Kama tuliwahamasisha wananchi kujiandikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa basi na fomu za kugombea tuwape kwa moyo mweupe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,615
141,445
Niwe mkweli wanabodi, binafsi napendelea kuona vyama vyote vinasimamisha wagombea kila mtaa ili chama changu CCM kipate fursa sahihi ya kupima jinsi kinavyokubalika.

Serikali imetumia nguvu kubwa kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga na " kupigiwa" kura hizi haki mbili zinakwenda sawia.

Hivyo wagombea wote wenye sifa bila kujali itikadi ya vyama wapewe fursa ili wananchi wenyewe wakaamue kupitia box la kura.

Binafsi ninaamini kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo itakuwa ni rahisi zaidi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mwananchi mwenye akili timamu kuchagua Upinzani.

Maendeleo hayana vyama!
 
@="johnthebaptist,

Ninapendekekza tubadili taratibu zetu za uchaguzi kwamba wagombea wawe wanachukua fomu na kujulikana kwanza ndipo taratibu za kujiandikisha zianze rasmi baada ya kuwajua wagombea.

Hii italeta hamasa kubwa na kuondokana na hali hii ya hovyo ya kuwabagua watanzania wanaotaka kuomba nafasi ya kuwaongoza wenzao.

Jamani kubaguana kunakera sana, watu wapewe fomu wagombeee kuna tatizo gani?
 
Ndi
Kuna tofauti kati ya CCM na wasimamizi wa uchaguzi, usichanganye mambo!
Ndiyo lakini , CCM tunachangia sana kwenye aibu hii.
Likitolewa tamko la kiungozi kwamba yeyote anayahusika kuharibu uchaguzi atashughulikiwa ipasavyo, na wakaanza na hawa ambao wameshaanza ubaguzi, hali itabadilika.

Tatizo wahusika wako kimya. Kweli sipendi hii hali.
 
@="johnthebaptist,

Ninapendekekza tubadili taratibu zetu za uchaguzi kwamba wagombea wawe wanachukua fomu na kujulikana kwanza ndipo taratibu za kujiandikisha zianze rasmi baada ya kuwajua wagombea.

Hii italeta hamasa kubwa na kuondokana na hali hii ya hovyo ya kuwabagua watanzania wanaotaka kuomba nafasi ya kuwaongoza wenzao.

Jamani kubaguana kunakera sana, watu wapewe fomu wagombeee kuna tatizo gani?
Kama Simba na Yanga.....wagombea wanachukua na kurudisha fomu ndipo wanachama wanaandikishwa/ hakikiwa kushiriki uchaguzi!
 
Kwa hili naunga mkono 100%.wagombea wote wanaotaka kugombea wapewe fomu bila kinyongo.

Ningelikuwa jaffo ningechukua hatua dhidi ya wasimamizi wote wanaotaka kuharibu zoezi hili.kila mgombea apewe fomu, wananchi waamue kupitia sanduku la kura.Tanzania Ni nchi yetu sote.
 
Nilifikiri ungeandika kama kweli mh John Joseph Pombe Magufuli anakubali kweli anayo ya fanya yana wamulika wananchi wake aka wanyonge wake.

Tunaka kuona kwa vitendo uchaguzi huru na haki sawa kwa viongozi wetu wote wakionyesha umahiri wao, kuongoza taifa kulifikisha kwenye maendeleo bora moja kwa moja kutoka juu mpaka chini nasio hila hila zenu za mara polisi mara uhujumu uchumi
 
Wasiochangia Mwenge wasipewe form bila ya kujali wanatokea Chama gani kwa kuwa wanakuwa wamekosa kigezo cha uzalendo kwa kupuuza Tunu ya Taifa
 
Wasiochangia Mwenge wasipewe form bila ya kujali wanatokea Chama gani kwa kuwa wanakuwa wamekosa kigezo cha uzalendo kwa kupuuza Tunu ya Taifa
Hahahaaa...... Kuna watu bila mbio za mwenge wasingekuwepo katika ulimwengu huu!

Hivi mwenge uliasisiwa lini vile?
 
Hakukuwa na haja ya kujiandikisha na wala hakuna haja ya kupiga kura kwakuwa CCM wameshapanga kugombea wenyewe vinginevyo wasingekuwa wanawazuia viongozi wa upinzani kuchukua fomu za kugombea
Kupiga na kupigiwa kura ni haki yako ya kikatiba!
 
Back
Top Bottom