Kama tabia za Wapinzani ni hizi, bora tusione kabisa Bunge

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Badala ya kujadili ukosefu wa maji kwenye Majimbo Yao wanataka kuuza sura runingani!!! Bora tusione kabisa hili Bunge.

Waziri Nape katoa Maelezo ya Serikali juu ya sababu za kutorusha live. Bado hamuelewi tu?

Kutumia bilioni 4 kutangaza sura za wabunge wakati watoto wanakaa chini na Akina mama wanajifungulia sakafuni, ni busara kweli?
 
Naona pro ccm wanajitahidi sana bunge lisionzeshwe hiz sio zama za ujima jamaa tunajidai eti democracz ya habari imekuwa huku mkiwanzima wananchi kupata uhuru wa kusikilya kianacho endelea kweli tz kila kitu kinawezekana.
 
Badala ya kujadili ukosefu wa maji kwenye Majimbo Yao wanataka kuuza sura runingani!!! Bora tusione kabisa hili Bunge. Waziri Nape katoa Maelezo ya Serikali juu ya sababu za kutorusha live. Bado hamuelewi tu???kutumia bilioni 4 kutangaza sura za wabunge wakati watoto wanakaa chini na Akina mama wanajifungulia sakafuni ni busara kweli????????????????
wewe msukule unashibishwa pumba hapo lumumba, wakati wote hawakuwaona hao watoto na akina mama!
 
Umeandika kiushabiki na mapenzi mazito sana kwa chama chako cha Magamba, kila mtu anajua watoto wetu wanakaa chini lkn hakuna jinsi kuna mambo ni lazima yafanyike, kila kitu tukifanya kwa tafsiri ya kubana matumizi itafika mahali hata tutaambiwa makanisani tusitoe sadaka kanisani au ili tubane matumizi, nina uhakika hilo katazo halilengi kukusanya hela bali ni kuikoa serikali ya Magufuli na misuko suko ya mijadala huko bungeni, kama serikali inabana matumizi basi iache watu binafsi wafanye hiyo coverage huko bungeni na sio kuwatisha mjadala ukiwa mkali wakate matangazo.
 
Naona pro ccm wanajitahidi sana bunge lisionzeshwe hiz sio zama za ujima jamaa tunajidai eti democracz ya habari imekuwa huku mkiwanzima wananchi kupata uhuru wa kusikilya kianacho endelea kweli tz kila kitu kinawezekana.
 
Badala ya kujadili ukosefu wa maji kwenye Majimbo Yao wanataka kuuza sura runingani!!! Bora tusione kabisa hili Bunge. Waziri Nape katoa Maelezo ya Serikali juu ya sababu za kutorusha live. Bado hamuelewi tu???kutumia bilioni 4 kutangaza sura za wabunge wakati watoto wanakaa chini na Akina mama wanajifungulia sakafuni ni busara kweli????????????????

Tafakari Bro hii picha chini hapo then utajua umelalia wapi.
ImageUploadedByJamiiForums1453909876.330386.jpg
 
Inapofikia Wabunge hawana kitu cha maana cha kujadili basi hata Yale mambo ya kipuuzi hugeuzwa kuwa mjadala!!
Majinga sana. Unakumbuka hata kwenye mjadala wa katiba walikosa mambo mazuri sana yakiwemo ya kuhoji matokeo mahakamani kwa kung'ang'ania serikali 3 hadi wakatoka nje ya bunge! na sasa eti ishu ya live tbc nayo inakuwa ni.chanzo cha vurugu huku kila siku wanaiponda tbc .
 
Hata likionyeshwa kuna mtu anakuwashia TV?

We kaa pembeni tutaangalia wengine kama wawakilishi wetu wanafanya tulichowatuma au la.

Kuhusu gharama kama ni kweli wanajali wafute mbio za mwenge then hiyo hela itumike kurusha matangazo ya bunge live.
 
Kwa hawa TBC hata taarifa ya habari wasi
rushe kupunguza ghara
ma maana habari wanazo
rusha ni comedy tuu na ni
hasara kwa taifa hili

Ila itafutwe kituo kingine
Chenye weredi warushe
Bunge live maana ni haki
ya kikatiba kupata habari.
 
Katika hali ya kushangaza wabunge wa upinzani leo wamefanya vurugu kitendo kilichosababisha Polisi wa kutuliza ghasia kuingia ndani ya ukumbi wa bunge ili kurejesha hali ya utulivu.

kitendo kilichofanywa na upinzani ni kujiabisha na kuonesha kwa dhati kuwa hawana nia ya kupigania yale ambayo wametumwa na wananchi zaidi ya kutaka umaarufu. Kwa vyombo viwili vya serikali kurusha matangazo ya bunge kwa wakati mmoja ni kupoteza muda na kuwanyima haki watanzania wengine ambao siasa kwao sio kipaumbele. Nia ya vyombo vya serikali ni kuelimisha, kufundisha na kuburushia wananchi wote na sio baadhi tuu ambao wana mlengo wa kisiasa.

Nia na Matarajio ya Watanzania ni kufuatilia kwa karibu shughuli za bunge na ni haki yao ya msingi. Kama TBCFM itarusha hayo Matangazo ya bunge moja kwa moja kuna haja gani ya kurusha matangazo hayo hayo kwa njia ya Televisheni? Tuweke mahaba kando na tujadili hii issue kwa utashi na weledi uliotukuka.

Sio watanzania wote wenye TV makazini kwao au sehemu wanayoyofanyia kazi. Bunge linaendeshwa muda ambao kila mtu yupo kazini au katika shughuli zao za kujipatia kipato sasa hamuoni kuwa kuonyesha hilo bunge ni kujitia hasara. Naunga mkono hoja ya Waziri wa habari kwa kipindi kwa bunge kuonyesha muda wa usiku kwani asilimia kubwa ya watu wazima na wapiganiaji uchumi wa nchi wanakuwa wako majumbani na wanapata muda wa kufuatilia kilichojiri bungeni kwa siku hiyo.

Suala la Bunge kuonyeshwa katika TV sijui lengo la hawa wanaopigania ni nini? Dereva bodaaboda hana TV muda wa kazi, Kondakta, Mama Ntilie, Wabeba Mizigo, Wakulima, Madereva, wafanyakazi wa maofisini katika sekta za viwanda na biashara katika mashirika ya umma na binafsi hawa wote Bunge kwenye TV watafuatilia saa ngapi kama sio kupoteza kodi zetu bure. Nasema TBCFM INATOSHA HAPA KAZI TU KUUZA SURA KWA MKEO.

NOTE: LEO NIMEGUNDUA WAFUASI WENGI WA VYAMA VYA UPINZANI NI WATU AMBAO HAWANA KAZI NA WAPIGA MAJUNGU MUDA WA KUFUATILIA TELEVISION MNAUPATA WAPI WAKATI BUNGE LINAENDESHWA MUDA AMBAO VIJANA WENYE NGUVU NA AKILI TIMAMU WANATAKKIWA WAWEPO KATIKA SHUGHULI ZA KUJITAFUATIA KIPATO?

HAINGII AKILINI HATA KIDOGO KUONA WABUNGE ETI WANACHAFUA AU KUFANYA VURUGU BUNGENI KWA SABABU TUU HAWATAONEKANA KWENYE TV. WABUNGE WA UPINZANI NI JIPU NA INABIDI LITUMBULIWE.

NJIA BORA YA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE NI KWA NJIA YA RADIO NA SIO TV KWA WENYE AKILI NADHANI WATAKUWA WAMEELEWA.
 
WABUNGWE WANAPOSHO KUBWA WALIPIE WENYEWE KUTOKA KWENYE POSHO ZAO KAMA WANATAKA KUONEKANA SISI TUNATAKA TUWAONE MAJIMBONI KAMA ALIVYOKUWA ANAFANYA DEO LUNJOMBE NA KUWA MBUNGE ALIYEPATA HESHIMA KUBWA TANZANIA
 
Nimeshangaa kuona wabunge wanapoteza muda kujadili hili swala. Kwa wananchi wa kawaida hii siyo issue muhimu. Kama serikali imesema inataka kubana matumizi nilidhani waheshimiwa wabunge wangeunga mkono.

Wengine watasema ni haki ya wananchi kufuatilia mijadala na mimi naungana nao lakini je serikali si imesema TBC watarecord na kutuonyesha baadae? Kwanini wabunge wapigane? Ama kuna agenda za siri ambazo wengine hatuzijui?

Mimi ni mtanzania ninayefuatilia mabunge mengine hasa ya nchi zilizoendelea kama Uk. Wenzetu wana live coverage ya nusu saa mara moja kwa wiki na ni siku ya jumatano kuanzia saa sita mpaka saa sita na nusu. Na hii ni siku maalum ambapo Waziri mkuu anapata kipindi kinaitwa PRIME MINISTE'S QUESTION. Zaidi ya hapo labda kuwe na suala muhimu na dharula na hii ni nchi tajiri ambayo wananchi wanalipishwa kitu kinaitwa TV LICENCE. Ambao kimantiki wakiwa na mawazo kama yetu wanahaki zaidi ya kudai kuona kila kitu live maana wana ifund tv yao siyo sisi tunalipa in direct.

Cha msingi wabunge wangeisukuma serikali ikusanye mapato zaidi na hata waishauri ianze kulipisha kila mtu mwenye tv awe na leseni. Hapo kuwe na kitu kinaitwa channel ya bunge kama uk bbc parliament.

Zaidi ya hapo sioni kama serikali imekosea na tujue RAIS KASEMA AWAMU YAKE NI YA KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI KAMA TUMESHANGILIA MAWAZIRI KUNYIMWA SAFARI ZA NJE TUSHANGILIE NA SISI KUNYIMWA LIVE COVERAGE YA BUNGE.
 
nauliza kwani waandishi wa habari hawapo bungeni? ?? kwani hawatoi habari kwa wananchi? ??
kuna waginjwa mahospitalini hawana dawa sahizi. kuna wananchi wanakufa na njaa kule dodoma wanakula mafinyofinyo. yaani ni balaa tupu! eti watu humu wanashabikia mabilioni yakatumike eti kuonyesha live tu bunge. then baada ya kuona litakutatulia matatizo ukishaangalia. nini hasa mantiki yake. au wabunge watuonyeshe jinsi wanavyojua kutumbua majipu! ! baasi
 
Back
Top Bottom