Kama Taifa, tunashindwa vipi kuwa na salamu yetu kwenye mihadhara ya kitaifa tukaepuka hizi za kidini?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
534
500
Unaelewa mantiki ya kusalimiana..!? Kama ndiyo, unaelewa umuhimu wa salamu ipi itumike wapi..!? Na kama una mchanganyiko wa makundi ya watu, unaelewa maana ya kuwa na salamu moja inayogusa makundi yote..!?

NA BAADA YA HAYA, FIKIRIA KUHUSU VAZI LA TAIFA
Sasa unamfundisha mtunzi wa hotuba, mwanasiasa nguli mantiki ya kusalimiana.
Hivi lengo la kiongozi kwenda mahala na kuanza kuhutubia huwa ni kwaajili ya kwenda kuwasilimia watu wa mahala hapo?
Ile salamu haina lengo la kuwasalimia kama unavyo dhani ina maana tofauti kabisa. Salamu inavuta attention ya hadhira ili awe tayari kumsikiliza mhutubiaji. Na ndio maana kiongozi aliye makini anatumia hadi salamu za makabila anapokwenda sehemu ambako watu wa huko wamezoea sana salamu hiyo.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,843
2,000
Hii ndio homework niliyo mpa mtoa mada. "Afungue notes zake za kiswahili mada ya hotuba za viongozi, kipengere cha MUUNDO WA HOTUBA. KAZI ZA SALAMU KWENYE HOTUBA"
Hii siyo homework, bali wewe umeshindwa kujua kazi ya salamu kwenye hotuba au mahubiri, etc...

Hotuba inaweza isifuatiliwe kama hujasalimia ipasavy
Sasa unamfundisha mtunzi wa hotuba, mwanasiasa nguli mantiki ya kusalimiana.
Hivi lengo la kiongozi kwenda mahala na kuanza kuhutubia huwa ni kwaajili ya kwenda kuwasilimia watu wa mahala hapo?
Ile salamu haina lengo la kuwasalimia kama unavyo dhani ina maana tofauti kabisa. Salamu inavuta attention ya hadhira ili awe tayari kumsikiliza mhutubiaji
Usiniwekee dhana... hakuna mahala nimedhani kitu... KUDANGANYA PIA NI ALAMA YA ALIYEKOSA HOJA.. Hata kusingizia ni alama ya kukosa hoja
 

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
534
500
Hii siyo hoja... ungweka tu hoja mezani... ULICHOKIANDIKA NI DALILI YA MTU ALIYEISHIWA HOJA...

ALIYEISHIWA HOJA, HUJILINDA KWA
1. Kutukana
2. Kufoka
3. Kurudiarudia matusi au majibu hata pahala yadipohitajika
4. Kutaja vilivyo nje ya mada
5. Kujisifisifia
Hii ni dalili ya kuchoka kujadili mada za shule ya msingi
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,843
2,000
Mkuu salamu za kiongozi anaye hutubu hubadirika kutokana na mazingira aliyopo mbona walimu walisha fundisha. Hakuna salamu specific, kiongozi yeyote kabla hajahutubia lazima awajue watu wake anaokwenda kuwahutubia. Akisha wajua lazima awasalimie kwa Makundi, hiyo ni kanuni ya kuhutubia. Lengo ni kuvuta attention kwa wasikilizaji wake wote.
Shida ni kwamba hatuna salamu inayotaja makundi yote.. hata kama kuna kundi liba wachache... hizo zilizozoeleka hazigusi kila kundi... mengine yameachwa... NA NDO HOJA YA MTOA MADA
 

wakubeti

JF-Expert Member
Oct 5, 2018
560
1,000
Rudi shule ukasome kiswahili kwanza, alafu urudi tujadili kuhusiana na hilo swala lako la hizo salamu.
Huwa sipendi kujadili vitu vidogo ambavyo walimu walisha tufundisha tangia sekondari wewe unatuletea hapa.
Au kama una mtoto wa sekondari karibu hapo muulize nini maana ya kiongozi kusema Bwana Yesu Asifiwe, Asalama leko, Tumsifu Yesu Kristo, Tanzania Oyeeeeeeeeeeee, Ukimwi safiiiiiiiiii, Jinga la Chadema upoooooooooo.
Asalama aleko???
 

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
3,530
2,000
Lakini jambo unalolizungumzia huwezi kuliepuka kama kweli unajali hadhira yako. Labda hujapata fursa ya kusoma kozi kama 'public speaking' au katika muktadha wa madhehebu ya dini 'homiletics' - uwasilishaji wa ujumbe kwa hadhira ni jambo muhimu sana.

Unaweza kuona kama kitu fulani ni kupoteza muda, lakini ni muhimu sana. Mfano, kama umetembelea nchi mbalimbali, hakuna kitu muhimu kama kumsalimia mtu kwa lugha yake au kulingana na mila na utamaduni wake. Of course, kuna aina ya viongozi na viongozi.

Kuna wasiojali imani ya dini ya wananchi wake na kuna wanaojali na wote wanaojali wanajua wanachokifanya na hasa kama hata wao ni waumini wa dini.

Unaweza kusema 'huwezi kumridhisha kila mtu', ndiyo. Lakini walau ujitahidi kufanya kitu hata kama ni kidogo kuliko kushindwa kufanya hivyo kabisa.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,099
2,000
Naunga juhudi mkono, kuwepo na salam moja ya kitaifa ili kuondoa sintofahan maana kuna wapagani wao hawasalimiwi. Mfano jana nilimsikia kiongozi mmoja wa Siri-kali anatoa salama ya upande mmoja tu nikawaza sana na akaendelea kwa kusema sisi (akataja dini yake) tunasema .........

Nukajiuliz sana ikabidi ninywe maji.

Barabara kabisa mkuu, na hicho ndo hasa kilinipa kuwaza hili jambo.... wazo langu limeanzia hapo.
 

Gidbang

JF-Expert Member
Jun 1, 2014
3,766
2,000
Mwanzoni mwa paragraph nilianza kuona unataka kuleta udini nikagundua baadae sio hasa ulipotafsiri Aslam aleikhum kuwa ni amani iwe juu yenu kwa mantiki hiyo sio salamu ya waslam bali ni kwa lugha ya kiarabu tu.Hata YESU alisemaga Amani iwe juu yenu.
Naona point yako ina mantiki mimi kuondoa kadhia hii napendekeza teseme UMOJA NA MSHIKAMO wanaojibu waseme NDIO NGUZO YETU hii iwe salamu ya kitaifa
Nisaidie kwenye hii salamu ya kitaifa anayesalimiwa ni nani kama ni wananchi basi swala la imani yao huwezi likwepa labda tufute kabisa hizi dini za wazungu na waarabu. Kila kabila lina salamau zake. Kwa kabila langu tunasalimia kwa kiongozi kusema tushikilie yaliyo mema sisi tunaitikia ndiyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom