Kama Taifa, tunashindwa vipi kuwa na salamu yetu kwenye mihadhara ya kitaifa tukaepuka hizi za kidini?

Pamoja na majivuno yako ila hata kuandika tu hujui, kwako wewe wasiosoma huko unaita sekondari hawafai kuheshimiwa na kuelekezwa nawe mwerevu... elimu yako iwanufaishe wengine pia.

Ukileta ukada hapa nitachagua kukupuuza tu.
Bora nipuuzwe tu na mleta maada za kitoto kama wewe, maana nitaambukizwa upumbavu bureee. Badala ya kuwaza mambo kukuza uchumi unatuletea utumbo kama huu. Sisi sio watoto wadogo bhana, hiyo maada kajidili na watoto wenzako huko
 
kwa hivyo basi mambo ya Dini huku ilikuwa ni swala la mtu binafsi na ukionekana unafanya hayo mambo ilikuwa unaweza kupata matatizo

Hapa ndipo tunapotofautiana hata na wao waliotuletea hizo dini (i.e western people), Unakuta mtu sijui ndio mtumishi au ostadh mpo sehemu ya public atataka awabugudhi watu wengine aidha kwa mazungumzo ya kidini au mambo mengine yanayofanana na hayo pasipo kuelewa sio wote wenye misimamo hiyo ya kidini au hata kuamini katika hizo dini,

wenzetu swala la imani ni swala binafsi ambalo muhusika anatakiwa abaki nalo yeye kama yeye, na ofcourse zipo sehemu husika kwa shughuli za kidini.

Nachukia sana kumpambanua mtu kwa sifa ya kidini, i completely hate that shit, utamsikia mtu "yule dada muislamu" au "yule kaka msabato/mlokole" hii kitu huwa inanikata moto sanaa.😤
Nashukuru Mungu nakiishi hiki ninachokiongea, kuna watu nimekaa nao over 3 years hawajui hata dini yangu zaidi ya kuishia kuguess tu.




Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Una point nzuri sana; hisi salamu za kidini zina ubaguzi fulani kwa sababu zinachukulia kuwa nchi ina dini mbili au tatu tu; uislamu, ulokole (waina zote za kikiristo) na ukatoliki tu. Unabagua dini ambazo hazijipangi katika makundi hayo. Zamani sana enzi za chama kimoja, salamu ilikuwa ni "Uhuru! ---Uhuru!", baadaye ikabadilika kuwa "Uhuru!---Kazi ya TANU!!

Ni kweli tunahitaji salamu ya kitaifa isiyokuwa na elements za kidini au za kisiasa. Tuanze tu kuwa tunasema "Tanzania juu!---Juu" na kuishia na "Mungu Ibariki Tanzania"
Shida tuliyonayo ni kuwa, kila salamu itakayotungwa, baada ya muda fulani kupita, hatukawii kuihusisha na dini fulani... MFANO NI YALE MANENO YANAYOTAMKWA BUNGENI NA SPIKA KABLA YA KUANZA BUNGE... yalikuwa maarufu sana enzi za Msekwa
 
Hapa ndipo tunapotofautiana hata na wao waliotuletea hizo dini (i.e western people), Unakuta mtu sijui ndio mtumishi au ostadh mpo sehemu ya public atataka awabugudhi watu wengine aidha kwa mazungumzo ya kidini au mambo mengine yanayofanana na hayo pasipo kuelewa sio wote wenye misimamo hiyo ya kidini au hata kuamini katika hizo dini,

wenzetu swala la imani ni swala binafsi ambalo muhusika anatakiwa abaki nalo yeye kama yeye, na ofcourse zipo sehemu husika kwa shughuli za kidini.

Nachukia sana kumpambanua mtu kwa sifa ya kidini, i completely hate that shit, utamsikia mtu "yule dada muislamu" au "yule kaka msabato/mlokole" hii kitu huwa inanikata moto sanaa.
Nashukuru Mungu nakiishi hiki ninachokiongea, kuna watu nimekaa nao over 3 years hawajui hata dini yangu zaidi ya kuishia kuguess tu.




Let's meet at the top, cheers 🥂
Mkuu salamu za kiongozi anaye hutubu hubadirika kutokana na mazingira aliyopo mbona walimu walisha fundisha. Hakuna salamu specific, kiongozi yeyote kabla hajahutubia lazima awajue watu wake anaokwenda kuwahutubia. Akisha wajua lazima awasalimie kwa Makundi, hiyo ni kanuni ya kuhutubia. Lengo ni kuvuta attention kwa wasikilizaji wake wote.
 
Rudi shule ukasome kiswahili kwanza, alafu urudi tujadili kuhusiana na hilo swala lako la hizo salamu.
Huwa sipendi kujadili vitu vidogo ambavyo walimu walisha tufundisha tangia sekondari wewe unatuletea hapa.
Au kama una mtoto wa sekondari karibu hapo muulize nini maana ya kiongozi kusema Bwana Yesu Asifiwe, Asalama leko, Tumsifu Yesu Kristo, Tanzania Oyeeeeeeeeeeee, Ukimwi safiiiiiiiiii, Jinga la Chadema upoooooooooo.
Hujatumia busara kuandika majibu haya.... KAMA UNAZO LAKINI...!!
 
Naunga juhudi mkono, kuwepo na salam moja ya kitaifa ili kuondoa sintofahan maana kuna wapagani wao hawasalimiwi. Mfano jana nilimsikia kiongozi mmoja wa Siri-kali anatoa salama ya upande mmoja tu nikawaza sana na akaendelea kwa kusema sisi (akataja dini yake) tunasema .........

Nukajiuliz sana ikabidi ninywe maji.
 
Na hizi zilizopo zinasaidia nini..!? Kwanini mtu asiende moja kwa moja kwenye jambo lililompeleka hapo sehemu husika.!? AU NINI MAANA YA SALAMU..!?
Hii ndio homework niliyo mpa mtoa mada. "Afungue notes zake za kiswahili mada ya hotuba za viongozi, kipengere cha MUUNDO WA HOTUBA. KAZI ZA SALAMU KWENYE HOTUBA"
 
Mkuu salamu za kiongozi anaye hutubu hubadirika kutokana na mazingira aliyopo mbona walimu walisha fundisha. Hakuna salamu specific, kiongozi yeyote kabla hajahutubia lazima awajue watu wake anaokwenda kuwahutubia. Akisha wajua lazima awasalimie kwa Makundi, hiyo ni kanuni ya kuhutubia. Lengo ni kuvuta attention kwa wasikilizaji wake wote.

Ahsante kwa mchango wako mkuu, ila specifically mchango wangu hapo juu ulikuwa ni kukazia baadhi ya maelezo ya mkuu Lucas Mobutu pale aliposema "Dini huku ilikuwa ni swala la mtu binafsi na ukionekana unafanya hayo mambo ilikuwa unaweza kupata matatizo" ambayo niliyaquote kabisa.

Ahsante!


Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Umuofia kwenu!

Bila shaka hii ni salamu timilifu na isiyobagua, labda kwa asiyeelewa tu.

Basi, kama Taifa tunakwama wapi?

Kuanzia vyama vya siasa, na hata timu za michezo wana salamu zao. Ukisikia CCM hoyeee, Haki Sawaaa, Mbele Daimaa... unapata picha halisi uko sehemu gani!

Hatuna dini ya Taifa, ila kila mtanzania anayo dini yake. Wala salamu hizi za kidini hazina ubaya, ni nzuri na tumezoea kuzitumia ila haiondoi ukweli kuwa si zetu.

Tatizo linakuja ni mambo ya imani, hivyo msemaji yampasa kutumia salamu kama zote ili tu kugusa makundi yote. Hili ni tatizo, ni kupoteza muda na kuwachosha waitikiaji.

Kwa uchache ni Asalaam aleykum, Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristo.... hizi ndo maarufu sana.

Mara nyingi sana ni ukakasi kwa muislamu kutumia hizo salamu za kikristo, hasa kutaja Yesu hivyo wengi huishia asalaam aleykum tu na wana maelezo yao.... watakwambia sio ya kidini bali ‘amani iwe nanyi’!

Wakristo mara nyingi sio watu wa kujali, hawana tatizo kutumia salamu zote. Nisieleweke vibaya sipo kwenye dini hapa, najenga hoja tu.

Yote hii ya nini, kutumia salamu nne tano kwa wakati mmoja na bado tu nina uhakika kuna makundi utayaacha!

Uhuru na Umoja ndiyo nembo yetu, pengine sio dili kwa sasa basi hata Amani na Upendo. Hii ni mifano tu, tulitunga nyimbo za Taifa itakuwa salamu!

Hebu tulione hili, tunaweza kupendekeza na mifano hapa. Mamlaka sikivu zikiona inafaa zitalifanyia kazi.

Wasalaam,

Ncha Kali.
Wazo zuri
 
Back
Top Bottom