Kama sio Mh Lowassa pengine tusingejua mengi katika siasa ya nchi yetu

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,323
29,584
Za asubuhi ndugu/ jamaa/ marafiki/ maadui.

Kutokana na hali tuliyofikia sasa, kila kona ni siasa tu, si wakubwa wenye sifa za kupiga kura wala si watoto wasio na sifa za kupiga kura. Stori ya mujini ni siasa na hasa uchaguzi.

BINAFSI NAOMBA MWENYEZI MUNGU AMPE AFYA NA MAISHA MAREFU SANA MH. WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD NGOYAI LOWASSA SABABU NAMUONA KAMA NI A BLESSING IN DISGUISE. Nasema hivi sababu ndugu ENL ametuwezesha kuwaona watu ktk rangi zao za ukweli, ametuwezesha tuone wasaliti wa nafsi zao na wanayoyasimamia. LOWASSA AMEKUWA KAMA CHUJIO fulani la kuchuja watu tuliodhani ni viongozi wazuri kumbe la. 'Viongozi' hawa wameshindwa kupita ktk hili chujio.

Pia upande wa sisi raia, tumewekwa ktk hili chujio na wapo waliopita na ambao hawajapita. Ujio wa Lowassa chadema umekuwa ni kipimo kikubwa sana cha uwezo wa watanzania ktk kufikiri, kuchuja zuri na baya, kufanya utafiti yakinifu, kutunza kumbukumbu na KUFANYA MAAMUZI mepesi tu na SAHHIHI bila kuumiza kichwa. Tumeona wenyewe uwezo wa watanzania kwa ujumla ktk kujenga hoja, kutetea hoja ktk misingi ya ukweli au ktk misingi ambayo wao wanaiamini.

Kupitia Lowassa binafsi nimeweza kuwajua watu ambao mwanzo nilidhani nawajua.

Najua kuwa watu tuna mitazamo tofauti ila kuna vitu vya msingi ambavyo tunaweza pishana kwa kupita njia tofauti ila tunakoelekea ni aehemu moja, hilo natambua. Ila tunapopishana kuwa nyekundu na njano sio rangi mbili tofauti, na bado mtu anajaribu kuaminisha kuwa ni rangi moja hapo kuna utata.

Hivyo sina budi KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa kutuletea Edward Lowassa. Lowassa umekuwa chujio la kipimo cha akili za watanzania.
Viva ENL.
 
Yes, Lowassa amekuwa ni tanuri la moto lililotumika na linaendelea kutumika kuwachoma viongozi wa kisiasa, wanachama, wapenzi na pia wapiga kura wasio na uhusiano wowote na vyama vya siasa.

Siku ambayo Magufuli atalizima hili tanuri Lowassa kupitia kura za wananchi wengi, ndiyo tutakapo kugundua kuna wengine wameishakuwa ni majivu, wengine wameungua sana wakihitaji msaada wa haraka.

Ninaamini kuna wachache sana watatoka salama.
 
Ujio wa Lowassa CHADEMA umewafungua macho Watanzania wengi waliokuwa wako usingizini, wengi wamegundua kumbe MABADILIKO yanawezekana, kumbe CCM sio baba wala mama yao, wamegundua kumbe CCM inaweza kutoka madarakani tena kirahisi kabisa, wamegundua kumbe CCM ni waoga sana na wepesi kabisa, wamegundua kumbe CCM ikizidiwa hadi Pushup zinaweza kupigwa majukwaani.
 
Kurasa mpya kaifungua hilo litabaki na litaingia katika historia. , .. .

Tumshukuru kwa hili
 
Hivi unaijua CUF NGANGARI WEWE?

UNAKUMBUKA ENZI ZA MREMA SEMA SEMA USIOGOPE???
 
Ebu tukumbushe, CUF NGANGARI vipi?
Binafsi naamini kuwa zama za Mrem na Lowassa ni tofauti sana, simu za smartphone na pia upatikanaji wa laptop/ desktop na pia makampuni ya simu na vifurushi vyao umefanya mapinduzi. Mrema zilikuwa zama za 'giza'. Tunategemea magazeti ya uhuru na mzalendo kupata habari.
 
Za asubuhi ndugu/ jamaa/ marafiki/ maadui.

Kutokana na hali tuliyofikia sasa, kila kona ni siasa tu, si wakubwa wenye sifa za kupiga kura wala si watoto wasio na sifa za kupiga kura. Stori ya mujini ni siasa na hasa uchaguzi.

BINAFSI NAOMBA MWENYEZI MUNGU AMPE AFYA NA MAISHA MAREFU SANA MH. WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD NGOYAI LOWASSA SABABU NAMUONA KAMA NI A BLESSING IN DISGUISE. Nasema hivi sababu ndugu ENL ametuwezesha kuwaona watu ktk rangi zao za ukweli, ametuwezesha tuone wasaliti wa nafsi zao na wanayoyasimamia. LOWASSA AMEKUWA KAMA CHUJIO fulani la kuchuja watu tuliodhani ni viongozi wazuri kumbe la. 'Viongozi' hawa wameshindwa kupita ktk hili chujio.

Pia upande wa sisi raia, tumewekwa ktk hili chujio na wapo waliopita na ambao hawajapita. Ujio wa Lowassa chadema umekuwa ni kipimo kikubwa sana cha uwezo wa watanzania ktk kufikiri, kuchuja zuri na baya, kufanya utafiti yakinifu, kutunza kumbukumbu na KUFANYA MAAMUZI mepesi tu na SAHHIHI bila kuumiza kichwa. Tumeona wenyewe uwezo wa watanzania kwa ujumla ktk kujenga hoja, kutetea hoja ktk misingi ya ukweli au ktk misingi ambayo wao wanaiamini.

Kupitia Lowassa binafsi nimeweza kuwajua watu ambao mwanzo nilidhani nawajua.

Najua kuwa watu tuna mitazamo tofauti ila kuna vitu vya msingi ambavyo tunaweza pishana kwa kupita njia tofauti ila tunakoelekea ni aehemu moja, hilo natambua. Ila tunapopishana kuwa nyekundu na njano sio rangi mbili tofauti, na bado mtu anajaribu kuaminisha kuwa ni rangi moja hapo kuna utata.

Hivyo sina budi KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa kutuletea Edward Lowassa. Lowassa umekuwa chujio la kipimo cha akili za watanzania.
Viva ENL.
Ujio wa Lowassa CHADEMA umewafungua macho Watanzania wengi waliokuwa wako usingizini, wengi wamegundua kumbe MABADILIKO yanawezekana, kumbe CCM sio baba wala mama yao, wamegundua kumbe CCM inaweza kutoka madarakani tena kirahisi kabisa, wamegundua kumbe CCM ni waoga sana na wepesi kabisa, wamegundua kumbe CCM ikizidiwa hadi Pushup zinaweza kupigwa majukwaani.
Na bado unawafungua macho zaidi watanzania.
 
Back
Top Bottom