Uchaguzi 2020 Kama sisi wapinzani tunataka kuingia Ikulu kivyetu tusimamishe mtu mnafiki ajifanye kuhubiri amani na utulivu

manafyale

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
280
250
Ndugu zangu wapinzani najua sana ukikosoa tu, cha kwanza unapata jina la ubatizo mtakatifu kuwa ni mamluki, umetumwa na mengine mengi. Ndugu zangu hata Mungu kama wewe ni msomaji wa Biblia utaona alikuwa anatulia anafundishwa na Musa na anakubali maelekezo sembuse Chadema na wapinzani? Tutakaa sana kwa ubishi na ukilitimba.

Kama ukituliza kichwa ukatulia na kuelewa utagundua siasa za Tanzania na Watanzania ni tofauti sana na siasa za Malawi, nitofauti na siasa za Kenya, ni tofauti na siasa Kongo, na nitofauti na siasa za Uganda. Na ukiwa mchunguzi sana utaweza kugundua nchi kama Zimbabwe yaani ZANU PF huwa wanakuja Tanzania kufanya mafunzo yote ya siasa hapa. Pia ANC nayo wanafanya kama ZANU PF na wameona manufaa yake ndiyo maana wanakujaga kimya kimya na wanarudi kwao wanamaliza biashara.

Wapinzani wengi wanaangalia siasa za kenya au Zambia na kunawakati mwingi wanalinganisha siasa za Tanzania na siasa za Marekani na kunawakati wanaenda mbali zaidi hata kulinganisha siasa za Tazaniaza na UK kule kwa malikia aliyeanza kutawala tangia 1952, hapa ndiyo tunapotea kabisaa. Watanzania wameathiliwa na siasa za Mwalimu, natoa siri, watanzania hawapigi kura kwa sababu ya maisha magumu, hapana, Watanzania ni watu wa tofauti sana hawapigi kura kwa sababu eti kunanjaa, hawapigi kura eti kwasababu hawana pesa no. Haya huwa hayawabadilishi hata kidogo. Watanzania wanataka kusikia neno AMANI NA UTULIVU basi. Wenyewe wameaminishwa kwa imani moja kuwa kama AMANI NA UTULIVU utakuwepo basi kunauwezekano wa mengine mazuri kuwepo. Vinginevyo wanawekaga ??????

Siku mpinzani yeyote atakapoamka na kuaza kuubiri haya CCM itakuwa bai bai maana ni chama kizee ambacho kimekosa mtoto wa kumrithi wengi ni wahuni wanataka kuwapa watanzania dotrini ambayo hawana hivyo wanakuwa na wasi wasi sana na mgombea huyo, na CCM inazidi kutawala na itaendelea kutawala maana tunaiga siasa za Kenya na Ulaya. Ndiyo maana Lowasa alipata kura nyingi sana kwani na yeye ni muuminina wa AMANI NA UTULIVU tuambiane ukweli.

Na kama sisi wapinzani tunataka kuingia Ikulu kivyetu basi tusimamishe hata mtu mnafiki ajifanye kuubiri AMANI NA UTULIVU alafu akiingia anakuwa kama Chiruba ataendelea kuamsha dude. Tunafeli wapi hata kuvaa ngozi ya kondoo tu tunashindwa, tunabaki na kutangaza maandamano na fujo neva evah Ikulu itakuwa hadithi. Leo mmetuletea Lisu msiseme natabiri liko wazi hata tukizili bila nguo hashindi ila tunakamilisha utaratibu na kujifariji tu, ila kushinda hakupo wandugu. Watanzania ni waajabu hawajachoka kama Walibya, sisi tunauoga sana alafu tuna tatizo la kufikiria vitu na hili ni tatizo na pia na kumkumbuka Nyerere na maneno yake. Pia wapinzani tutengeneze propaganda za kuwakataza wananchi wasimsikilize Baba wa taifa kwani bado anatuharibia sana sisi kuingia Ikulu kwa njia ya fujo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom