Kama Taifa tujitafakari, ni haki neno "dot.tz" ikulaze rumande?

Mdogo wangu nilikuacha la tano b miaka ile sikujua kuna wakati ungekuja kujulikani hivi ila mola atakutoa mkuu tupo nyuma yako nilikuwa nje mda mrefu nimeingia jana naambiwa wewe ni mharifu napata shida kidogo

Huyu jamaa anapakaziwa uhalifu,wahalifu wenyewe kama wauza pembe za ndovu tumeshuhudia wakipatiwa dhamana,ila huyu hatakiwi kupatiwa dhamana,inasikitisha sana hii nchi aisee
 
Na wanataka dot tz ili waweze kuzima kwa sababu ikiwa dot com hawawezi kuzima. Hali ni mbaya kwa kweli tuendako!
 
Serikali ya CCM Wanatulazimisha turudi nyuma ki-teknolojia ili wadukue mawasiliano yetu kirahisi.

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
 
Siyo kukulaza rumande tu, Afungwe kabisa huyu mjinga ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kuvunja sheria kwa makusudi.
 
Wakitaka kukubambikia kesi Mkuu hata ikiwa dot tz watatafuta lingine la kukubambikizia ili watimize mradi wao wa kishetani tena bila hata aibu wala woga.
Simba alishuka toka mlimani akakuta mwanambuzi anakunywa maji pale bondeni.Mazungumzo yakawa hivi
Simba;wewe mwanambuzi mbona unanichafulia maji?ndio maana nakunywa maji machsafu!
Mwanambuzi;Hapana mbona mimi niko bondeni wewe ndiye ulikuwa mliamani yanakotoka maji!
Simba; mwaka juzi ulinitukana nakumbuka sana
Mwanambuzi;aka! Mbona mimi nina umri wa miezi mitatu tu!sijakutukana
Simba;basi kama sio wewe ni mama yako na lazima uliwe!
 
Udikteta uchwara hauna nafasi katika nchi yoyote ile yenye vyama vingi. Kulewa madaraka na kujiona wewe ni Mungu mtu na kufanya vile utakavyo bila kuheshimu katiba na utawala wa sheria ni kosa kubwa sana katika nchi yoyote ile ambayo baadhi ya wananchi wake hawako tayari kuwa na mtawala kama huyo.

Kama hakuamua kubadilika ili kuongoza nchi katika misingi ya sheria, kuheshimu katiba ya nchi, kuheshimu uhuru wa habari na freedom of expression basi ataendelea kujuta sana kwanini alichukua form ya kugombea Urais. Watanzania wa 2016 si sawa na wale wa mwaka 47. Hatuwezi kuendelea kuona gari linaendeshwa kama gari bovu halina sukani.

Simba alishuka toka mlimani akakuta mwanambuzi anakunywa maji pale m
Simba alishuka toka mlimani akakuta mwanambuzi anakunywa maji pale bondeni.Mazungumzo yakawa hivi
Simba;wewe mwanambuzi mbona unanichafulia maji?ndio maana nakunywa maji machsafu!
Mwanambuzi;Hapana mbona mimi niko bondeni wewe ndiye ulikuwa mliamani yanakotoka maji!
Simba; mwaka juzi ulinitukana nakumbuka sana
Mwanambuzi;aka! Mbona mimi nina umri wa miezi mitatu tu!sijakutukana
Simba;basi kama sio wewe ni mama yako na lazima uliwe!
 
Mimi naona ni kichekesho na ni "kamchezo"

Kwa nini mkuu qa mahakama ya kisutu alizitawanya kesi kwa mahakimu tofauti japo hazina utofauti?

Kama kajidhamini mahakamani hapo kwa kesi mbili zinazofanana,kwa nini dhamana hiyo,kwa busara ikaenda kwenye kesi ya tatu?

Kwa nini kwenye dhamana wanageukana lakini tarehe ya kesi walikubaliana ikawa tarehe moja? Je kwa kuwa tarehe ya kesi ni moja,kwa kesi zote tatu,je angeruka dhamana kwenye kesi moja wakati angekuja kwenye zile mbili?

Nadhani sasa jaji mkuu atolee tamko huu mwenendo unaokanganya katika mahakama zetu

Yaani kesi ya dot tz ambayo hata kutoandikwa kwake hajuamdhuru mtu nalo linalaza mtu rumande? Ni hatari kwa usalama wa nchi? Ni mauaji?

Kuna yule mwanajeshi mstaafu alisema kadi yake ya uanachama wa chama cha siasa ilikuwa imetunzwa, nina wasiwasi hata ya huyo unayetaka atoe tamko ya kwake bado itakuwa imetunzwa pia.
 
Siyo kukulaza rumande tu, Afungwe kabisa huyu mjinga ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kuvunja sheria kwa makusudi.
unauhakika ww uko salama? tukichukua post zako tangu 2014 zikafanyiwa kazi utabaki salama?
 
Back
Top Bottom