Kama Taifa hatutakuwa na Sera moja ya maendeleo basi maendeleo tutayaona kwa wenzetu

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Tanzania tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi. Hili ni jambo jema ili kushirikisha watu wote katika maendeleo yetu. Lakini hatuwezi kupata maendeleo kama kila chama au kiongozi kuwa na sera yake ya maendeleo.

Mfano CCM imekuwa chama tawala tangu tupate uhuru lakini kila awamu imekuwa na sera yake na pia kila kiongozi amekuwa na sera yake mbali na sera ya chama. Hii ni changamoto kubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo au kuendeleza nchi.

Katika awamu ya tatu CCM ilikuwa na sera yake lakini pia Rais Mkapa alikuwa na sera yake. Hivyo kwa miaka 10 ya utawala wa Rais Mkapa serikali ilikuwa inatekeleza sera ya CCM na ahadi za Mkapa wakati wa kampeni. Awamu ya nne ya Rais Kikwete hali ilikuwa hiyo hiyo. Katika awamu hiyo kwa mfano tuliaminishwa tutatumia umeme wa gesi, lakini ilivyokuja awamu ya tano ya Rais Magufuli alitupilia mbali umeme wa gesi na badala yake akaja na umeme wa maji wa bwawa la Nyerere. Awamu ya sita ya Rais Samia iko njia panda haijui ifuate umeme wa maji au wa gesi.

Sasa utaratibu huu hauwezi kutuletea maendeleo badala yake tutakuwa tunakwenda mbele na kurudi nyuma. Hivyo mabadiliko yanahitajika kama kweli tunataka kusonga mbele kimaendeleo. Tunatakiwa kuwa na sera moja ya maendeleo ya Taifa. Sera ambayo itafuatwa na vyama vyote vya siasa na viongozi wote tutakaowapata. Vyama vya siasa na viongozi washindane katika kutengeneza mikakati ya utekelezaji (Strategies). Siyo kila chama kiwe na sera yake na viongozi wawe na ahadi zao tofauti na sera ya Taifa. Sisi wananchi tutakuwa na kazi nyepesi ya kuangalia, kupima na kuchagua mkakati upi ni bora na inatekelezeka kirahisi katika mazingira yetu. Pia wananchi tutakuwa na kazi ya kuchagua ni kiongozi yupi anauwezo mkubwa zaidi wa kutekeleza mkakati wa chama chake.

Nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kutuletea maendeleo vinginevyo tutasota kwa muda mrefu kama Taifa.
 
Ndio maana mkuu piga kelele tupate katiba mpya kwa ajili yetu sisi sio watawala, katiba mpya itatupatia taasisi imara na zenye kujitegemea, katiba mpya itatupatia CEOs wote watakaojitegemea yaani IGP, CDF,DPP, etc etc maana hawa watapatikana thr Bunge means kuwatoa au kuwasimamisha ni lazima bunge lihusishwe, our no 1s watakuja na kuondoka bila kuathiri Sera zetu
 
Suluhisho hili hapa.

Hili andiko limesimama na ni mujarabu walitumie wasione aibu
 
Nchi ambayo inatumia kipato chake kwa 75% kwa ajili ya kulipa mishahara, inategemea kutakua na Maendeleo gani?
 
Tanzania tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi. Hili ni jambo jema ili kushirikisha watu wote katika maendeleo yetu. Lakini hatuwezi kupata maendeleo kama kila chama au kiongozi kuwa na sera yake ya maendeleo...
Nina mashaka sana kama unajua hata maana ya sera kutokana na haya maelezi yako
Mfano rahisi wa sera ni: kuwapatia wananchi umeme wa gharama nafuu.

Hii ni sera ila njia za kuitekeleza hazitafanana Kati ya kiongozi mmoja na mwingine na Kati ya chama kimoja na kingine. Ndio maana tuna uchaguzi ili kuwaadhibu wale ambao mipango yao imeshindwa kutekeleza sera ya kutupatia umeme wa uhakika na gharama nafuu
 
Sidhani kama umesoma sera ya Taifa ya nishati! Kuhusu kuelewa maana ya neno sera nakuachia wewe ujielimishe. Lakini lengo langu ni kuwa tuwe na sera moja ya Taifa ambayo itatekelezwa na ye yote atakayekuwa madarakani. Sasa kama ni umeme wa gharama nafuu au ghali itategemea na aina ya vyanzo vya nishati vilivyopo na uwezo wa kuviendeleza.
 
FB_IMG_16464816685050176.jpg
 
Tanzania tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi. Hili ni jambo jema ili kushirikisha watu wote katika maendeleo yetu. Lakini hatuwezi kupata maendeleo kama kila chama au kiongozi kuwa na sera yake ya maendeleo.

Mfano CCM imekuwa chama tawala tangu tupate uhuru lakini kila awamu imekuwa na sera yake na pia kila kiongozi amekuwa na sera yake mbali na sera ya chama. Hii ni changamoto kubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo au kuendeleza nchi.

Katika awamu ya tatu CCM ilikuwa na sera yake lakini pia Rais Mkapa alikuwa na sera yake. Hivyo kwa miaka 10 ya utawala wa Rais Mkapa serikali ilikuwa inatekeleza sera ya CCM na ahadi za Mkapa wakati wa kampeni. Awamu ya nne ya Rais Kikwete hali ilikuwa hiyo hiyo. Katika awamu hiyo kwa mfano tuliaminishwa tutatumia umeme wa gesi, lakini ilivyokuja awamu ya tano ya Rais Magufuli alitupilia mbali umeme wa gesi na badala yake akaja na umeme wa maji wa bwawa la Nyerere. Awamu ya sita ya Rais Samia iko njia panda haijui ifuate umeme wa maji au wa gesi.

Sasa utaratibu huu hauwezi kutuletea maendeleo badala yake tutakuwa tunakwenda mbele na kurudi nyuma. Hivyo mabadiliko yanahitajika kama kweli tunataka kusonga mbele kimaendeleo. Tunatakiwa kuwa na sera moja ya maendeleo ya Taifa. Sera ambayo itafuatwa na vyama vyote vya siasa na viongozi wote tutakaowapata. Vyama vya siasa na viongozi washindane katika kutengeneza mikakati ya utekelezaji (Strategies). Siyo kila chama kiwe na sera yake na viongozi wawe na ahadi zao tofauti na sera ya Taifa. Sisi wananchi tutakuwa na kazi nyepesi ya kuangalia, kupima na kuchagua mkakati upi ni bora na inatekelezeka kirahisi katika mazingira yetu. Pia wananchi tutakuwa na kazi ya kuchagua ni kiongozi yupi anauwezo mkubwa zaidi wa kutekeleza mkakati wa chama chake.

Nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kutuletea maendeleo vinginevyo tutasota kwa muda mrefu kama Taifa.
Kila raisi ana kuja na style yake ya kuendasha nchi, kutoka chama hicho hicho kimoja. Nadio maana mpaka Leo tunashule shikizi
 
Ndio maana mkuu piga kelele tupate katiba mpya kwa ajili yetu sisi sio watawala, katiba mpya itatupatia taasisi imara na zenye kujitegemea, katiba mpya itatupatia CEOs wote watakaojitegemea yaani IGP, CDF,DPP, etc etc maana hawa watapatikana thr Bunge means kuwatoa au kuwasimamisha ni lazima bunge lihusishwe, our no 1s watakuja na kuondoka bila kuathiri Sera zetu
Katiba mpya ni muhimu kupunguza ukiritimba wa madaraka kwa mtu mmoja; Rais!
 
Back
Top Bottom