Kama Tanzania tumeamua kufuata mfumo wa kinga ya jumuia (herd immunity) tufanye haya kupunguza maafa

microbiologytz

New Member
May 2, 2020
1
3
Utangulizi

Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona umevamia kila nchi duniani na kila nchi imeamua namna yake ya kupambana nao

Kwa sasa kuna namna kuu mbili zilizoko duniani ni kupunguza maambukizi (flattening the curve) na Kinga ya pamoja au ya jamii (Herd immunity). Kila moja ina uzuri na ubaya wake kutokana na mazingira ya nchi husika

Kinga ya jumuia (herd immunity) ina maana watu wengi wapate maambukizi na wapate kinga (immunity) dhidi ya vijidudu vya Corona, ikiwa na maana wakishapata hawawezi kupata maambukizi mapya hivyo watazuia watu wengi wasipate. Ili kujua tumefikia wapi kufikia kinga ya jumuia toka tutangaze mgonjwa wa kwanza march 16 mpaka leo inabid tupime kinga za mwili (IgG) dhidi ya ugonjwa huu kwenye jamii umefikia ngapi.

Kupunguza maambukizi (Flatten the curve) hii nia yake kubwa ni kupunguza watu kuumwa kwa wingi kwa wakati mmoja na kulinda huduma za afya kwani wakiumwa wengi hospitali zitashindwa kuwahudumia

Njia zote zinapendekezwa ila hatujui ipi itafaa muda ndio utahukumu muhim kujua kwa eneo lako,uwezo wako ipi unaweza kuifuata. Kwa hali ilivyo sisi inaelekea tumeamua kufuata nadharia kupata ya kinga ya jamii (herd immunity)

KInga ya jumuia hapa Tanzania
Kwa hali ilivyo Tanzania hasa katika miji kama Dar es salaam na Zanzibar bila shaka watu wengi sana wana maambukizi ila kwa kuwa wanaafya njema hawajaonyesha dalili. Ikumbukwe hii namba tunayotangaziwa na idadi ya watu waliopata dalili kali wakaenda hospitali wakapima . Kwa hiyo wengi zaidi wako wanaendelea na shughuli zao wakiwa hawana dalili kabisa au dalili chache wanazojitibu wenyewe.

Tanzania kadiri ya umri wa mtu kuishi (life expectancy) ni miaka 64 .Huu ugonjwa unaathiri zaidi umri unavyozidi kusogea hasa ukiwa na miaka zaidi ya 60 pia ukiwa na wowote ugonjwa wenye kudhoofisha kinga ya mwili ( commorbities) mfano kisukari, presha unene, nk. Katika jamii yetu hawa watu sio wengi ukilinganisha na chi za Ulaya na Marekani

Nchi zilizoathirika sana kama Italy wengi waliofariki ni wenye miaka Zaidi ya 80 na ni kati nchi inayosifika kuwa na wazee wengi duniani. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wengi hapa Tanzania hasa Dar es salaam washapata Corona na wanakinga ila hawajajijua tu. Kuna utafiti umefanyika hivi karibuni New York Marekani wamegundua kuwa asilimia Zaidi ya 20% ya watu ambao hawakuwahi kuwa na dalili washapata maambukizi na ukumbuke wao tayari wao wako kwenye kufungiwa ndani(Lock down) sisi tuko huru tutakuwa tumeambukizana zaidi.

Ingawa wanasayansi wengi wanaamini nchi nyingi zilifungwa lockdown wakati tayari kiwango cha juu cha maambukizi kishafika ndio maana pamoja na lock down bado vifo ni vingi vimetokeo hata kuzidi nchi chache zilizoamua kufuata kinga ya pamoja (herd immunity) kama Sweden. Kwa lugha nyepesi Lockdown haijasaidia kitu kwani walifunga tayari maambukizi yashaenea na Tanzania kwa sasa nadhani tushafikia pointi hiyo.

Pia aina ya watu wanaoishi katika nchi husika. Nchi zenye watu dhoofu wenye maradhi mengi huu ugonjwa umewaathiri sana kuliko nchi watu wenye afya mfano Marekani wanasifika kuwa na maradhi mengi yasio ambukiza mfano presha kisukari nk ndio maana vifo viko juu.

Uzuri wa Kinga ya jamii/Pamoja (Herd Immunity)
Wanasayansi wote wanakubaliana kinga ya jamii ndio njia pekee ya kuondokana na haya maradhi. Swali gumu ni namna ya kufikia kinga ya pamoja.Nchi nyingi za magharibi zinakuja na dhana ya chanjo . Tatizo ni kwamba hatujui chanjo itapatikana lini kwani hata SARS ugonjwa ambao unasababishwa na kirusi ambacho ni jamii ya Corona toka 2003 kilipotokea mpaka leo wanasayansi hawajaweza kutengeneza chanjo.Hivyo kujifungia ndani kusubiri kitu ambacho hujui kitapatikana lini linaweza lisiwe jambo la busara.

Njia rahisi ya kupata kinga ni watu wengi waambukizwe ili walinde wale wadhaifu hii inatokea endapo asilimia 60-70 ya jamii ishaambukizwa. Uzuri wa hii inakukinga hata ukipata tena maambukizi mwili unakuwa unanguvu ya kupambana nayo ingawa swali linalokuja kinga hii inadumu kwa muda gani? Kwa kawaida ya virusi vinavyoshambulia mfumo wa hewa huwa sio ya kudumu ingawa inaujengea mwili uwezo mkubwa hata ukiupata ugonjwa tena hauwi mkali kama mwanzo.

Kwa hali ilivyo toka Marchi 16 mpaka leo inawezekana tunakaribia kufika kinga ya pamoja kwani kwani kwa kawaida wiki 4-8 toka ugonjwa uanze watu wengi tayari wanakuwa washapata.

Kwa sasa inabidi pamoja na kupima maambukizi mapya pia tupime kinga watu walionazo kwenye jamii na kiasi cha hizo kinga (IgG).

Changamoto za kupunguza maambukizi (flattening the curve)
Nchi zote ambazo zinafata mfumo huu zinafanya hivi zikitegemea kuwa karibuni itapatikana kana dawa ingawa sio rahisi kiasi hicho.

Changamoto kubwa ni kuwa watu walioifungiwa ndani (Lock down) wakiruhusiwa watoke itakuja wimbi lingine la maambukizi na vifo kama kawaida je watafanya lockdown tena na watafanya marangapi?

Na kitaalam ni kwamba inatakiwa irudiwe lockdown hivi mpaka ifikie hatua kinga ya pamoja(Herd Immunity) ifikiwe kwa chanjo au watu wote wapate maambukizi.Kumbuka lengo la flattening the curve ni kulinda mfumo wa afya usizidiwe na wagonjwa.

Changamoto za Kinga ya Jamii (Herd Immunity)
Kinga ya jamii ni kitu bora sana ila kina kuja kwa gharama kubwa kwani watu wote ambao hawatamudu maradhi wataugua na wenine watakufa kwa wakati unaokaribiana. Hii itasababisha janga kubwa hospitalini kwa kushindwa kumudu idadi ya wagonjwa.

Tupige hesabu za mkoa wa Dar es salaam ambao una idiadi ya watu wanao kadiriwa kuwa milioni 6, tafiti zinasema asilimia 20% ndio watapata dalili hivyo ni watu wastani ya watu milioni moja laki mbili (1,200,000) katika hawa asilimia 5% wanaweza hitaji kulazwa. Hii ina maana mkoa wa Dar es salaam pekee watu 300,000 wanaweza kuhitaji kulazwa.

Sasa tujiulize je kwa hospital za Dar es salaam zinaweza mudu idadi hii ya wagonjwa watakao kuja hospitalni kwetu.Je zinaweza kulaza wagonjwa laki tatu(300,000)

Hesabu hizi ndizo zilizofanya nchi za magharibi zilizokuwa zinafata mapango wa Kinga ya jumuiya( Herd Immunity) kuuacha na kufuata wa flattening the curve ili kupunguza idadi ya wagonjwa watakaoshindwa kuhudumiwa na huduma za afya.

Pia ikumbukwe mfumo wa hospitali za umma nyingi zilishazidiwa hivyo ukiongeza idadi ya wagonjwa wengi hivyo hali itakuwa mbaya sana.

Watu watakoaathirika ni watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama kisukari,Presha nk ambao huwa wanahitaji huduma za dharurua mara kwa mara. Pia watu wenye maradhi mengi yanayotibika watashindwa kwenda hospital.

Hii itasababisha idadi kubwa ya vifo toka pande mbili ya wagonjwa wa Corona na pili wagonjwa watakaopoteza maisha kwa kuwa mfumo wa afya haufanyi kazi ipasavyo

Changamoto za upimaji
Corona ni ugonjwa mpya hivyo pia vipimo vingi bado havijathibithishwa uwezo wake wa kupima. Kwa hivyo wengi wanatumia PCR hii inapima vinasaba vya virus kwenye sampuli inayochukuliwa kwenye njia ya hewa. Tatizo ni kuwa machine haiwezi kutofautisha kirusi hai na kilichokufa. Mfano hivi karibuni Korea kusini wamesema watu waliowapima waliosema wamepata tena maambukizi hawakuwa nayo bali wallikuwa na virusi vilivyokufa ambavyo PCR machine haiwezi tofautisha . Machine hii kutegemeana protokali yake inaweza pima sampuli moja ndani ya saa 1-4.

Nyingi ambazo zinatumika sasa ni zinamtegema zaid mtalaam (manual) ndizo zinatumia muda mwingi ila hizi zinazo jiendesha zenyewe(Automatic) zinatumia muda mchache zaid angalu saa 1. Mfano afrika kusini wanatumia Gene Xpert ambayo inatumia dakika 45 kwa sampuli moja kumaliza sampuli moja.Kila machine ina uwezo wake wa kuchakata sampuli ngapi kwa wakati mmoja kutokakana na ilipotengenezwa. Kama machine inauwezo wa kuchakata sampuli tisini na sita kwa mara moja na protokali yake ni masaa manne hivyo kila baada ya saa 4 tutapata majibu 96 kama kila kitu kilienda sawa.

Njia nyingine ni kupima kinga mwili hii ni nzuri na kwa nchi yetu tunatakiwa tuanze kupima hii kama tukianza kupima kwenye jamii badala ya kupima virusi kwani toka ugonjwa uanze watu wengi watakuwa washapata

Tukionyesha data zetu tutajua tuna safari kiasi gani kufika herd immunity na pia tunaweza hata kufungua mipaka yetu mapema zaidi kwani hatuogopi tena haya maradhi.

Changamoto za utoaji takwimu
Katika kitu kinasikitisha katika hili janga utoaji takwimu umekaa kishabiki kuliko kitaalam kote duniani hasa katika vyombo vya habari. Namba za maambukizi zinasubiriwa kama matokeo ya mpira .Watu wanakufa sababu nyingi ajali,kujiua,njaa nk kwanini tusitangaziwe kila siku bila shaka kwa kuwa ni ugonjwa mpya basi tupewe taarifa za kina zilizochambuliwa sio za jumla jumla. Kila chombo cha habari kinatangaza kila siku wamekufa watu wangap kwa kila nchi.

Huwezi linganisha vifo vya nchi ya China ,Marekani na Italy. Kwanza nchi ina watu wangapi China 1.4 billion, Marekani Milioni 330 na Italy milioni 60. Pia kundi gani linaathiriwa zaidi umri, kipato na hali ya kiuchumi mfano wa Marekani na Waingereza wanasema weusi ndio wanaathirika zaidi ingawa ukweli ni kuwa tatizo ni umaskini wao ndio wanaishi wengi nyumba moja wanakula vyakula vya barabarani( Junk food) inawasababishia unene na maradhi yasiyoambukiza ukilinganisha na jamii zingine . Pia inabidi watoke nje pamoja na lockdown wafanye kazi hatarishi na hata mahospitalini kwa wao ndio wako mbele kuona wagonjwa kwa kuwa wako level za chini.

Na katika uhalisia hamna data za uhakika za Corona kwani kila nchi kwani kila nchi mpango tafauti wa kupima mfano Ulaya na Marekani wanapima wenye dalili tu. Korea na Afrika kusini wanapima kwenye jamii hata wasio na dalili. Idadi ya vifo ni kwa takwimu rasmi zile zinatoka hospitali na zinazotangazwa na serikali . Uchina waliongeza idadi hivi karibuni, Uingereza walikuwa hawajumuishi watu wanaofia kwenye nyumba za wazee pia tuisahau kuna wanaofia nyumbani.

Tutegemee nini kwa kufuata dhana ya kinga ya Jamii (Herd immunity)
Kwanza tujiandae kisaikolojia ya kutokea vifo vingi sana WHO ili kadiria kuwa watu 112,000 wanaweza kufa kwa corona nchini Tanzania.

Hivyo misiba itakuwa mingi pia ikumbukwe kutakuwa na watu wengine wengi watakufa kutokana na ukosefu wa huduma za afya .Wagonjwa wengi wanaohitaji huduma za dharura waweza kufa kwa kuwa hospitali zimejaa hii ina maana mtu anaweza kufa kwa magonjwa ya kawaida kama malaria au kuishiwa maji au sukari mwilin wakati anasubiri kupata huduma za afya.

Wagonjwa na wazee wasioweza toka majumbani wataletewa Corona na ndugu zao wanotembea mtaani ambao hawatakuwa na dalili.Wagonjwa hawa kwa kuwa wana kinga dhaifu watazidiwa haraka na wanaweza kufia nyumbani.Hii itaongeza sana idadi ya wanaofariki

Pia wale ambao watapata bahati ya kupokelewa hospitalin je kutakuwa na machine za kupumulia za kutosha au mitungi ya oksijeni

Tufanyeje kama nchi katika wakati huu
Mji kama Dar es salaam inakaribia kufikia Kinga ya jamii( Herd immunity) hivyo njia kama kutenga jamaa ya mtu mwenye ugonjwa hazina ulazima. Wagonjwa ambao wanapimwa wana dalili chache hawana sababu ya kwenda hospitalini. Hospitali ihudumie wagonjwa waliozidiwa tu.

Tutafute vitendanishi ambavyo tutajua kinga ya watu katika jamii yetu hii itakuwa rahisi hata siku mipaka ikifunguliwa watu watajua nchi yetu ni salama na hatutugemei wimbi la pili au la tatu la maradhi kwa kuwa tayari tuna herd immunity

Tuweke mikakati maalum ya kuzika wapendwa wetu yasitokee yale ya Ecuador kwani jinsi tunavyokaribia kilele cha herd immunity ukweli mchungu ni kwamba misiba itatokea kwa wingi na mingine nyumbani.

Tuwe ni mpango kabambe wakuzika watu kwenye maeneoa yetu. Watu walioko kwenye jamii Mabalozi,Mwenyekiti wa mtaa na viongozi wa dini sehem husika wapewe mafunzo maalum namna ya kukabiliana na hali ya vifo vingi kama vikitokea na waweze kuzika .Hivyo kwa kutumia watumsihi waafya ya jamii au watu wengine watakao pata mafunzo maalum waweze kuhudumia watu watakofariki majumbani na vifaa vya kujikinga vipatikane kwa urahisi na bei nafuu.

Hii itaondoa tatizo la maiti kuchelewa kuzikwa kwani kila jamii watachukua tahadhari na kuzika wapendwa zao haraka.Jamii ikieleweshwa na watu wanaowaamini wataelewa na tutaondokana na tatizo watu kusubiri kuzika siku nyingi.

Ushirikishwaji wa sekta binafsi
Sekta binafsi hasa viwanda wangepewa maelekezo ya kutengeneza vifaa vya kujikinga (PPE) kwa wingi mfano Mask gloves na nguo maalum zinazotumika wakati wa kuhudumia wagonjwa wakiumwa na wakifa na kwa bei ya chini ili changamoto yoyote ikitokea watu wote wajue zinapopatikana.Mfano nchi ya uturuki ilitoa kazi kwa vyuo vya ufundi vishone Barakoa na wakagawa bure kwa wananachi sisi tunaweza kuvipa material standard kama mtaji na tukawavipangia bei ya kuuzia.

Uvaaji wa barakoa, kukaa umbali wa mita 1 na kuepuka mikusanyiko
Pamoja na kuwa tumeafuata mfumo wa kinga ya jumla bado umakini unahitajika watu wandelee kuvaa barakoa na social distancing (kukaa mbali) hii ina faida ya mtu katopata maambukizi makali. Vimelea vyovyote vya maradhi vina kiwango maalum pindi kikupatacho kupata maradhi. Kiwango kikiwa kidogo (infection dose) na mdudu asipokuwa mkali sana (virulence) basi mwili unaweza pata maambukizi madogo ambayo kinga ya mwili inaweza pambana nayo na bado utakuwa umeweza jenga kinga inayochangia kwenye herd immunity.

Kuepusha mikusanyiko na misongamano hasa sehem za biashara na starehe, kwa mfano sehem za biashara inaweza kuamuliwa kuwa pawe na zamu za kuuza hivyo kama watu 10 wanuza bidhaa moja watano wanakuja leo watano kesho. Kwa maana kupunguza uwingi wa watu hii pia inaweza kufanyika sehem zingine za biashara.

Sehem za ibada ingekuwa na jambo bora kufungwa ila kama mikusanyiko mingine kama sokoni na kumbi za starehe ziko wazi itakuwa vigumu keulewesha watu kwanini nyumba za ibada zifungwe. Hivyo waumini wasisitiziwe waepushe misongamano na wakiwa huko wafate masharti walio elekezwa.Sehem zote watu wakipungua na pakisisitizwa kuwa asiye na sababu asitoke nyumbani na watu wakiwa na elimu ya kutosha watu wenyewe watapapungua kwenda nyumba za ibada na sehem zingine.

Wakati huo huo kuna mikusanyiko inaweza kuendelea usiku hii pia serikali inaweza weka sheria ya mwisho wa muda wa kuonekana njiani kama wanavyofanya Kenya na Rwanda, kwani usiku ni vigumu kuhakikisha kama watu wanazingatia sharia.

Unaweza kujiuliza kwanini hizi tuendelea kuzifanya hizi wakati lengo ni kupata kinga ya jamii (herd immunity). Kupata herd immunity ni jambo bora ila bora tuifikie taratibu hasa ukizingatia huduma zetu za afya inabdi zipate wagonjwa kidogo kidogo.

Hospitali zote na taasisi zenye uwezo zipime
Serikali iruhusu hospital na taasisi yoyote kama vyuo vituo vya tafiti kama wanauwezo basi muhimu wanunue vitendanishi vilivyovyo halisi (original) vilivyopasishwa na mabaraza husika. Sampuli zenye zitazo pimwa zikaonyesha maambukizi zipelekwe maabara ya taifa kuhakikiwa.Hivyo mtu atapewa majibu ya kwanza akiambiwa una maambukizi ila kipimo cha pili kitaenda maabara ya Taifa kuthibitisha.

Hii itapungiza hali lkubwa ya sintofaham iliyopo mtaani kwani kuna watu wengi wanahamu ya kupima hata kwa gharama kubwa ila hawawezi.

Utumiaji wa dawa za mitishamba na dawa za asili
Jamii ya Afrika wameishi kwa kutumia dawa za asili kwa muda mrefu ila palikuwa na wazee wanaoshauri namna ya utumiaji, kiasi na madhara yanayowezekana kutokea. Changamoto ya sasa kila mtu ni mtaalam hivyo kiasi na madhara tutakuja kuyaona punde hili janga likipita.

Kwa sasa Tanzania inakabiliwa na janga kubwa sana ya maradhi ya figo na ini, wagonjwa wakusafisha figo(dialylisis) wakiongezeka kila siku wataalam wanaamin moja ya sababu ni utumiaji wa dawa za mitishamba bila viwango.Hivyo tuwe makini ugonjwa huu ukiisha tusije kuwa na janga lingine la maradhi mapya figo,ini mapafu kwa kutumia dawa za asili zisizo na kiwango.

Taasisi za Tiba asili itoe miongozo rahisi kufuata na kuandika madhara pindi mtu asipofuata muongozo ulioandikwa kiasi gani cha dawa mara ngap nk.

Tuwakinge tunaowapenda wazee na wagonjwa
Wazee na wagonjwa hasa wenye magonjwa ya kudumu wakipata haya maradhi watazidiwa na wanaweza hitaji mashine za kupumulia hivyo tuwakinge. Kwa familia zenye wazee bora wawatenge kwa na wakae na watu ambao hawatoki toki nje wakuwahudumia ili wasiwaletee maradhi au wawahamishie eneo ambalo ni salama ambalo sio rahisi kuingiliana na watu.

Pindi kinga ya jamii ikishathibiti basi wanaweza rudi na kuchanganyika na wengine kwani kinga ya jamii itawalinda

Pia hawa watu wakitengwa itapunguza mzigo mkubwa kwenye huduma za jamii kwani wengi wao ndio wanakuwa na dalili kali na wanaweza hitaji machine za kupumulia.

Ushauri wa jumla
Tupo vitani na adui yetu hatumjui na pia silaha bado hatujazijua kwanza kabisa tusitegemee nchi za nje kwani ni mabingwa wakutumia shida zetu kwa ajili ya kujinufaisha.Tujipange kwa kidogo tulichonacho.

Tukumbuke mashirka makubwa ya dawa mengi hayathamini utu zaidi ya faida hivyo nchi inabid iwe na mkakati wake binafsi unaoendana na tafiti za kisayansi zakupambana na hili janga. Kuna nchi zimeweza haya mfano Senegal

Kwenye swala la kinga ya jumuia Sweden ni mfano bora ya kuigwa.Hivyo hamna njia inayofaa kila nchi itumie wataalam wake wawe na mkakati wao kutokana na hali yao kupambana na virusi hivi.

Wenye maswali wanakaribishwa pia wenye maoni juu ya namna bora ya kupambana na maradhi haya.
 
microbiologytz, Bandiko lako lina maelezo marefu yasiyo na jipya. Mods bandiko kama hizi zingeunishwa tu.

Kwa ufupi COVID-19 kwa sasa haina dawa ya kinga wala kutibu, njia iliyopo ni maamuzi ya dhati ya kila mtu duniani KUJILINDA HAWALINDE wengine dhidi ya maambukizi.

Kama ilivyo kwa UKIMWI, jisalimishe kwa kipimo. Ukijua umeambukizwa jifungie na kutumia tiba mbadala km kujifukizia. Kama huna maambukizi chukua tahadhari zaidi ya kujikinga.

Ni uzembe, jeuri na ujinga kusubiri Serikali ikusimamie kuchukua tahadhari. Wale wanaoilaumu Serikali kwa janga hili ni wenye nia ovu na inawezekana ni wahusika wakuu wa kusambaza. Kwa wale, wa aina hii wanaojulikana, kaa nao mbali. Wale wasiojukikana, amini kila mtu ni mwathirika hivyo mwogope kama ukoma na zingatia ushauri wa kitaalamu.

TUBADILIKE KITABIA WAKATI NDIO HUU
 
Ila tumetoka mbali sana, yaani tulishikwa masikio kweli kweli na story za covid,

R.I.P Jiwe, sasa dunia nzima imekuelewa.
 
Ewaaaah, sasa hii ndiyo mikrobiolojia.

Ivi kwa nini usifanyike utafiti wa nchi zoote kuangalia njia zilizotumika na matokeo waliyopata.

Mfano hapa bongo hata wangeangaliaga ufanisi wa mbinu.

Ilikuwa simple tu NIMRI wangepima antibodies za watu na kutuambia. Sasa nchi iko na kinga kwa asilimia XX, then kwa matokeo hayo chanjo haihitajiki (au inahitajika) kwa sababu tumefikia zaidi ya asilimia zinazopaswa kuwa zimechanjwa katika nchi.

Hili suala la eti Tanzania hatujawahi kugundua kitu chochote ni uzembe tu. Mbinu ya kudili na corona ya JPM ichunguzwe
 
Kwa sasa chanjo ya kovid 19,itatolewa sambamba na chanjo nyinginezo
 
Yaani, mbona ni masikitiko makubwa.

Utafiti ufanyike wachukue sampuli shaghalabaghala (hahahahaaa! Ndio randomly😆). Kama watu wengi wataonesha kureact kwamba walishaugua, sasa chanjo ya nini?

Maana ni ukweli usiopingika kwamba sie hatukujikinga ipasavyo, tuliendelea kuchapa kazi na japo mwendokasi hazikuzidisha, zilijaza magari na vituoni...... uwezekano ni mkubwa sana tushambukizwa.

Magonjwa ya virusi, ukishaugua ni chanjo tayari. Ni sayansi ipo.

Tunataka personalized (nationalozed in this case), informed, evidence based decision making in healthcare.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom