Kama Tanzania tukiwa kama.U.S.A. siasa itakuwa imekomaa

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,514
2,732
pamoja na kwamba mpinzani wa CLINTON, kutotendewa haki na kukili lakini bado anamuunga mkono kwa nguvu kubwa.
chanzo V.O.A.
Wademocrat wameanza mkutano wao
mkuu Jumatatu huko Philadelphia
wakitaka kuweka kando msimu wa
uchaguzi wa awali wa kuwania uteuzi
wa chama.
Baadhi ya sauti zenye nguvu
zikizungumzia kuungana pamoja na
mgombea wa urais Hillary Clinton.
Seneta wa Vermont, Bernie Sanders
ambaye alishika nafasi ya pili katika
kinyang’anyiro cha uteuzi wa chama
cha Democrat, alisema nchi inahitaji
uongozi ambao unawaleta watu pamoja
badala ya kuwatusi walatino, waislam,
wanawake, watu weusi na mashujaa wa
vita.
Wakati Donald Trump yupo na
harakati nyingi za kutusi kundi moja
baada ya jingine, Hillary Clinton
anafahamu kwamba mchanganyiko
wetu ni moja ya nguvu zetu imara,
alisema Sanders.
Alizungumzia kuhusu namna kampeni
yake ilivyoweza kushinikiza chama cha
Democrat kupitisha baadhi ya
mapendekezo yake ikiwemo Wall
Street, mageuzi katika fedha za
kampeni na kupinga mikataba ya
biashara kama Trans-Pacific
Partnership.
Sanders alielezea kutoridhishwa kwake
na namna utaratibu wa uteuzi
ulivyokuwa, lakini alisema Clinton
lazima awe rais ajaye wa marekani.
 
Back
Top Bottom