Kama Tanzania inataka kusaidia Congo, isifanye kwa siri

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,598
8,738
Tanzania tunachezewa na Rwanda na Uganda kwenye swala la Congo.

Rwanda na Uganda wamekuwa waliiba Diamond za Congo kwa muda mrefu sasa na ni wakati wa Tanzania kukaa chini na kabila na kufanya kama USA.

Tutawasaidia na lakini tutataka wafanyabiashara wa Tanzania waweze kufanya biashara Congo, Kampuni za madini zifungiliwe Tanzania na Congo iwekeze kwenye baadhi ya miradi kama reli na kutumia bandari ya Tanzania.

Sisi tutawapa ulinzi wa jeshi.
 
Nafikiri umetazama karibu sana.

Nafikiri hatuna sababu, haja na zaidi uwezo wa kuwasaidia hawa jamaa. Tanzania kujiingiza kwenye huu mgogoro ni hatari. Mgogoro wa kongo ni zaidi ya Rwanda na Uganda, tafuta docomentary ya Aljezeera ya "Who assacinated Kabila" utagundua hili.

Umasikini tulio nao kwa sehemu fulani ni madhara ya vita ya kagera.vita ni gharama/ghali sana tusijiingize kwenye vita. Usisahau kuna Malawi hatujui litaishaje.

Nafikiri serikali iwe neutral na ilinde mipaka yake, itusaidie kupata maji safi, umeme, huduma za afya, itujengee barabara zaidi nk.
 
Ya nini tupoteze muda mwingi na nguvu nyingi hivyo kwenda umbali wote huo kufuata kitu ambacho hata sisi tunacho na hatujanufaika kwa kuwepo kwake? Hapa si tutatengeneza dili jingine la watu kupeleka fedha Uswis?

Siungi mkono hii hoja.
 
umuachie mkeo mgeni uende ukapigane kwa ajili ya mke wa jirani yako? loh!
 
ukweli ni kwamba. Askari wetu wanapigana bega kwa bega na wenzao wa Congo. Waliondoka kama wiki mbili zilizopita na walipanda ndege tokea Znz.
 
Toa data acha uongo! Hamna mwanajeshi wa JWTZ anayeweza kwenda kupigana bila ruhusa ya amiri jeshi mkuu au bunge kuidhinisha. Vitani kuna kifo na si rahisi serikali kujibu lolote Kama haikuwataarifu wananchi!
 
ukweli ni kwamba. Askari wetu wanapigana bega kwa bega na wenzao wa Congo. Waliondoka kama wiki mbili zilizopita na walipanda ndege tokea Znz.
unataka kusema serikali imeweka siri kwa faida, ya nani.?
 
Kuna mipango inafanyika kuwapeleka wanajeshi wetu (kaka na dada zetu) kupigana (maana hakuna amani ya kulinda kule).

Je bunge limekaa lini na kuidhinisha huu mpango?

Waziri wa Ulinzi alitoa justifications zipi za sisi kwenda kwenye hii vita? je kama taifa tutafaidika na nini wanajeshi wetu kwenda kuuliwa kule?

Je tutatumia bilioni ngapi kupigana vita isiyo tuhusu?

Je wanajeshi wetu watatucost bilioni ngapi per day kupigana kule?

Pesa hizo kwa nini zisiimarishe ulinzi kwenye mpaka wetu na Congo?

Na kama bunge letu ambalo limejaa mbumbumbu ikipitisha huu mpango je timetable ya hawa vinaja wetu kukaa kule ikoje?





wafuatao hawajatoa tamko lolote lile:

IKULU
OFISI YA WAZIRI MKUU
WIZARA YA ULINZI
WIZARA YA NCHI ZA NJE
JWTZ
WAZIRI KIVULI WA UPINZANI KWA NIABA YA KAMBI YA UPINZANI


Hivi kweli hawa wanasiasa wanatutakia mema sisi?


At least 10 presidents from the Great Lakes region are expected to converge for an emergency meeting in Kampala this Saturday to discuss the ongoing hostilities in eastern DR Congo.

The fall of Goma, North Kivu’s commercial capital, to M23 rebels is said to have precipitated the weekend summit of the International Conference for Great Lakes region (ICGLR).

Despite presidents Museveni, Kagame and Kabila meeting on Tuesday night and yesterday, the ministers from ICGLR, who have separately been meeting in Kampala, resolved that there was need for all heads of state from the regional body to participate in the process.

They are also expected to address themselves to the United Nations Security Council for approval of the deployment of the proposed 4,000 neutral forces from Tanzania, Kenya, DR Congo and Angola. Tanzania has already pledged 500 soldiers for the mission and is likely to command the force.


10 presidents to meet in Kampala over DRC - National - monitor.co.ug
 
Back
Top Bottom