Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Mbali na kusababisha madhara ya kijamii ni wazi corona itaathiri uchumi wetu kwani inagusu sekta muhimu kwa uchumi wa nchi yetu ambayo ni sekta ya utalii,sekta tunayoambiwa inachangia asilimia 25 ya mapato ya nchi yetu.
Vile vile ikitokea ugonjwa unasambaa na kutulazimisha kufikia hatua ya ku-restrict movement na shughuli za watu,sekta nyingi zaidi zitaathirika na hivyo kuongeza hatari ya kuporomoka kwa uchumi.
kwa maana hiyo, kama kweli Bajeti yetu haiangalii athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ugonjwa huu kama Mhe.Mbowe alivyodai Bungeni,sitashangaa kuona siku moja tunalazimika kuwa na Bunge la dharura kupitia upya Bajeti yetu au kuwa na vikao vya Bunge vya kupitia upya Bajeti yetu katika mojawapo ya mikutano ya Bunge iliyopo katika ratiba za Bunge.
Japo kuna taarifa za mashirika na taasisi za kifedha kutoa mikopo kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na corona pamoja na mapendekezo ya kutufutia madeni, sidhani kama hatua hizi zinaweza kutunusuru ukizingatia uwezekano wa ahadi hizi za mabeberu kutotimizwa kabisa au kutotimizwa kwa asilimia mia moja.
Hivyo,ushauri wa Mbowe na ule wa ACT uzingatiwe, vinginevyo ipo siku tunaweza kujikuta tunalazimika kutekeleza ushauri huo tukiwa tayari tumechelewa.