaofanywa katika viwanja vya ndege unatosha kukabiliana na ugonjwa huu kuingia nchini.

Ni bahati mbaya tunasahau katika nchi za wenzetu, mfano Rwanda,mtu aliegundulika kuwa na ugonjwa huo aliingia nchini humo huku akionekana hana ugonjwa huo ila baada ya siku chache akaanza kuonyesha dalili na alipopimwa aligundulika kuwa na huo ugonjwa

Taarifa kama hizi zinatosha kabisa kutufanya tuchuke maamuzi magumu ya kuzuia ndege kuingia nchini kwa muda fulani huku tukiangalia hali ya kusambaa ugonjwa duniani.

Na kwakuwa tumeruhusu ndege na wageni kuendelea kuingia nchini,basi ni vizuri tukachukua hatua za kudhibiti mikusanyiko isiyo ya lazima humu ndani ya nchi kama vile kuzuia watu kukusanyika ili kufanya ibada,kukusanyika katika viwanja vya michezo,kwenye masoko,n.k vinginevyo unaweza kuja kutokea mlipuko wa ghafla utakaotushinda kuudhibiti na tukalazimika kuchukua hatua hizi when it is already too late.

Kwa mfano,sioni logic ya Raisi kusema kaagiza vibali vya watumishi wanaokwenda nje ya nchi kudhibitiwa wakati wageni kutoka nje ya nchi bado wanaingia nchini tena kwa wingi tu kama hakuna tishio la ugonjwa huu.

Nchini Hispani kama siosei,serikali sasa inachukua hatua za kudhibiti raia wake kutoka nje ya majumba yao lengo likiwa ni kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huu.

Naelewa serikali ikichukua hatua hizi wakati huu ambapo hakuna mtu aliethibitika kuugua ugonjwa huu humu nchini,watu hawataielewa serikali na wataanza kulaumu ila ni wananchi hawa hawa watakaokuja kuilaumu serikali kwa kutochukua hatua mapema na hasa pale itakaposhindwa kuwahudumia wahanga wa gonjwa hili maana binadamu ndivyo tulivyo.

Inawezekana pia tunaangalia zaidi impact za kiuchumi zinazoweza kutokana na kuzuia ndege kuingia nchini kama vile kukosa mapato yatokanayo na watalii kuingia nchini ingawa sidhani kama na hao watalii kwa sasa wana moyo wa kusafiri huku hali ya ugonjwa ikiendele kuwa tishio duniani au tunahofia kuharibu mahusiano yetu na nchi zingine ila ni lazime tupime impact ya gonjwa hili kuingia nchini ukilinganisha na impact hizo za kiuchumi na za kidiplomasia.

Kama tunangoja mpaka ugonjwa uingie nchini kisha usambae na watu waanze kupukutika ndio tuchukue hatua,basi tusubiri wakati huo ufike alafu tutakuja kuona kama tumefanya maamuzi sahihi au laa.

Nayasema haya nikizingatia pia ukubwa wa nchi yetu,umasikini wetu na teknolojia duni tuliyonayo kama Taifa kuweza kukabiliana na milipuko ya magonjwa achilia mbali uewlewa mdogo walionao watu wetu.
Fact indeed.
 
Ibada tena zizuiwe wakati ndizo zinazotakiwa kutumika kwa kumuomba Mungu atuepushe na hili janga.
 
Ibada ni mkusanyiko usiokuwa lazima? Ndugu yangu hata kama huna imani usidhihaki wenye imani zao
 
Ibada tena zizuiwe wakati ndizo zinazotakiwa kutumika kwa kumuomba Mungu atuepushe na hili janga.
Mungu katupa akili na maarifa tuvitumie ili tuweze kuishi maisha bora tofauti na sio tuishi kama wanyama wasio na akili,maarifa na utashi.
 
Ibada ni mkusanyiko usiokuwa lazima? Ndugu yangu hata kama huna imani usidhihaki wenye imani zao
Panapokuwa na janga au tishio kama hili, mikusanyiko ya lazima ni kama ile ya watu kukutana na kukusanyika sehemu za matibabu (mahospitalini) na mikusanyiko mingineyo yenye.umuhimu/ulazima kama huo.
 
Haya Sasa..kitu kishasoma bongo

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Back
Top Bottom