Kama Taifa tujitafakari, ni haki neno "dot.tz" ikulaze rumande?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Mimi naona ni kichekesho na ni "kamchezo"

Kwa nini mkuu qa mahakama ya kisutu alizitawanya kesi kwa mahakimu tofauti japo hazina utofauti?

Kama kajidhamini mahakamani hapo kwa kesi mbili zinazofanana,kwa nini dhamana hiyo,kwa busara ikaenda kwenye kesi ya tatu?

Kwa nini kwenye dhamana wanageukana lakini tarehe ya kesi walikubaliana ikawa tarehe moja? Je kwa kuwa tarehe ya kesi ni moja,kwa kesi zote tatu,je angeruka dhamana kwenye kesi moja wakati angekuja kwenye zile mbili?

Nadhani sasa jaji mkuu atolee tamko huu mwenendo unaokanganya katika mahakama zetu

Yaani kesi ya dot tz ambayo hata kutoandikwa kwake hajuamdhuru mtu nalo linalaza mtu rumande? Ni hatari kwa usalama wa nchi? Ni mauaji?
 
dendaboy

JF-Expert Member
Sep 15, 2016
884
1,000

ni mambo yamepangwa lazima yawe kama yalivyopangwa
 
Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
2,000
Kuna roho chafu inayotawala awamu hii inayowafanya wenye madaraka au kwa jina jingine "watoa maelekezo kutoka juu" waweke pembeni sheria za nchi na katiba halafu waamue kufanya mambo wanavyotaka wao.
This primitive tendency will backfire with time.
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,494
2,000
Daaaaaaaaah,kwa hiyo mshkaji Mexence bado anashikiliwaa,daaaaaah,something is very wrong in current leadership style,vyombo vya kutenda haki vinakandamiza haki
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,877
2,000
CCM inafanya siasa za kishamba sana !
Bora hata za kishamba, hizi ni za kishetani kabisa. Mtu aliyeanzisha na kuuendeleza mtandao ambao umeisaidia sana nchi hii katika kufichua mambo mengi mabaya kwa faida ya nchi hivi kweli badala ya kuwa shujaa anafanyiwa ukatili wa aina hii kama vile ni mhaini?
Mangapi ambayo yamefichuliwa hapa JF yameiokoa nchi na hasara kubwa? Elimu kiasi gani watu wamepeana humu na imetumika kusaidia nchi? Wangapi wameutumia mtandao huu kuipigia kampeni serikali iliyoko madarakani hadi kufanikiwa kuingia madarakani? Ni mengi ya kutaja.
Waziri wa habari Nape mwenyewe ni member humu tena verified, waziri wa mambo ya ndani Mwigulu, Mazingira Makamba, Waziri Kigwangwala wote hao ni verified na wameutumia mtandao huu kujijenga kisiasa lakini malipo kwa Founder wake ni hayo ya kishetani hadi njama kwenye dhamana. Kweli ni watu hao?
Hata wale wapenzi wa CCM walio waungwana kwa kweli wamechukizwa na kushangazwa na mwenendo huu wa serikali yao dhidi ya watu walio wema. Wenye akili watajua kuwa kuna siku nao wawatafunwa na shetani hilo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom