Kama Taifa, tunashindwa vipi kuwa na salamu yetu kwenye mihadhara ya kitaifa tukaepuka hizi za kidini?

Umuofia kwenu!

Bila shaka hii ni salamu timilifu na isiyobagua, labda kwa asiyeelewa tu.

Basi, kama Taifa tunakwama wapi?

Kuanzia vyama vya siasa, na hata timu za michezo wana salamu zao. Ukisikia CCM hoyeee, Haki Sawaaa, Mbele Daimaa... unapata picha halisi uko sehemu gani!

Hatuna dini ya Taifa, ila kila Mtanzania anayo dini yake. Wala salamu hizi za kidini hazina ubaya, ni nzuri na tumezoea kuzitumia ila haiondoi ukweli kuwa si zetu.

Tatizo linakuja ni mambo ya imani, hivyo msemaji yampasa kutumia salamu kama zote ili tu kugusa makundi yote. Hili ni tatizo, ni kupoteza muda na kuwachosha waitikiaji.

Kwa uchache ni Asalaam aleykum, Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristo... hizi ndo maarufu sana.

Mara nyingi sana ni ukakasi kwa muislamu kutumia hizo salamu za kikristo, hasa kutaja Yesu hivyo wengi huishia asalaam aleykum tu na wana maelezo yao. watakwambia sio ya kidini bali ‘amani iwe nanyi’!

Wakristo mara nyingi sio watu wa kujali, hawana tatizo kutumia salamu zote. Nisieleweke vibaya sipo kwenye dini hapa, najenga hoja tu.

Yote hii ya nini, kutumia salamu nne tano kwa wakati mmoja na bado tu nina uhakika kuna makundi utayaacha!

Uhuru na Umoja ndiyo nembo yetu, pengine sio dili kwa sasa basi hata Amani na Upendo. Hii ni mifano tu, tulitunga nyimbo za Taifa itakuwa salamu!

Hebu tulione hili, tunaweza kupendekeza na mifano hapa. Mamlaka sikivu zikiona inafaa zitalifanyia kazi.

Wasalaam,

Ncha Kali.
Kama asalaam aleykum sio ya kidini kwanini wasiseme amani iwe kwenu badala ya kutumia kiarabu?
 
Salam yangu kubwa na yenye maana nzuri na inanipatia thawabu nyingi ni "ASSALAAM ALAYKUM" Hii ni spesho kwa waislamu tu,,kwa wakristo utanisamehe mkuu.


Kwa wakristo "Habari yako, habari za saa hizi" "Mambo" Shikamoo"

Kama kuna aliyemwelewa huyu naomba anistue!
 
Salam yangu kubwa na yenye maana nzuri na inanipatia thawabu nyingi ni "ASSALAAM ALAYKUM" Hii ni spesho kwa waislamu tu,,kwa wakristo utanisamehe mkuu.


Kwa wakristo "Habari yako, habari za saa hizi" "Mambo" Shikamoo"

Kwahiyo wewe guruguja ‘habari yako’ ni salamu ya Kikristo.?

Uamkie huu uzi umekuzidi mbali sana mlamu.
 
Mwanzoni mwa paragraph nilianza kuona unataka kuleta udini nikagundua baadae sio hasa ulipotafsiri Aslam aleikhum kuwa ni amani iwe juu yenu kwa mantiki hiyo sio salamu ya waslam bali ni kwa lugha ya kiarabu tu.Hata YESU alisemaga Amani iwe juu yenu.

Naona point yako ina mantiki mimi kuondoa kadhia hii napendekeza teseme UMOJA NA MSHIKAMO wanaojibu waseme NDIO NGUZO YETU hii iwe salamu ya kitaifa
kwanini tusiseme amani juu yenu na watu wajibu nawewe pia
 
Back
Top Bottom