GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Hiki kitendo kama tukikiacha basi Wasomi tuliopo Tanzania tutaonekana wote ni wa hovyo hovyo kwani kinachofanyika sasa ni kupuuza sauti nyingi za Watanzania walioguswa na upuuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda ( siyo jina lake halali ) kwa aliyemteua kushindwa kumng'oa ( kumtumbua ) Madarakani.
Nakumbuka mwaka jana November kuelekea December CEO wa Whistle blowing site JamiiForums Ndugu Maxence Melo alikamatwa na kupata usumbufu wa hapa na pale lakini ni sisi sisi humu JF na katika Mitandao mingine tuliweza kuunganisha nguvu moja na kupaza sauti ya kutaka aachiwe huru na kweli Sheria ikachukua mkondo wake na akapata haki yake ya Kikatiba na leo tunatiririka nae mitaani kama kawaida.
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda ( siyo jina lake halisi ) ameingia katika shutuma kama siyo tuhuma kubwa sana ya Kufoji Cheti cha Kidato na nne na kutiririka nacho mubashara kinyume na Sheria za nchi na hata za Mwenyezi Mungu / Allah.
Kinachotusikitisha sisi tunahangaika kupambana Makonda ang'olewe Madarakani lakini Mteule wake ndiyo kwanza anazidi kuburudika na Juice, Pipi na Korosho zake pale pande za Magogoni hali ambayo inaonyesha kuwa ni kama vile tunapaka rangi upepo.
Nitoe tu RAI yangu kwenu Wana JF kama tuliweza kupaza sauti zetu ambazo kwa namna moja ziliweza kusaidia kupata haki kwa Ndugu yetu Maxence Melo na akaachiwa kwa dhamana basi niwaombe tu kuanzishwe Kampeni MAALUM ya kupinga kuendelea Kuongoza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda ( siyo jina lake halisi ) na tusinyamaze hadi pale mla Pipi,Juice na Korosho atakapochoka na mikelele yetu na hatimaye amtumbue.
Katika hili tukinyamaza au kulipotezea nitaanza rasmi kuwadharau Wasomi wa nchini Tanzania kwani kiuhalisia tunaodhihakiwa hapa ni sisi sisi Intellectuals wa Kutukuka ambao kimsingi tunaongozwa na Intellectual feki ambaye takwimu zinasema alianza kuchemsha tokea akiwa darasa la Saba na akaja kugotea kidato cha Nne na leo anatusumbua na usomi wetu halali.
Tuamke rasmi, tupambane na tusichoke hadi Ndugu Paul C. Makonda ( siyo jina lake halisi ) ang'olewe madarakani.
Kila la kheri nyote.