Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
132,649
2,000
Si mlikuwa mmechoshwa na upole wa JK nyinyi? Mmeanza kumkumbuka hata mwezi haujaisha. Tena wengine mlisema rais ajaye awe dikteta. Sasa kilio chenu kimesikiwa makelele ya nini tena?
 

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,839
2,000
Huyu ndie rais Tz inamtafta, ww ilimpigia chapuo Eddo wako subir siku edo akiwa rais ndo mwekee misingi yako.... Goo John Gooooo
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,915
2,000
Mkuu hii ni DEMOKRASIA MTAMBUKA...! Hautaki....Rejea kauli ya Membe kipidi cha dk 45 ITV.
==================================
Pasco CSR gani unazungumza zaidi ya hiyo ya kununua vitanda....! Charity ya hizo kampuni imekusanywa pamoja....kutatua kiasi tatizo sugu la hospitali kuna ubaya gani hapo...!?
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu 'YES!", "ndiyo mzee!". Ila kwa hali ninayoina sasa, jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kamu huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, kuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokotaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli atafanikiwa sana!.

Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporation, kama sehemu yao ya CSR kuwakiimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private entities watumieje fedha zao?!, kwa sheria ipi, kanuni ipi na taratibu ipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!.

Alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, agizo hilo amelitoa kwa mamlaka gani?!.

Njuavyo mimi mashirika na makampuni yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli za CSR ili ku achieve specific objectives kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge liliomba udhamini wa mlo wa usiku, na mashiika na makampuni wakaona zina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa, rais alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia na kuamuru diferent use ya private money?!.

Hata kama rais ameona matimizi yale yalikuwa ni anasa tuu, angeliamuu bunge likatae michango hiyo, na kuirudisha kwa wenyewe ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, angeomba kama waombaji wengine!.

Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jinginekufuta parade ya uhuru!. Swali ninalojiuliza hivi kumbe parede ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli ais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya parade ya uhuru yafutwe just like that?!, mamlaka hayo rais wetu ameyatoa wapi?!.

Mbaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama atasitisha utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia pesidential decrees pekee?!.

Kuna Jambo niliwahi kulizungumza hapa, sasa naona kama linakwenda kutokea!.

If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Pasco.
Talking of presidential decrees...hazikutakiwa kutumika katika nchi zinazohubiri utawala wa kidemokrasia. Kwenye nchi za kifalme yes!
 

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
9,442
2,000
Kwa nia ya kusave money ni uamuzi mzuri sana. Uzuri kaishasema hizo pesa za Uhuru zinaelekezwa wapi!!!!

Tuacheni kushabikia sherehe wakati wagonjwa wanalala chini, dawa hakuna, maji hakuna, umeme shida eti tunakomalia tufanye shehere, what for???
 

Clemence Baraka

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,597
1,500
Hata kama ni cost cutting sio kufuta kabisa ile fhifa ya kitaifa

Jamaa wa parade waende wapige kwata wale hakuna posho mshahara si wanalipwa

Jiburudishe na parade za zamani kama ulizirekodi. Zinasaidia nini? Watu mlo wa pili hawana unangangania kwata.
 

nyantasingah

New Member
Mar 16, 2013
3
0
Tumuunge mkono rais wetu JPM, nilivyoelewa hajafuta sherehe kwa kiburi tu bali ameeleza sababu ya msingi kwamba maeneo mbalimbali nchini yanakabiliwa na kipindupindu mnataka busara gani zaidi ya hizo. Au mnataka turudi mwaka 1992 madaktari na manesi wamegoma mhimbili rais wa wakati huo (mzee ruksa) yuko uwanja wa taifa kumpokea kanda bongoman?. halafu wewe elewa kuazimisha sio lazima gwaride tupate staili zingine kama hizi kulingana na mazingira. ndiyo kusema ingetokea ajali mbaya bado ungeendelea kupigia debe sherehe?
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
132,649
2,000
1448298525473.jpg
 

AdanaVural

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
616
500
Kwangu hata akisema ku.tom.ba mara moja tu kwa wiki na goli moja tu na muda uliobaki tukafanye kazi ili tutoke hapa, sawa tu! Kama unataka mambo ya demokrasia, kuandamana na kuunda tume ya kila upuuzi hamia Kenya huko ndiyo kuna huwo upuuzi, ila hapa kwetu ni amri tu ktk juu kushuka chini na hakuna kupingwa!

Aisee mmehamasika kweli, kama vipi tumshauri atuletee zile sera za china kabisa kina Pasco watapukutishwa kweli
 

Lisa Rina

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
2,166
2,000
umeongea vyema kabisaaaaa!!!u dictator pkus usanii alafu ukiwa unaongoza mapoyoyo basii utawala kunoga kweli!
 

Yurri

Senior Member
Apr 29, 2015
136
250
Do you mean raisi alifanya kosa kuzielekeza pesa zile kununulia vitanda vya hospital.
 

luck

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
991
1,000
mwezi umeisha bila baraza la mawaziri, mtu mbili tu zinaendesha nchi magufuli na ombeni tosha kabisa, pale bungeni walivyokuwa wanafanya fujo angelifuta bunge palepale ingekuwa bonge la big up.


Nimecheka sana hapa
 

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
6,997
2,000
umeongea vyema kabisaaaaa!!!u dictator pkus usanii alafu ukiwa unaongoza mapoyoyo basii utawala kunoga kweli!

Wewe mpuuzi jitazame sana! Usidhani kuwa kwako JF kuna kuhakikishia usalama. Tutakutafuta na kutakufanya kitu mbaya. Mshenzi mkubwa wewe.
 

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,451
2,000
Wewe unauelewa wa kutosha za kujua au kuona jitihada za rais za kujaribu kutoa nchi kwenye hili shimo. Pasco ni adui wa mabadiliko! Wewe ni adui wa mabadiliko unanitia kichefchefu
 
Last edited by a moderator:

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
22,161
2,000
Pesa ilitolewa na private entities kweli, lakini zikishafika serikali si zao tena bali ni za serikali, and we can do what we pretty much damn wish to do with it. Huna hoja. Hapa kazi tu.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,090
2,000
Mimi nashauri Magufuli atoe tamko kuwa nchi ipo kwenye mkwamo wa kiuchumi hivyo yoyote popote alipo afunge mkanda.

#Hapa Kazi tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom