Kama sio usanii kauli mbiu ya ccm igunga ingelikua "tunajivua magamba"

Jan 16, 2007
721
175
Kwa anaefuatilia kampeni za uchaguzi Igunga kwa upande wa CCM kuna vitendo ambavyo hata mtu asie na akili timamu anaweza kujiuliza na jibu akalipata bila kuumiza kichwa "yote yanayoendelea Igunga kwa CCM ni usanii.Kwanza tujiulize uchaguzi wa Igunga unafanyika baada ya Mbunge Rostam kujiudhulu kufuatia tuhuma za ufisadi na ikiwa hatua ya CCM kujivua magamba,sasa iweje mtuhumiwa mkuu katika kashfa ya magamba alambwe miguu na kubembeleza kuongoza kampeni za CCM kumpata mbunge mpya????Pili kama mbunge aliyepita kaondoka ikiwa matokeo ya kujivua magamba kwanini Chama tawala CCM kukwepa walau katika kampeni zao kunyoosha kibao vita vya mafisadi au kujivua magamba???Kwa mawazo yangu kauli mbiu ya CCM kama wanania nzuri kwa wana Igunga na Watanganyika ingelikua"TUNAJIVUA MAGAMBA MWANZO ROSTAM AZIZI WENGINE WANAFUATA"Hapo tungewaelewa.Lakini katika kampeni zao mbali na kukwepa kutamka neno mafisadi wanajaribu kwa kadri ya uwezo wao kutomuudhi Rostam Aziz.WANAIGUNGA FANYENI UAMUZI WA MAANA MSIGEUZWE MAZUZU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom