battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,672
- 2,539
Hapa naanza kuona machungu ya kila siku Tanzania kufungwa sisi tuu?, tumegeuzwa kichwa cha mwenda wazimu.
Lakini kwa upande mwingine nachelea kusema ni aina fulani ya ROHO MBAYA WALIYONAYO NDUGU ZETU WA TANGANYIKA DHIDI YA ZANZIBAR(yaani TFF dhidi ya ZFA) pale walipoomba kutambuliwa na FIFA na CAF na kutakiwa wapate saini ya TFF KAMA MDHAMINI WAO kwa vile wao ndio wanaosimama kwa jina la Tanzania (sovereign).
Hivyo hivyo siku ile timu ya Zanzibar ya vijana(Zanzibar Herro) ilipocheza na Bara na kuifunga, wenzetu Bara wakatununia, na siku tulipoingia fainali na Kenya wakahiari kutupikia majungu ili kenya ishinde kulikoni sisi ndugu zao.
Hapa naona jambo la Muungano halikuleta udugu wala mapenzi baina yetu,na ndio maana kila siku wenzetu Bara hujivutia maslahi kwao tuu na hata kusababisha Miradi ya Kiuchumi ya Zanzibar kama Bandari ya Mpiga duri,Uwanja wa Ndege wa Unguja,na Barabara ta wete mkoani ambazo tayari tumesha pata ufadhili, wao watie saini kama mdhami tu kwa vle wao ndio wenye (sovereign) wametukatalia eti wakidai kuwa Bandari ya Mpiga duri itauwa Bandari ya Dar.
HIVI KUMBE ZANZIBAR SI TANZANIA !?
Ndio maana jana nimeona Vijana wa kizanzibari wakiishangilia SENEGAL DHIDI YA TAIFA STAR
Nlishangaa lakini ndio ukweli wenyewe ,unyama unyama tuu, ila hali si nzuri Muungano wetu Uko mahskani
TUJADILI