Kama tumeshindwa kuinua uchumi kwa rasilimali zilizopo hatuwezi kuuinua kwa tozo

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika Tanzania ni moja ya nchi zilizobarikiwa kuwa na RASILIMALI nyingi sana. Tanzania ina
  • Maziwa
  • Mito
  • Mabawa
  • Mbuga za Wanyama
  • Mabonde
  • Milima
  • Ardhi
  • Watu
Pamoja na Vyote hivi Tanzania ni nchi huru kwa Miaka 60 sasa bado Tanzania ni nchi masikini.

Tumewasikia viongozi wetu Wakijitatapa kuwa Wanataka Kujenga uchumi kwa Kutoza wananchi masikini tozo la Miamala ya simu.

Najiuliza kama Tumeshindwa kujenga uchumi kwa rasilimali hizo hapo Juu Kweli tutajenga uchumi kwa tozo la Miamala ya simu?
tatizo la Tanzania ni siasa na uongozi.

Na hayati Baba wa taifa aliwahi kusema ili tuendelee Lazima tuwe na Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora ,Tatizo ni Kutokuwa na siasa safi na uongozi bora.

Ili kuyaondoa hayo suluhisho ni Katiba Mpya tusitafute mchawi hatujarogwa.
 
MADINI pia umesahau.

Tanzania pekee inatoa madini aina ya TANZANITE.

Hivyo tungeweza kuwa nchi tajiri kwa kupanga bei tuitakayo.
 
MADINI pia umesahau.

Tanzania pekee inatoa madini aina ya TANZANITE.

Hivyo tungeweza kuwa nchi tajiri kwa kupanga bei tuitakayo.
Watanzania wengi wanafiki tu, Magufuri alipoingia tu madarakani kaanza kubadilisha vipengele vya Sheria za madini ili yaweze kutunufaisha.

Watanzania walianza kumtukana matusi ya nguoni,wakaanza kumtishia kuwa atafirisi nchi, tutashitakiwa miga,kina Kabendera wakaanza kuandika nakala kwenye forms za kimataifa kuonyesha kuwa Magufuri ni Rais asiyefaa (Burudooze) kajenga ukuta mererani kwa kejeli na matusi makubwa, na kilichomsaidi kupunguza matusi, ni kuibuka kwa akina Raither, hii tufikie Marengo tunaitaji watu kariba ya Magufuri hawamu kama tatu hivi, maendeleo hayaji kwa kubembelezana.

Nchi kama China urusi mataifa yote yenye maendeleo makubwa waliweka Sheria kali ili kuweza kufikia mafanikio,huku ukiweka sheria za kukusanya kodi, unaambiwa utafukuza wawekaji, it's shame.
 
Kwani pamoja na kubadili hizo sheria madini yamesaidia nini mbona tumekimbilia tozo? Hii nchi ina tatizo sugu la siasa chafu na uongozi wa hovyo viongozi wanavurunda hakuna kuwajibika wanalindana unatarajia nini.
 
Back
Top Bottom