Kama Slaa, Migiro, Salim, Lowassa, Shein hawafai kuwa Rais; nani atatufaa 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Slaa, Migiro, Salim, Lowassa, Shein hawafai kuwa Rais; nani atatufaa 2015?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Dec 30, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ukifuatilia kwa karibu kwenye thread mbalimbali zinazoanzishwa humu ndani kuhusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa nafasi ya Urais utagundua majina yanayotajwa sana kufaa na kutokufaa kuwa Rais wa JMT ni haya ya kina Asha Rose Migiro, Edward Lowassa, Salim Ahmed Salim, Mohamed Shein na Wilbrod Slaa.

  Asha Rose Migiro

  Huyu mama ni msomi na ni mama ambaye anaheshimika kwa kutokuwemo kwenye kashfa mbalimbali za kifisadi. Utumishi wake kwenye nyanja ya siasa si wa muda mrefu sana lakini amepanda vyeo haraka haraka hadi kufikia nafasi aliyo nayo sasa ya unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa. Wanaompigia chapuo huyu mama wanasema kutokana na elimu na nafasi yake aliyo nayo sasa amepata uzowefu wa kutosha kuwa Rais wa Tanzania na ikitiliwa maanani Marais wote wanne waliopita walikuwa ni wanaume, basi sasa ni zamu ya mwanamke kuwa Rais wa Tanzania.

  Lakini wanaompinga Migiro wanasema hata hiyo nafasi yake aliyonayo ni nafasi iliyotolewa na Ban Ki Moon kama upendeleo kwa Tanzania baada ya Tanzania kupigana kufa na Kupona kuhakikisha kwamba Ki Moon anakuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Wanadai Migiro yuko hapo alipo si kutokana na weledi wake kwenye siasa bali ni kutokana na uhusiano wake Binafsi na Rais Jakaya Kikwete.

  Salim Ahmed Salim
  Huyu ni mtu ambaye watu wengi hawahoji usomi wake wala uzowefu wake kwani anajulikana na kuheshimika kwa vitu hivyo viwili, yaani usomi na uzowefu wake kwenye siasa baridi za nchi hii. Salim aliwahi kujaribu kuwa mgombea Urais enzi za mfumo wa chama kimoja hapo mwaka 1985 lakini akashindwa kwa kura na Ally Hassan Mwinyi kwenye vikao vya CCM vya kupitisha mgombea Urais. Miaka 20 baadaye (2005) alijaribu tena na safari hii akashindwa tena kwa kura na Jakaya Kikwete.

  Kwa wengi wanaomuunga mkono Salim wanaona yeye ni mtu bora kabisa ambaye kama taifa alifaa kuwa Rais wetu lakini amekumbwa na msinambi wa kukataliwa na watu wa "kwao" Zanzibar kwa sababu za Kihistoria. Lakini kwa wale wanaompinga Salim wanaona ni mtu anayesafiria nyota ya kupendwa na Mwalimu Nyerere lakini yeye mwenyewe hana kitu cha kukumbukwa ambacho amewahi kufanya akiwa mwanasiasa hapa nchini wala kwenye ngazi za kimataifa.

  Edward Lowassa
  Lowassa anajieleza na mfanikio na kuanguka kwake kunajieleza pia. Mbali ya kuwa ni mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwenye mizingo ya kisiasa mwaka 1995 alilazimika kurudi nyuma na kumtanguliza Rafiki yake Kikwete kupambana kugombea Urais baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kumkataa na kupiga kampeni ya Lowassa kukataliwa na vikao vya uteuzi ndani ya CCM.

  wanaomuunga Mkono Lowassa wanaamini kwa hali tuliyonayo hivi sasa ya kuwa na serikali isiyofanya maamuzi kwa wakati au kutokufanya maamuzi kabisa, basi tunahitaji mtu kama Lowassa ambaye huwa hasiti kufanya maamuzi hata kama maamuzi hayo yatamletea madhara ya kisiasa na hadhi yake kiujumla.

  Lakini Lowassa amelibeba tangu mwaka 1995 zigo la tuhuma za kuwa na mali nyingi sana zisizo na maelezo amezipataje huku wengine wakizihusisha na nafasi ya ukuu wa Ukumbi wa Mikutano wa Arusha aliowahi kuwa nao, na wengine wakisema mali hizo zimepatikana kutokana na Lowassa kujihusisha na mitandao ya kiuhalifu. Lowassa anaonekana kuchafuka zaidi kuliko wote wanaotajwa kufaa au kutokufaa kugombea Urais 2015

  Wilbroad Peter Slaa
  Slaa ni ingizo jipya kwenye nafasi hii ya ugombea Urais wa JMT. Nguvu kubwa aliyo nayo kutokana na matokeo na Kampeni zilizokuwa zinajaza watu kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Slaa anafahamika kwa misimamo yake isiyoyumba kwa mambo ambayo anaamini yana maslahi mapana na makubwa kwa taifa letu. Slaa siasa zake zimejikita zaidi kwenye falsafa ya " No research No right to speak" kuendesha siasa kwa kufanya utafiti.

  Nguvu ya chama chake cha CHADEMA na uwezo wake wa kujenga hoja umemjengea umaarufu Slaa miongoni mwa vijana na wasomi wa nchi hii. Kwa upande wa wale wanaompinga Slaa wanasema Slaa ni mropokaji, anapenda uimla, hana uwezo wa kuendesha Oganaizesheni hata ndani ya chama chake, ni mwepesi wa kufikia hitimisho kwa kutumia hisia zake tu na wanadai Slaa amewekeza kwenye udhaifu wa CCM bila yeye nweyewe kuwa na maono Yakinifu mbadala.

  Mohamed Ally Shein
  Huyu naye ni gwiji kwenye nyanja yake ya utabibu na kwenye siasa si mtu mwenye makeke wala kupenda kujitangaza (Publicity) sana kama walivyo wanasiasa wengi wa Tanzania. Shein anaheshimika zaidi kwa utu uzima wake na kufanya kwake maamuzi bila ya kuegemea upande wowote. waliowahi kufanya naye kazi wanadai kwamba kwa Shein mwenye haki atapata haki yake na asiye haki hapati upendeleo wowote hata kama ni rafiki wa namna gani wa Shein.

  Shein aliingia kwenye duru za siasa kitaifa baada ya kufa ghafla kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Omary Ally Juma. Tangu wakati huo Shein ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza bila ya kuwa na papara ya kufanya maamuzi na yeye amejitenga kwa kiasi kikubwa na siasa za kimkakati za Zanzibar. Lakini kwa wanaompinga wanadai Shein akiwa Rais hawezi kuubomoa mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki kwenye nchi yetu kwa sababu ni mfumo huo ndiyo unaolea viongozi waliopo sasa ambao ndiyo kama Shein atataka kuwa Rais wa JMT basi hana budi kuigia nao mkataba wa kuwalinda pindi atakapokuwa Rais.

  Hawa watu watano ndiyo wanaotajwa sana kufaa kuwa Rais wa Tanzania lakini ni hao hao pia ndiyo wanaoongoza kwa kutajwa kutokufaa kuwa Rais wa Tanzania. Kama hawa hawafai ni nani basi anayefaa kuwa Rais wa Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji kiongozi ambaye hajawa "tainted" na rushwa. Tunahitaji kiongozi ambaye atapambana kwa dhati kuondoa mfumo ambao umewezesha rushwa kukithiri nchini. Kati ya wote uliowataja ni wawili tu ambao wakisema watapambana na rushwa na kuwatizama usoni wanaaminika kuwa watafanya hivyo. Na hao ni Salim Ahmed Salim na Wilbroad Slaa. Wengine wote kwenye hiyo orodha ni mageresha tu.
   
 3. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kazi yetu Watz badala ya mawazo ya maendeleo, tumekwama kwenye kuwaza marais 2015. Tukishampata wa 2015, tutaanza wa 2020...
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hatujakwama kwenye kufikiria uchaguzi wa 2015 bali tumeshachoshwa na hawa waliopo na hatuna tena imani nao. Maendeleo yanafanyika lakini yanahitaji msukumo mpya na hauwezekani kutoka kwa hawa waliopo sasa.
   
 5. m

  masabuda Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Harrison Mwakyembe
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  KATIBA MPYA kwanza. Kuwazungumza watu bila kuwasikia wana agenda gani kwa TAIFA hili, bila kujua kama wanazifahamu nyufa mpya na za zamani zinazotuhangaisha, bila kuwaandalia ILANI ya TAIFA na kuwapima kuona kama wanaweza kuitekeleza, bila kujua vyama vyao vitawasaidiaje kutekeleza ilani ya Taifa na sio za vyama vyao,..., tutarudi humohumo.
  Kuna wengine umewataja humo inasemekana wamefanya maangamizi makubwa kuuweka utawala uliopo madarakani. Bado tunawataka tu!
   
 7. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WildCard nakubaliana na wewe kwamba KATIBA kwanza, lakini lazima tukubali katiba zote hutungwa kwa kuzuia au kuruhusu mambo fulani fulani kutokana na TABIA za viongozi waliiopo na wananchi wa nchi husika. Unafikiri wamarekani walipoweka kwenye katiba yao kwamba kila mtu ana haki ya kumiliki silaha ILIZUKA tu hivi hivi?
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu wanatajwa wengi tu:

  Dr. John Pombe Maghufuli
  Mr. Membe
  Mr. Six
  Mr. Sumaye
  Mr. Mwinyi
  Ms. Tibaijuka, nk.

  Mkuu analysis yako ni nzuri kwa hao watu uliowataja lakini bahati mbaya hujatuwekea umri wao ifikapo October 2015 ambao ni mwezi wa uchaguzi.

  Matatizo yangu ni kwamba watu humu JF tumekuwa tukisema wazee wetu ni vyema wakapumzika kama tulivyotoa maoni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Lakini linapofika suala la Urais tunawaangalia watu ambao wako beyond 60 years! Hawa wanatakiwa wawe wameenda kupumzika baada ya kuutumikia umma (Najua urais hauna retirement age).

  Nadhani kwa mantiki ya kutaka vijana watwae madaraka basi ni vyema wakatwaa na Urais pia. Ningefurahi kuona wana JF wanakuwa chachu katika hili kwa kuwapendekeza vijana na si wazee ambao wanatakiwa wawe washauri tu kama mzee Mtei, Kisumo, nk.

  Ningefurahi kuona tunawapigia chapuo vijana na wala si babu zetu (najua wana JF wengi ni .com na Tab).

  Kwa nini tusifikirie majina kama haya:
  • Emmanuel Nchimbi
  • Zitto Zuberi Kabwe
  • John Mnyika
  • January Makamba
  • William Ngeleja
  • Nape Nnauye
  • Halima Mdee
  • n.k
  Lakini wawe of age but below 60 years by October 2015. Kila siku wazeee wazeee. Ni muda muafaka wa kutafuta vijana na kuwakabidhi mikoba. Ila wasiwe wavuta shisha tu!
   
 9. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Madhaifu mengine yanaweza kurekebika, lakini ya Silaa hapana, anatupeleka kubaya zaidi ya hapa. Lowasa tunaweza kutaifisha mali zake, Asha, Salim, Shein wanaweza kudhibitiwa na Katiba iliyo serious. Lakini la Silaa ".......mropokaji, anapenda uimla, hana uwezo wa kuendesha Oganaizesheni hata ndani ya chama chake, ni mwepesi wa kufikia hitimisho kwa kutumia hisia zake tu .....amewekeza kwenye udhaifu wa CCM bila yeye nweyewe kuwa na maono Yakinifu mbadala." Haya hayarekebishiki wala hayadhibitiki.
   
 10. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hata kama unayosema yangekuwa kweli(kwa sbb mimi siamini hivyo) bado hatuwezi kuongelea jambo litakalofanyika 2015 leo. Ni muhimu kuangalia lililopo machoni kwa sasa ambalo ni la maendeleo ya kila mmoja wetu na taifa kwa ujumla. Labda kama tunajadili mipango yetu ya muda mrefu, hapo sawa. Ila hapa hatufanyi hivyo. Nakupa mfano wa mpira: Simba na Yanga, mmojawapo kafungwa na ligi inaendelea. Sasa badala ya kuangalia mipango ya timu kwa mechi zingine kwenye ligi, tuanze kupanga list ya wachezaji kwa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa miezi kadhaa baadae.
   
 11. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Kwa nini tusifikirie majina kama haya:
  •Emmanuel Nchimbi
  •Zitto Zuberi Kabwe
  •John Mnyika
  •January Makamba
  •William Ngeleja
  •Nape Nnauye
  •Halima Mdee
  •n.k

  Afazali Zitto mi namkubali, Lakini hawa wengine mmmmh.... Mungu apishie mbali
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Timu ipo uwanjani inaboronga na dirisha dogo linakaribia ni kwa nini usifikirie kununua wachezaji watakaoziba udhaifu unaoonyeshwa na waliopo uwanjani? Hata Wenger siku hizi kabadilika!!
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ngoja KATIBA MPYA itupatie sifa na miiko ya UONGOZI tunaoutaka sasa huko tuendako. Tunakotoka na tulipo tumekosea sana tu na inatugharimu sana.
   
 14. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Watz. Kwa bla bla na shortcut tupo mbaaali! Lakini kwenye mambo ya msimgi tumeyapa kisogo.
   
 15. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hilo bandiko langu ni la tarehe 6 Mei 2008 miaka zaidi ya mitatu iliyopita lakini ndenda kwenye hiyo thread si zaidi ya watu 40 ambao wamechangia kwenye hoja za katiba mpya. Mimi najua nni rahisi watu kuzungumzia katiba lakini kwa uzowefu nilioupata sidhani kama watu wako makini kujadili katiba mpya kuliko kujadili uchaguzi wa mwaka 2015.
   
 16. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mtoa mada nakupongeza kwanza kwa kuleta orodha angalau kdg ina uwiano kuhusu na hali ya kisiasa na pili kuanisha sifa za hao wagombea angalau kwa muonekano ambao watanzania wengi wanaweza kukubaliana nawe.

  Lakini mm naona ni matatizo na mahitaji ye2 mpaka kufikia mwaka 2015 ndy yatakayo toa Mgombea urais anayèfaa. Wote wanaowania nafasi hii wajiulize wanauwezo wa kuisaidia Tanzania? kukabiliana na hayo? Na tukiwatazama usoni mwao kweli wana uwezo huo na sifa? Kama wapo na wanaweza bs tutaanza kutafuta majina yao.. Lakini cha msingi ni kuangalia mahitaji ye2 kwanza,, Rais wetu wa sasa mh, jakaya ameacha uwanja mpana sana katika hili watu tunaona mapungufu yote yaliyojitokeza kuanzia uhuru mpaka sasa kuanzia ngazi , nyanja, mpaka sekta zote na siasa watu wamekuwa huru kujadili kila jambo bila uwoga ingawa wengine wanaitumia vby nafasi hii,, lakini tukiwa makini wote wenye nia njema ya kuongoza taifa hili kwa nafasi zote 2015 watajichuja wenyewe bila ku2mia gharama..

  Nafikiri ni wajibu kwa kiongozi wetu alisimamie hili bila upendeleo, na kwa ngazi zote , hapo tutaianza safari ingine kuelekea miaka hamsini ingine tukiwa na rais mwenye uwezo na mwenye nguvu ya kukabiliana na hali iliyopo...

  Na ni lazima awe amejiandaa kweli kweli na kwa muda mrefu( namaanisha uzowefu). Siyo mtu anaibuka tuu na kuanza kuwafuraisha watu majukwaani kwa maneno na porojo za ahadi ambazo hazitekerezeki,, kuwadanganya wananchi hata wasiwajibike hata kuitumikia serikali yao kama kutokulipa kodi na kuchangia shughuli za maendeleo. Hawa hawatufai kbs.
   
 17. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kuna wale wanaohubiri kuwa hivi sasa ni zamu ya Wanzanzibari, tena Wapemba, vipi mbona umemsahau Maarim Seif! Tehe tehe tehe
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna uhusiano wowote kati ya umri wa mtu na uwezo wake kuongoza. India ni nchi inayoendelea kwa kasi sana ki uchumu na inaongozwa na waziri mkuu wake Singh ambae umri wake ni zaidi ya miaka 70. Marekani haijapata kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi kama ile miaka nane ambayo Ronald Reagan alikuwa Rais wao na yeye wakati akiwa Rais alikuwa na zaidi ya miaka 70!! Sina haja ya kutoa mifano lakini kuna nchi zinaongozwa na watu wasio na umri kama niliowataja hapo awali , lakini nchi zao ingawa ni tajiri wa maliasili uchumi wao ni hohe hahe; kazi kuzunguka dunia nzima kuomba omba misaada!! Tusiwakatae watu kuongoza nchi kwa sababu ya umri wao, dini zao rangi zao na makabila yao; watu wapewe nafasi stahili kufuatana na jinsi wanavyoweza kuliletea Taifa maendeleo. Vijana wamepewa kuendesha wizara ya Nishati na kila leo tunalala giza wenyewe wako Rose garden kula bata!!
   
 19. M

  Mwl Ryoba Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ktk sifa za kiongozi hakuna swala la age.unaweza ukawa kijana au mzee lakini mambo yasiende vizuri.mojwapo ya sifa zakiongozi ni
  1.maturity and not of age but mind:it is age independent.
  2.optimistic
  3.faithfulness
  4.flexibility etc
  kwa hiyo mambo ya uzee au ujana hayana tija.hata kikwete aliaminiwa eti kwa sababu ni kijana kumbe hana lolote,hivyo tunamhitaji kiongozi mwenye maono ya kuwainua watanzania ambao wamekata tamaa ya maisha kwa sababu ya upofu wa mioyo ya viongozi wetu.
  Tunamuhitaji kiongozi kama Nyerere aliyekuwa na huruma kwa watz.
  By diwani stand kuu serengeti.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimekuelewa. Mimi nilijikita kwenye umri tu siyo dini wala kabila!! Mantiki yangu ni kwamba tusiwe na double standard. Kwa Lubuva tukasema mzee lakini linapokuja suala la Rais kwa kuwa mtu watu ana umri zaidi ya miaka 60 basi tunasema uzee dawa!!
   
Loading...