Kama siyo TANESCO Basi Waziri mwenye dhamana ya umeme acha kupuuza kelele za mitandao ya kijamii

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nadhani lipo tatizo lakukatika umeme mara kwa mara hasa Dar, hii ni kwa mujibu wa wananchi wanaotumia social media. Mliopo dar mnaweza kusaidia kama Kuna ukweli ndani ya hizi habari.

Lakini nichukue fursa hii kuwakumbusha Tanesco au Wizara kuchukua hatua. Kama kelele hizi zina ukweli watafute ufumbuzi wa tatizo na kama hazina ukweli maafisa habari kanusheni adharani.

Kumbukeni mteuzi wenu yupo Dodoma na anasoma kinachoondikwa huku mitandaoni, nadhani vipo vinavyomkera hasa hizi taarifa za kukatika umeme kwa sababu amejipambanua kama mwanamapinduzi wa viwanda na Tanzania ipo uchumi wa Kati, Kama nishati itatiliwa mashaka basi wawekezaji wataogopa kutia mitaji yao na wale waliotia mitaji yao watapata hasara.

Umeme tuliambiwa ni historia kwanini ukatikekatike?
 
yaani wa tegeta ndio kabisaa hata luku ikiharibika wanachukua wiki mbili kukuhudumia
 
Back
Top Bottom