Kama taifa ni muda wa kuangalia vipaumbele vyetu, policies za emergencies preparedness na uthamini wa maisha ya binadamu

Planet FSD

JF-Expert Member
Oct 24, 2019
455
938
Wakuu, najua ni mapema sana kuanza kulizungumzia hili jambo kufuatia ajali ya leo ya ndege huko Bukoba bila kuwa na majibu kamili lakini ni wazi kama taifa kuna mahali tunakosea na tunahitaji kujitathmini upya.

Katika swala zima la uokozi muda wa majanga watanzania tumefeli na tunaendelea kufeli. Hatuthamini kabisa maisha ya binadamu. Tunawekeza hela kwenye vitu vingine ila tunaacha mambo ya wokozi kama vile ni jambo lisilo na maana.

Kwa ajali ya leo nilitegemea kuona hata boats kadhaa na divers wakifika pale kwenye tukio na kuanza kuwatoa majeruhi kabla ya kuanza kufikiria kuivuta ndege.

Unapotumia masaa zaidi ya 8 kuvuta ndege ndo uje kuwatoa waliomo huo sio wokozi, hapo unatafuta maiti tu. Binadamu hawezi kuhimili kuwa hai muda wote huo ndani ya maji bila hewa.

Nadhani leo tutakuwa tumetia fora duniani huko na tutaongelewa vya kutosha. Kuvuta ndege kwa kamba kwa kutumia mitumbwi au mikono ya binadamu ni jambo la kustaajibisha sana na linatupa jibu moja tu, hatujajiandaa na majanga.

Hii inabidi iwe wake up call kwa serikali yetu. Ni muda sasa wa kuweka vifaa vya uokoaji kwenye maeneo kama haya ya viwanja vya ndege, ziwani na baharini.
 
This country sucks!!! It hurts kuona watu wanakufa kwa kuwa tu hatujiandai kwa majanga na dharura
 
Back
Top Bottom