Kama tumeridhika yanini malumbano???

Nov 10, 2016
32
16
Wanajamvi nawasalimu!!! Tuliaminishwa kwamba asilimia 96 ya watanzania wanaridhika na utendaji wa Serikali!!! Sasa najiuliza kwanini tulalamika tena juu ya vimambo vidogovidogo kama eti vimkopo vya elimu ya juu, vidawa vimepotea kwenye mahospitali, eti maisha yamekua magumu, eti bado kuna watu wanataka mikutano ya kisiasa ya hadhara ya nini sasa wakati asilimia nne tu ndio wanaolalamika?? Sizonje ameamua kwenda na asilimia tisini na sita na ile nne kaachana nao!!!
Sizonje kuna ka usemi kanasema wengi wape wachache wasikilize maana inawezekana ukawa nao wengi wasiojielewa na wachache wanaojielewa!!!
Sitaki kukukumbusha ya kua wewe ni baba wa wote waerevu na sisi tusiojua kitu na vile vijiswali kuhusu mikopo, madawa, maisha kuwa magumu na vijiswali vingine vingi tu!!
Hakika tunaolalama si wote ni wapiga dili la hasha!!! Wengine hatujawahi hata kuonjeshwa unachakiitadili!!" Pengine tulipiga deal indirectly yaani tulikua tunaingiza vipato tukidhani ni halali na kodi tukikatwa kumbe ilikua haramu loh!!
Wapendwa hapa hakuna cha CCM wala CDM hapa ni mkorogano tu!! Maana hakuna njaa inayouliza hapa kuna chama gani wala wewe ni itikadi gani?
Mungu tuokoe kwanza kabla ya kutubariki maana sijaelewa wapi tunaelekea kwa sasa!! Mimi na watu wangu ndio dua letu si kwa wote maana kuna watu wapo peponi hapahapa duniani!!
Tujaalie uvumilivu na unyenyekevu ee muumba wa vyote na wote!! Waliopo magerezeni kwa sababu za uonevu ingiloa kati!! Waliokosa dawa baba waponye na wadhulumiwa watetee baba!!Laana ya mto Ruvu ni ya waliotenda uhalifu huo si ya watanzania wote tuhukumu individual not as nation kwasababu ukweli waujua wewe na si kiumbe chochote kile!!
 
13dd2eab4e76fc3cefd83160a9a9ca0a.jpg


SITAKI SHARI
 
Back
Top Bottom