Mabibi na mabwana sisi ni taifa na kama taifa cheo ni dhamana tu.
Kiongozi yeyote kwa uongozi wake ni muhimu akazingatia ukweli kuwa kwa dhamana aliyo nayo si kuwa sasa eti ndiyo anayo fursa kamili ya kufanya au hata kusema lolote kwa kuwa tu eti dhamira yake itakuwa imemtuma huko.
Rais wetu kutaka kutuaminisha kuwa chanjo ya corona inaweza kuwa na walakini kwa kuwa tu imetengenezwa na anaowaita mabeberu ni jambo lisilokubalika.
Kwani ni chanjo ipi au dawa ipi ambayo haitengenezwi na mabeberu? Kama ana mashaka hayo kwanini hajawahi kusema lolote kwenye chanjo za polio, Pepo punda, ndui, nk?
Ieleweke kuwa kutofautiana kwa mawazo ni jambo la kheri wala si uhaini.
"Kama watoto mapacha hufikia hatua ya kutokuelewana. Sembuse mimi na wewe Neema?"
Sisi: mmoja mmoja na kwa jumuiya mbali mbali zikiwamo wana harakati, madhehebu za dini, wasomi, nk kwa roho safi ni muda sasa wa kumhitaji mheshimiwa huyu kubadili uelekeo.
Kwa hakika, kuunyamazia uelekeo huu ni kuyaweka maisha yetu wenyewe hatarini pasipo na uhalali wowote.
Ninawasilisha.