Kama tuhuma dhidi ya Kinana zilikuwa siyo za ukweli basi Msigwa ana uwezo mdogo wa akili. Kama zilikuwa na ukweli basi kuna dili lilichezwa

Kejuu

New Member
May 20, 2020
3
45
Ndugu watanzania wenzangu,

Natumaini mko salama.

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza. Nilimsikiliza kwa makini sana ndugu Msigwa wakati akiongea na wanahabari kuhusu kuomba msamaha kwa Kinana dhidi ya tuhuma za ujangili alizozitoa bungeni. Katika maelezo yake, mambo mawili niliweza kuyadadavua: (a) Kama tuhuma zilikwa siyo zaukweli, he is really a low-IQ political leader ever, na (b) kama zilikuwa na ukweli, basi kuna dili limechezwa kati ya hawa watu wawili kulinda maslahi yao.

Kwanini Msigwa nimemuita a low-IQ political leader ever? Kwanza kabisa na mnukuu “Katika kesi hiyo iliyosikilizwa na kuhukumiwa na jaji Zainabu Mluke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya mahakama. Leo nakiri mbele yenu, kupitia ninyi mbele ya watanzania kwamba, tuhuma hizo nilizozitoa mara kadha dhidi ya Kinana, hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote, taarifa nilizopewa nakuzitumia hazikuwa na ukweli bali malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nachukua full responsibility, kwa sababu mimi nilikuwa waziri kivuli, nilipaswa nifanye homework yakutosha pamoja na kwamba taarifa hizo nilipewa na mtu ninayemuamini”………

Kwanza nilianza kwa kutafiti ili nijue kiwango cha elimu cha msigwa, nkaipata CV yake ambayo inaonyesha, Msigwa ana shahanda ya kwanza (Theology) 2004-2007, All African Bible College, Durban, Kwazulu Natal, South Africa (ABBC-Durban). Hii ndiyo elimu ya juu aliyonayo ndugu Msigwa kwasasa. Kwa kiwango hiki cha elimu, na wadhifa wa uongozi aliokuwa nao (waziri kivuli-mali asili na utalii), siamini kama kweli alikuwa hajui kama hauna nyaraka za kuthibitisha unachokisema, utakuwa unaudangaya umma.

Isitoshe, sina uhakika kama Msigwa hakujua kuwa kauli zake hizo tayari zimeathiri reputation yake (Hapa na maana ya kwamba, Msigwa atakuwa na ujasiri gani tena wa kuuambia umma kwa jambo lolote lile?). Hii inafanana na tuhuma za ufasidi walizompa Lowasa, baadae hao hao wakamsafisha akawa tena siyo fisadi, na jambo hili (political gambling), imeathiri taswila ya chama mpaka leo. Upeo wa kufikiria wa Msigwa hapa ulikuwa mdogo sana, inaonekana maslahi binafsi yalitawala bila kufikilia kwa kina ni kwa kiwango gani hizi kauli zinaenda kuiathiri his political career.

Msigwa alitakiwa ajifunze kwa Dr. Slaa, mzee huyo alikuwa akiambatana na nyaraka kwa kila tuhuma aliyokuwa akiitoa kwa serikali au mtu binafsi. Hapa naona thamani ya mzee Slaa ndani ya CDM. Kutokuwepo kwa mzee huyu, chama kimekosa watu weledi na focus ya c hama iko dilemma mpaka leo. It is time to go back to the drawing board, au Chama kitafute mathink tank wapya.

Hawa wawili (Msigwa na Kinana), kunauwezekano wamekula dili pamoja. Inawezekana ushindi wa Kinana uliambatana na Msigwa kutakiwa kumlipa Kinana findia ya kumchafua, na inawezekana ni hela ndefu sana ambayo msigwa ilimshinda kuilipa (just my speculation), ndiyo ikampa kinana fulsa ya kumwambia Msigwa amsafishe mbele ya umma (you scratch my back I scratch yours).

Nawasilisha kwa majadiliano

Kejuu
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,189
2,000
Kila kitu kaweka sawa, labda kama kuna lingine. Mh Kinana baada ya kuona amechafuliwa kwa tuhuma ambazo aliamini siyo za kweli alikwenda mahakamani kutafuta haki yake.

Mahakama ikamtia hatiani Mh Msigwa, ambaye kwa mujibu ya maelezo yake ya kuomba msamaha moja kwa moja unagundua kuwa ni sharti alilopewa na Mh Kinana ili walimalize shauri lililoko Mahakamani kiungwana.

Mh Kinana ni Mwanasiasa mzoefu na aliyejitosheleza anafahamu harakati za siasa zina vita vya kweli na vya kubumba.

Anafahamu kijana aliteleza hivyo hana haja ya kumkazia. Kwa kuwa ameelewa kosa lake kupitia mahakama amemtakia kheri katika harakati za kisiasa zaidi kuliko kummaliza.

Mh Slaa naye pia aliwahi kutamka hadharani kuwa kuna lori linapita mpaka wa Tunduma likiwa na karatasi za kupigia kura , amepewa taarifa , aliyasema hayo akiwa jukwaani mkoani Singida.

Ilipofuatiliwa taarifa zilikuwa siyo sahihi, hata yy alikubali na kusema ni kweli alipokea taarifa isiyo sahihi.

Mwanasiasa hayo ni mambo ya kawaida na hata kuomba msamaha ni kitu cha kawaida.
 

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
3,390
2,000
Nilivyomwelewa ni kwamba source yake ya habari haikumpa taarifa sahihi na he relied on that na baadaye ndipo alipogundua siyo kweli. Otherwise, si vizuri hata kidogo kumzushia mtu kashfa na kuishia kusema "I am sorry". Pengine kama unavyodhani alienda kumwona mhusika na akamshauri kama anataka amsamehe basi yeye mwenyewe aseme kwa maneno yake kwamba alimsigizia uwongo. Huenda ni hivyo.
 

ngulukizi

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
219
1,000
Tunachojifunza ni kuwa tusipende kushabikia maneno ya wanasiasa mana huongea wakiwa na lengo la kichafua wenzao ili wao wafaidike mwisho wa siku siye wafata mkumbo tunaumbuka kama hili la Kinana tulishabikia sana leo tunakula matapishi yetu
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
6,571
2,000
"Mchngaji" Peter Msigwa si tu amejichafua, lakini ile kitu wazungu wanaita intergrity, imeporomoka mmpaka sifuri.
Angalia vizuri "Mchungaji" nimewekea inverted comms kuonyesha kuwa hata hadhi ya kulisha kondoo sasa hana, hawezi kuwa mwongo na akawa mchungaji wa kanisa lolote la Kikristo.
Mtu mwongo n muuaji.
Msigwa alipata wapi ujasiri wa kuongea unsubstantiated claims ambazo zingepelekea kuumizwa au kuuwawa kwa Nd Kinana?
Amri moja ya Mungu kati ya zile kumi: "USIMSHUHUDIE MTU UONGO"

Katika hili Msigwa amefeli, na kalazimishwa kukiri kutokana na amri za kimahakama, otherwise angeishi na uongo huo dama dumu.
 

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,088
1,500
Ukitaka kujua ujinga wa watu ndio hapo na ndio utajua kwamba chama cha kuing'oa CCM bado hakijazaliwa,hizi ndio akili ambazo unaweza kusema eti mtu ana utimilifu wa akili kweli?wameona wamtumie yy kwa sababu anajiita mchungaji kwamba watu wataamini upumbavu wake kirahisi,Kikwete alitufundisha kwamba za kuambia changanya na za kwako sasa bwana msigwa yy amebeba za kwake na ameangukia pua hata kama ni kutumika sio hivyo yeye anasahau kwamba sasa anaiambia jamii ya watanzania kwamba mambo mengi sana yanayosemwa na upinzani bungeni yamejaa uongo mkubwa sana na kwa sababu hivyo Rais wetu ni mzuri kuliko kawaida na kuanzia sasa jamii ya WATANZANIA isisikilize tuhuma zozote dhidi ya viongozi wa serikali maana ni uzushi mtupu,huyu anajiita mchungaji akumbuke kwamba kina watu wameumia sana baada ya kusikia jinsi nchi inavyohujumiwa na wengine wamekufa kwa pressure kwa sababu tu mchungaji fulani alisimama na kuongea uzushi kwa kutafuta populality.Ndugu zangu watanzania unaweza kuhoji mambo mengi sana juu ya misamaha ya kijinga na kipumbavu kama hii inayotolewa na watu tuliowaamini kwamba ni makini na wana akili kumbe ni hamnazo ni wakati sasa tuamke tusije poteza maisha kwa siasa kama hizi za kitanzania na kiafrika kwa ujumla.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom