Kama Taifa hatujui tulipo wala tunapoelekea

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Habari wanajamvi!
Naam hakika unaweza kusema pasipo mashaka yoyote kwamba sasa kama Taifa ujinga wetu umefikia full tank.

Tumekuwa hatujui wapitulipo na wapi tunaelekea. Walau wachache wanajua tulipo toka. Tunabishana hata mambo ya msingi kabisa kwasababu za kisiasa tuna acha Taifa likiangamia na kufedheheka. Kisa wanasiasa na siasa. Ujinga ulioje?

Tazama,thamani ya Shilling imeshuka kwa kiwango kikibwa sana kuliko wakati wowote tangu tupate Uhuru. Kwasasa Dollar moja ya Marekani ni sawa na shilling 2548 za Tanzania. Au Shilling moja ya Kenya ni Shilling 28 za Tanzania. Badala ya kukaa chini tutafakari nini kimesababisha jambo hili kutokea?

Tunakuja na sababu za kisiasa eti tunahujumiwa!! Kwanini wasomi waseme hivi? Wanajua ili wabaki salama ni bora waseme hivyo kuliko kuusema ukweli mchungu. Ukweli una tabia moja huwa haumpambi mtu. Hapo ndipo walipo ogopa kusema ukweli kwasababu watawakwaza wanasiasa. Bora Taifa liangamie kuliko kuonesha kuwa wana siasa wamekosea hapa au pale. Kizazi cha wanafikh!

Je, Shilling itaendelea kuporomoka? Hakika itaendelea kuporomoka zaidi na zaidi. Yafaa tuchukue hatua muafaka sasa tena bila kuchelewa. Hatua gani tuchukue? Ni lazima tuchukue hatua zifuatazo:-

Kwanza, lazima tujenge mazingira ya kuaminika Kati yetu na wenye mitaji. Tabia ya kubadili gia angani kuhusu mazingira ya uwekezaji imewafanya wawekezaji wengi kuwa na mashaka na mitaji yao.

Pili, Biashara ya utalii imevurugwa sana siku za karibuni kwa kuweka kodi mbalimbali kuwa juu kuliko Nchi jirani. Purukushani anazo fanya Kigwangala zitazidi kuporomosha mapato. Kwenye tatizo ni bora kutumia diplomasia kuliko ubabe wa madaraka.

Biashara ya dhahabu na makinikia ni lazima tukubali baadhi ya mambo yaende kama wawekezaji walivyoingia mikataba hapo awali. Kunyanyasa wawekezaji wenye mitaji mikubwa ni kujichimbia kaburi kiuchumi. Ni lazima tuheshimu Mikataba iliyoingiwa .
Tuongeze uzalishaji wa bidhaa na huduma za kuuza Nchi za Nje.

Nini tutegemee? Bidhaa zote tutakazo agiza sasa zitapanda bei mara dufu. Maisha baada ya Desemba,2017 yatakuwa ni shida. Bidhaa zote zitapanda bei. Twafa twafa!
 
Asubuhi asubuhi ushavurugwa ...siasa weka pembeni tafuta kitu ufanye kwa ajiri ya heshima yako na kesho yako haitakuja kusema eti mambo yako yaligoma kisa shilingi ilishuka. This is life mkuu
 
Asubuhi asubuhi ushavurugwa ...siasa weka pembeni tafuta kitu ufanye kwa ajiri ya heshima yako na kesho yako haitakuja kusema eti mambo yako yaligoma kisa shilingi ilishuka. This is life mkuu
Ndio hapo ninapo ona ujinga umejikita chini kuliko kawaida. Uchumi ukiporomoka zaidi itafika mahali hata kuagiza viberiti hatuta weza. Mtabaki kusifia wanasiasa eti ni jembe. Hapa tulipo fikia kuna jambo hata wajinga watajifunza. Let us wait and see.
 
Moja ya matatizo makubwa tuliyonayo watanzania na yanayotugalimu ni kukosa elimu inayoitwa 'exposure'. Watu wengi hawajui dunia inaendaje. Na kutokujua kwetu kiingereza ndo kabisaaa kunasababisha watanzania tusifuatilie mambo yanaendaje kwingineko.
 
Tumia akiliyako, usishikiwe akili nenda na uangalie Leo shilingi inabadilishwa kwa kiasigani cha dola.
Yaani mnazusha mambo ya ajabu alafu mnaleta humu jamiiforum tuyajadili.

Nenda Leo kwenye maduka yafedha popote uone kama kunaduka linabadili dola 1 ya marekani kwa shilingi 2500 ya Tanzania. Meanzisha viwanda vya uongo bila aibu.
 
NASKIA BOMBADIA ZETU ZIMECHELEWA ZINAFANYIWA VIPIMO ZINAKUJA MWAKANI
 
Tumia akiliyako, usishikiwe akili nenda na uangalie Leo shilingi inabadilishwa kwa kiasigani cha dola.
Yaani mnazusha mambo ya ajabu alafu mnaleta humu jamiiforum tuyajadili.

Nenda Leo kwenye maduka yafedha popote uone kama kunaduka linabadili dola 1 ya marekani kwa shilingi 2500 ya Tanzania. Meanzisha viwanda vya uongo bila aibu.
Wewe ndo wale wale waliokosa exposure! Hebu nenda London kabadilishe hela ije kwenye madafu ndo utajua!
 
Ulikuwa na wazo,,ila umekosa hoja kwa sababu umeandika kwa hisia kuliko uhalisia!
 
na bado itafika Tshs 3000 muda si mrefu wacha tutiane ujinga na wanasiasa
Mawazo Yangu Yote Nilikuwa Najua Imeshafika Kumbe Ndio 2500

Daaaaaahhh Alafu Wale Jamaa Wa Takwimu Wanasema Zito Anaongopa......!!!!!

Maisha Ya Kibongo Bhana
 
Back
Top Bottom