Kama taifa tunaweza kuishi na hili janga la kupata changamoto za kupumua?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,939
2,000
Nimekaa nakutafakari sana juu ya hii changamoto inayotukabili kama taifa. Maana mwaka jana mkuu wa nchi alitoa hofu wananchi kwa kutuambia tujiandae kuishi na huu ugonjwa kama magonjwa mengine. Na alitolea mfano Hiv kipindi inaingia nchini watu walikuwa na hofu hata kushika mikono wagonjwa, leo hii watu wanaishi na Hiv.

Swali ambalo tunatakiwa kujihoji. Je, HIV ipo sawa na Covid 19? Maana pamoja na kuwa miaka tisini watu walihofu lakini HIV ilikuwa inachukuwa muda mrefu kumaliza uhai wa mtu.

Sasa hii type mpya iliyokuja ya kuletea watu changamoto za kupumua, tutaweza kuishi nayo kama Hiv? Maana inakuletea matatizo ya kupumua na kama haukofit unaweza ukakata roho ndani ya nusu saa.

Mfano upo kijiweni unachapa kazi ghafla unapata changamoto ya kupumua, usafiri upo mbali utaweza kutoboa?

Ipo haja ya kuchukua tahadhali kama taifa kukabiliana ma hii changamoto. Maana hili janga sio la kukabiliwa na wananchi peke yao huku serikali ikijifanya haioni kama kuna tatizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom